Wanazuoni wengi zaidi wanakubaliana ya kuwa sura hii surat At-Takaathur ilishuka Makka, na hizi ndio sababu za kushuka kwa sura hii
SURAT AT-TAKAATHUR
Wanazuoni wengi zaidi wanakubaliana ya kuwa sura hii ilishuka Makka. Imam Bukhari anaeleza ya kuwa ilishuka Madina. Lakini sahaba mmoja, Ibni Abbas, anasema ya kuwa ilishuka Makka. Neno Takaathur anasema Ibn Abbas maana yake ni tamaa nyingi ya mali na watoto (Bukhari). Abu Huraira anasimulia ya kuwa Mtume s.a.w. aliposoma sura hii alisema, "Mwanadamu anasema, hii ni mali yangu, hii ni mali yangu. Kumbe aliyokula na kuvaa ameichakaza, aliyotoa katika njia ya Mwenyezi Mungu, ndiyo kaiweka akiba na iliyobaki si yake ni mali ya watu."
Sababu za kushuka sura hii:-
Muqatil na Al-Kalb wamesema “sura hii ilishuka kutokana na makabila mawili ya Kikurayshi, ambayo ni Banu Abd Manafi na Banu Sahm. Kila kabila lilikuwa likijisifu na kujigamba juu ya lingine. Hivyo ikafikia hadi wakaanza kuheabu ni kabila lipi lina machifu wengi na viongozi wengi kuliko lingine. Banu Abd Manafi walikuwa wakisema “sisi tuna machifu wengi, viongozi wengi na hata kabila letu lina watu wengi”. pia banu Sahm walikuwa wakisema hivyohivyo. Basi baada ya kuhesabu ikaonekana kweli Banu Abd Manafi wana watu wengi kwenye kabila lao. Baada ha yapo wakasema “twendeni tukahesabu makaburi ya watu wetu waliokufa. Hivyo wakayaendea makaburi hapo wakaata jibu kuwa Banu Saham ni wengi waliokufa kuliko Banu Abd Manafi.
Qatada amesema kuwa sura hii ilishuka kuwahusu Mayahudi waliosema “sisi ni wengi ssana kuliko wakina fulani na fulani ….., hivyo walikuwa wakiendelea na madai yao haya na kujisahau, kumuasi mungu hadi mauti anawafikia.
‹ Nyuma
› Endelea
‹ Books
‹ Apps ››
Umeionaje Makala hii.. ?
Sura hii ni miongoni mwa Sura fupi sanya huwenda ndiosura yenye aya chache kuliko sura zote katika Quran.
Soma Zaidi...Kama tulivyoona kuwa id-ghamu ipo katika aina kuu mbili ambazo ni id-ghamu bighunnah na id-ghamu bighair ghumnah. Sasa hapa tutajifunza makundi mengine ya idhgamu.
Soma Zaidi...