Dai kuwa Muhammad (s.a.w) aliitunga Qur-an ili Kuwania Madaraka na Ukubwa

(x) Dai kuwa Muhammad (s.

Dai kuwa Muhammad (s.a.w) aliitunga Qur-an ili Kuwania Madaraka na Ukubwa

(x) Dai kuwa Muhammad (s.a.w) aliitunga Qur-an ili Kuwania Madaraka na Ukubwa:



Aidha, fikra kuwa huenda Muhammad (s.a.w) aliitunga Qur-an kwa sababu aliwania ukubwa na madaraka pia ni vigumu sana kuithibitisha, kwa sababu zifuatazo:
Kwanza, Muhammad (s.a.w) alijulikana sana ulimwengu mzima kama kiongozi aliyefanikiwa sana katika historia ya binaadamu. Mtu mwenye sifa kama hizo angeweza kuchukua uongozi na madaraka bila hata kudai kwanza utume. Kwa hakika kufanya hivyo kungekuwa rahisi zaidi kwake kama alikuwa anataka madaraka kuliko kudai utume kwanza.



Pili, Qur-an imetamka wazi wazi kuwa hakuna mtu yeyote ikiwa ni pamoja na Muhammad (saw) mwenyewe awezaye kuleta mfano wake. Kama lengo lake lilikuwa kupata utukufu miongoni mwa watu angejitapa kuwa ndiye mtunzi wa kitabu hiki kinachovishinda vitabu vyote.



Hata hivyo tabia yake haikuonesha dalili zozote za mtu anayepigania madaraka au utukufu. Kupenda madaraka na utukufu kwa kawaida kunajionesha kwa mtu kutaka majumba ya fahari ya kifalme, nguo za kipekee,kutaka kusifiwa na kuabudiwa na watu, n.k. Muhammad (s.a.w) alionesha mfano wa ajabu kabisa wa unyenyekevu. Pamoja na amana kubwa ya unabii aliyokuwa nayo na dhamana kubwa sana ya kuongoza dola ya Kiislamu, Muhammad (s.a.w) alikuwa akisaidia kufanya kazi ndogo ndogo za nyumbani. Akishona nguo zake na kuripea viatu vyake na akimkama mbuzi wake. Alikuwa akimsikiliza kwa makini kila aliyemwendea, kiasi ambacho Qur-an imesema makafiri walikuwa wakilalamika kwanini anawasikiliza hata wanyonge (Qur-an 9:61).



Wakati fulani Waislamu walikuwa wanasimama walipotaka kumwamkia kama ishara ya heshima. Lakini aliwakataza na kuwaambia, β€œMsisimame kama Waajemi wanavyofanya, baadhi yao kuwatukuza wengine.”


Mifano mingine ya unyenyekevu wake ni ile iliyotajwa na mwanachuoni maarufu Dk. Gamal Badawi:
Siku moja Mtume Muhammad (s.a.w) alikuwa akisafiri pamoja na baadhi ya maswahaba wake ambao njiani walipiga kambi na kuanza kupika chakula kwa kugawanya kazi za kufanya. Muhammad (s.a.w) alichagua kazi ya kutafuta kuni.Maswahaba wake wakamwambia asifanye kazi yoyote kwani wao watamfanyia. Muhammad (s.a.w) akawajibu, "Najua kuwa mnaweza kunifanyia lakini nachukia kupewa nafuu kuliko nyinyi."



Mfano mwingine ni huu:
Mtu mmoja alimwendea Mtume (s.a.w) huku akitetema kwa kumheshimu. Muhammad (s.a.w) alimwomba mtu yule amsogelee na akamkumbatia na kumpigapiga mgongoni kwa huruma kubwa, halafu akamwambia, 'Tulia ndugu yangu, mimi ni mtoto wa mwanamke aliyekuwa anakula mkate mkavu.'



Aidha imeripotiwa kuwa baadhi ya watu walimwendea Mtume (s.a.w) na wakamsifu kwa kusema: "Ewe Mjumbe wa Allah(sw), wewe u-mbora kuliko sote na wewe ni mtoto wa mbora wetu, wewe ni kiongozi wetu na ni mtoto wa kiongozi wetu. Jibu lake lilikuwa:



Enyi watu, semeni lile mlilolisema mwanzo (yaani "Ewe Mjumbe wa Allah, ") na msikubali shetani awapotezeni. Mimi ni Muhammad, mja wa Allah na Mjumbe wake. Sipendi nyinyi muiinue daraja yangu kuliko ile daraja ambayo Allah (s.w) amenipa.



Vile vile ilisadifu kwamba kifo cha mwana mpenzi wa Muhammad (s.a.w) aliyeitwa Ibrahim kilitokea na jua likapatwa. Watu wakasema huo ni mwujiza utokao kwa Allah unaoonesha kuwa mbingu na ardhi zina majonzi kuhusiana na kifo cha Ibrahim.


Aliposikia maneno hayo, Muhammad (s.a.w) alikasirika sana akasema: "Jua na mwezi ni dalili mbili miogoni mwa dalili nyingi za Allah (s.w). Jua na mwezi havipatwi kwa sababu ya kufa au kuzaliwa mtu yeyote."



Mifano yote hii inaonesha kuwa madai kwamba Muhammad (s.a.w) aliitunga Qur-an ili ajipatie madaraka na utukufu pia hayana nguvu.
Kwa nini kwa mfano, atunge kitabu kinachomwamuru yeye mwenyewe awatangazie watu wote kuwa yeye hana uwezo wowote wala hana elimu ya ghaibu na kwamba lau angekuwa nayo angejizidishia heri zote na shari isingemgusa(Qur-an 7:188)? Au kwanini aandike kitabu kinachomwamuru aseme kwamba hakuja na itikadi mpya na kwamba hata hakutazamia kuwa kitabu kama hiki kingefunuliwa kwake na hivyo awaambie watu kuwa yeye ni mtu kama watu wengine? (Qur-an 46:9, 28:86, 8:110 na 6:50).



Pili, hisia za Muhammad (s.a.w) baada ya kupata wahy mwanzo zaonyesha kuwa hakuwa anawania ukubwa kisiri siri. Baada ya yaliyomtokea katika pango la Hira alirejea haraka kwa mkewe hali ya kuwa anatetemeka kwa hofu kana kwamba alikuwa na homa kali. Akamwomba mkewe amfunike nguo nzito. Baada ya hofu kumwondoka akamsimulia mkewe yote aliyoyaona kisha akasema: 'Ewe Khadijah, ni lipi linalotaka kunisibu?'Ni dhahiri kuwa kama kusingizia kupata wahy ilikuwa ni mbinu tu ya kujipatia ukubwa Muhammad (s.a.w) asingehofia chochote. Ushahidi uliopo unaonesha kuwa hakupanga apate wahy wala hakutegemea kupata wahy. Alijistukia tu analetewa wahy. Na juu ya jambo hili Qur-an yasema:


Nawe hukuwa unatumai ya kwamba utaletewa Kitabu, lakini ni rehema ya Mola wako. (28:86)


Tatu Jambo jingine linalozidi kudhihirisha kuwa Muhammad (s.a.w) hakuwania ukubwa na utukufu ni kule kukataa kwake alipopewa pendekezo hilo na Maquraishi.
Wakati ambapo Waislamu walikuwa wakibughudhiwa na kuteswa, Machifu wa Maquraishi wa Makka walimtaka Muhammad (s.a.w) aache kuhubiri dini ya Uislamu na wao watampatia alitakalo miongoni mwa yafuatayo:
(1)Kama anataka mali watampatia mali nyingi hadi awe tajiri kuliko watu wote.
(2)Kama anataka utukufu, watamfanya bwana wao na hawataamua lolote bila ridhaa yake.
(3)Kama anataka ufalme, watamfanya awe mfalme wao, na
(4)Kama amepagawa na pepo na ameshindwa kumwondoa mwilini mwake wao watamtafuta mganga atakayemtibu kwa gharama yoyote.



Lakini Muhammad (saw) aliyakataa yote hayo na badala yake akamsomea mjumbe aliyetumwa kumletea mapendekezo hayo, Utbah ibn Rabia, aya ya 1-38 ya Sura ya 41.




                   


Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Quran Main: Dini File: Download PDF Views 685

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
πŸ‘‰1 Kitau cha Fiqh    πŸ‘‰2 Bongolite - Game zone - Play free game    πŸ‘‰3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    πŸ‘‰4 kitabu cha Simulizi    πŸ‘‰5 Kitabu cha Afya    πŸ‘‰6 Simulizi za Hadithi Audio   

Post zinazofanana:

mafunzo ya TAJWID na imani ya dini ya kiislamu

Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa

Soma Zaidi...
mgawanyiko katika quran

MGAWANYIKO KATIKA QURAN Juzuu, Sura, Aya, Manzil, Qara Wataalamu wa elimu za Qurani katika fani za uandishi na usomaji wameigawanya Qurani katika mafungu ili kuwezesha urahisi kwa wasomaji wa qurani.

Soma Zaidi...
Hukumu ya tafkhim na tarqiq katika usomaji wa Quran tajwid

Tarqiq ni kuisoma herufi kwa kuipa wepesi na tqfkhim ni kuisoma herufi kwa kuipa uzito.

Soma Zaidi...
Sababu za kushukasurat an Nasr

Sura hii ni katika sura za mwisho kushuka, huwendakuwa ndio ya mwisho kabisa. Masahaba waliamini kuwa sura hii imetabiri kifo cha Mtume S.A.W

Soma Zaidi...
IDGHAAM KATIKA LAAM

Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa

Soma Zaidi...
HUKUMU YA NUN SAKINA NA TNWIN

Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa

Soma Zaidi...
Sababu za kushuka surat al Quraysh

Qurayh ni jina la kabila la Mtume Muhammad S.A.W. Sura hii itakwenda kukujulisha neema ambazo Maquraysh wamepewa na hawataoewa wao wowote baada ya wao.

Soma Zaidi...
Uthibitisho kuwa Qur-an ni neno la Allah (s.w)

Uthibitisho kuwa Qur-an ni neno la Allah (s.

Soma Zaidi...
Quran si Mashairi kama wanavyodai makafiri

(i)Dai kuwa Qur-an ni Mashairi aliyotunga Muhammad (s.

Soma Zaidi...
Sababu za kushuka kwa surat al-Fiil

SURAT AL-FIILSura hii imeteremshwa Makkah na ina Aya Sita pamoja na Basmallah.

Soma Zaidi...