Haikufundisha Mtume Muhammad quran kwa lengo la kurekebisha tabia za waarabu

Haikufundisha Mtume Muhammad quran kwa lengo la kurekebisha tabia za waarabu

(viii)Dai la Kurekebisha Tabia ya Waarabu:



Miongoni mwa wale wanaosema kuwa Muhammad (s.a.w) ndiye aliyetunga Qur-an wapo wanaodai kuwa Muhammad (s.a.w) alifanya hivyo kwa nia nzuri ya kutaka kujenga tabia na mwenendo mzuri miongoni mwa ndugu zake Waarabu. Yaani, Muhammad (s.a.w) alichukizwa sana na tabia mbaya walizokuwa nazo


Waarabu wa zama zake na hivyo akaona lazima ajitahidi kuziondoa. Na ili afanikishe lengo lake hilo akaona atunge Qur-an na asingizie kuwa inatoka kwa Allah (s.w). Dai hili pia halina nguvu kwa sababu zifuatazo:



Kwanza, kujenga mwenendo mzuri wa tabia za watu ni jambo jema ambalo laweza kutekelezwa pasi na kutumia udanganyifu na uovu mwingine. Ni kipi kilichomfanya Muhammad (s.a.w) atumie uwongo na udanganyifu ili awafundishe watu kuwa wa kweli na waaminifu?



Pili, Qur-an imeitaja dhambi ya kuzua uwongo kuwa ni miongoni mwa madhambi makubwa:


"Na nani dhalimu mkubwa kuliko yule amtungiaye uwongo Allah au mwenye kusema: "Nimeletewa wahyi," na hali hakufunuliwa chochote; na yule asemaye: "Nit ateremsha (ufunuo) kama ule aliouteremsha Allah." Na kama ungewaona madhalimu watakapokuwa katika mahangaiko ya mauti, na Malaika wamewanyooshea mikono yao (na kuwaambia): "Zitoeni roho zenu! Leo mtalipwa adhabu ifedheheshayo kwa sababu ya yale mliyokuwa mkiyasema juu ya Allah pasipo haki na kwa vile mlivyokuwa mkizifanyia kiburi Aya zake." (6:93)



Aya hii inasema hakuna dhalimu mkubwa kuliko yule mtu ambaye atamzulia uwongo Allah au atakayesingizia kuwa amepata wahyi kutoka kwa Allah na ilhali hakupata.Halafu aya hii inataja jinsi watu wa aina hiyo watakavyofedheheshwa na jinsi watakavyopapatika wakati wa kutolewa roho zao.



Lau kama Muhammad (s.a.w) angekuwa ndiye aliyeitunga halafu akamsingizia Allah (s.w), asingeiweka aya kama hii katika Qur-an kwa sababu angehisi kuwa anajitukana mwenyewe na kujilaani mwenyewe. Pia kwa kuhofia kuwa yaweza kutokezea siku ambayo watu watamgundua angehakikisha kuwa anaiandika aya hii kwa namna ambayo haitamfedhehesha hapo atakapojulikana.



Angeweza kwa mfano kusema: "Hapana lawama kwa wale ambao, ikiwa hapana budi kusema uwongo kwa ajili ya Allah." St. Paulo kwa mfano ameandika hivi katika Biblia:
Lakini ikiwa kweli ya Mungu imezidi kudhihirisha utukufu wake kwa sababu ya uongo wangu, mbona mimi ningali nahukumiwa kuwa ni mwenye dhambi." (Warumi 3:7)
Aidha madai kuwa Muhammad (s.a.w) alitunga Qur-an ili aitumie katika kurekebisha mwenendo wa tabia za watu pia yanatenguliwa na ukweli kwamba Qur-an haikushuka yote mara moja bali ililetwa kidogo kidogo kwa muda wa miaka 23. Na katika kipindi hicho Qur-an ilitoa ahadi ya kujibu maswali yote yatakayoulizwa wakati Qur-an bado inashuka.


Na kama mtayauliza, maadam inateremshwa Qur-an mtabainishiwa " (5:101)
Watu waliitumia fursa hiyo iliyotolewa na Qur-an kuuliza maswali mbali mbali kama vile juu ya ulevi, kamari, hedhi, ngawira, roho na hata juu ya watu kama Dhur-qarnain. Katika kuyajibu maswali hayo


Qur-an imetumia msemo "Wanakuuliza juu ya jambo kadhaa. Sema: Lipo namna kadhaa." Kwa mifano halisi tazama Qur-an 2:189, 2:215, 2:217, 2:219, 2:220, 2:222, 5:4, 7:187, 8:1, 17:85, 18:83, 20:105 na 79:42.



Tatizo linalojitokeza hapa ni kwamba Muhammad (s.a.w) asingeweza kujua kuwa maswali aliyowaruhusu watu kuuliza yatakuwa yanahusu marekebisho ya mwenendo na tabia za watu. Kwani inadaiwa kuwa haitakuwa jambo la busara kwa rais anayetaka kuzungumzia hali ya chakula nchini mwake kuwaita waandishi wa habari na kuwaruhusu waulize maswali yoyote yanayowatatiza. Rais huyo atakuwa na hakika gani kuwa watauliza juu ya hali ya chakula na siyo juu ya wafungwa wa kisiasa?




                   


Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 103

Post zifazofanana:-

STANDARD FOUR ENGLISH TEST 005
SECTION A: DICTATION. Soma Zaidi...

fadhila za sura kwenye quran
FADHILA ZA BAADHI YA SURA Umuhimu na ubora wa baadhi ya sura na aya. Soma Zaidi...

lengo la kuswali za faradhi na suna
Soma Zaidi...

HUKUMU ZA IDGHAM
Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa Soma Zaidi...

Maradhi ya Ini na dalili zake, na vipi utajikinga nayo
MAGONJWA YA INI NA DALILIZAKE, NA KUKABILIANA NAYO Ini ni katika viungo vikuu katika mwili wa binadamu. Soma Zaidi...

Uthibitisho kuwa Qur-an ni neno la Allah (s.w)
Uthibitisho kuwa Qur-an ni neno la Allah (s. Soma Zaidi...

surat al mauun
SURATUL-MAM'UUN Imeteremshwa Maka, anasimulia Ibn Jurayj kuwa Abuu Sufyan ibn Harb alikuwa na kawaida ya kuchinja ngamia wawili kila wiki, hivyo siku moja yatima mmoja alikuja kwake na kumlilia shida, na hakumsaidia kwa chochote na hatimaye akampiga yat.. Soma Zaidi...

Zijuwe aina za swala za Suna na namna za kuziswaliWitri, Dhuha, Idi, tarawehe, tahajudu na nyingine
Soma Zaidi...

Chemsha bongo namba 09
16. Soma Zaidi...

Sababu za kushuka kwa surat al-Fiil
SURAT AL-FIILSura hii imeteremshwa Makkah na ina Aya Sita pamoja na Basmallah. Soma Zaidi...

Milki ya raslimali katika uislamu
Milki ya RasilimaliIli kujipatia maendeleo ya kiuchumi katika zama zote mwanaadamu anahitaji rasilimali za kumwezesha kufikia azma hiyo. Soma Zaidi...

Waliomuamini Nabii Nuhu(a.s)
Waliomuamini Nuhu(a. Soma Zaidi...