Al fiyl ni neno la Kiarabu lenye maana ya tembo. Sura hii inazungumziakisa cha jeshi lenye tembo. Jeshi hili lilikuwa na nia ya kuvunja al qaaba
SURAT AL-FIIL
Sura hii imeteremshwa Makkah na ina Aya Sita pamoja na Basmallah. Sura hii imeshuka ili kueleza kuhusu tukio la kuangamizwa kwa jeshi la tembo. Na hii ni katika sura ambazo zinataja neema ambazo wamepewa Maquraysh, nao ni ule ushindi dhidi ya Makafiri walotaka kuvunja Al-Ka’abah. Tukio hili limeelezwa kwa kirefu kwenye vitabu vya Sirah na hapa nitaleta kwa ufupi zaidi
Kiongozi mmoja wa kiyemeni aliyetambulika kwa jina la Abrah aliona waarabu kutoka maeneo mbalimbali wanafunga misafara kuelekea Makkah kwa lengo la kwenda kuhiji. Hivyo akaamuwa kujenga kanisa kubwa sana ambalo alifikiri kuwafanya waarabu wasiende Makkah ila waende kuhiji kwenye kanisa lake. Kulikuwa na kijana mmoja kutoka katika kabila la Kinana alifahamu jambo hili la Abraha. Hivyo akaingia kwenye kanisa wakati wa usiku kisha akachafua ukuta wa kanisa kwa kuupaka vinyesi. Abraha alipolijuwa jambo hili akaandaa jeshi kubwa sana ili akaivunje Al-ka’aba. Jeshi la Abraha lilikuwa na washujaa elfu sitini (60,000). kisha akachaguwa tembo aliye mkubwa ndio akampanda yeye. Katika jeshi hili kulikuwa na tembo kati ya tisa mpaka kumi na tatu. (9-13)
Safari ya Abraha iliendelea mpaka akafika sehemu inayoitwa Magmas. Na hapo ndipo akaliweka sawa jeshi lake na akaliweka tayari kwa kuingia Makkah. Akaendelea mpaka akafika sehemu iitwayo Bonde la Muhassar bonde hili lipo kati ya Muzdalifah na Mina. Na hapo ndipo tembo wa abraha akakataa kuendelea na safari. Tembo alipiga magoti na kukaa chini, na kugoma kabisa kuelekea upande wa Makkah. Basi akimuelekeza upande mwingine anakubali lakini pindi akimuelekeza upande wa Makkah anagoma kabisa.
Na hapo ndipo Allah alipoleta jeshi la ndege waliobeba vijiwe vya moto na kuwapiga nvyo jeshi la Abraha. Ndege hawa kila mmoja alibeba vijiwe vitatu, kijiwe kimoja kwenye mdomo na viwili kwenye miguu yao. Kila kijiwe kiliuwa mtu katika jeshi la Abraha. Kuna wengine walikufa palepale na wengine walikimbia na kufia mbele ya safari. Abraha alibahatika kukimbia kwani alijeruhiwa vibaya, alipofika sehemu iitwayo San’a hali yake ikawa mbaya zaidi na akafariki.
Kwa upande mwingine wakazi wa Makkah walikimbia mji na kujificha kwenye majabali. Na huu ni ushauri walopewa na kiongozo wao Abdul Al-Muttalib. Baada ya maombi waloyaomba kwa Allaha na hatimaye wakamuachia Allah ailinde Nymba yake na wao wanusuru maisha yao. Basi jeshi la Abraha baada ya kuangamizwa wakazi wa Makkah wakarudi majumbani kwao wakiwa salama.
Tukio hili lilitokea mwezi wa Muharram siku hamsini aua hamsini na tano kabla ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (s.a.w) ambapo ni sawa nan Mwezi wa Pili au mwanzoni mwa Mwezi wa Tatu mwaka 571 B.K. na hii ilikuwa ni zawadi kutoka kwa Allah kwenda kwa mtume wake na watu wa familia yake. Na hapo ndipo Nyumba ya Allah yaani Al-ka’aba ilipata maarufu kwa utukufu wake. Na mwaka huu waarabu wakauita mwaka wa Tembo
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowJe umeipenda post hii ?
Sababu za kuteremshwa baadhi ya sura Katika darsa hii tutaangalia sababu za kushuka kwa aya na sura ndani ya quran.
Soma Zaidi...Qur-an inavyogawa MirathiMgawanyo wa mirathi umebainishwa katika Qur-an kama ifuatavyo:Mwenyezi Mungu anakuusieni juu ya watoto wenu: Mwanamume apate sawa na sehemu ya wanawake wawili.
Soma Zaidi...Surat al Baqarah ni katika sura ambazo tunapaswa tuwe tunasoma mara kwa mara. Post hii itakufundisha kuhusu fadhila za sura hii.
Soma Zaidi...Kama tulivyoona kuwa id-ghamu ipo katika aina kuu mbili ambazo ni id-ghamu bighunnah na id-ghamu bighair ghumnah. Sasa hapa tutajifunza makundi mengine ya idhgamu.
Soma Zaidi...waqfu ni misimamo ambapo msomaji wa Quran anaruhusiwa kusimama, kuhema au kumeza mate. Na ibtidai ni kuanza baada ya kutoka kwenye waqf
Soma Zaidi...Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa
Soma Zaidi...