Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa
SURA YATISA
HUKUMU ZA WAQFU AL-IBTIDAI
l-Waqfu Wal-Ibtidaai β Kisimamo Na Kianzio
Msomaji si kwamba muda wote atakuwa anasoma bali, wakati mwingine anapumzika, au anasimama kidogo kumeza mate au kupumua ana atakata kabisa kusoma. Hivyo hapa kuna kauli tatu ambazo inatupasa tuzijue kabla ya kuenddelea. Kauli hizo ni;-
1.Al-waqfu: maana yake ni kisimamo nako ni kukata kusoma kwa muda wa kawaida kwa ajili ya kuvuta pumzi huku msomaji akiwa na nia ya kuendelea kusoma.
2.Al-sakt:maana yake ni kipumziko nako ni kupumzika kwa muda kwa kiasi cha haraka mbili huku msomaji akiwa na nia ya kuendelea kusoma.
3.Al-qatwβu;maana yake ni ukataji nako ni kusimama kusoma kwa lengo la kumaliza kusoma. Hapa inabidi mtu amalize kusoma kwake mwishoni mwa aya au sura. Na inatakikana pindi anapotaka kuendelea kusoma aanze na istiβadha
ALAMA ZA WAQFU KATIKA QURAN:
1.aAlama hii(Ψ΅ΩΩ) inamaanisha inajuzu kuunganisha.
Yaani pindi msomaji anapokuta alama hii anaweza kuunganisha maneno hayo, yaani neno la nyuma na maneno yanayofata. Hivyo hapa msomaji ana hiyari ima kuunganisha au kusimama (kufanya waqfu).
2.Alama hii (ΩΩΩ) inamaanisha inajuzu kusimama.
Yaani pindi msomaji anapokuta alama hii atakuwa na hiyari ya kusimama.
3.Alama hii (Ψ¬) inamaanisha inajuzu kusimama ila kwa ufupi. Yaani msomaji anapokutana na alama hii ataweza kusimama hapa, ila usimamaji wake usiwe mrefu.
4.Alama hii (Ω
) inamaanisha kusimama kwa lazima. Yaani msomaji anapokutana na alama hii kusimama kwake ni kwa lazima.
Alama hii (ΩΨ§) inamaanisha hairuhusiwi kusimama sehemu hii. Hii inamaanisha msomaji hatakiwi kusimama pindi anapokutana na alama hii.
Umeionaje Makala hii.. ?
Sura hii inaonya vikali tabia ya kusengenya na kusambaza habari za uongo. Wameonywa vikali wenye tabia ya kujisifu kwa mali, kukusanya mali bila ya kuitolea zaka.
Soma Zaidi...Al fiyl ni neno la Kiarabu lenye maana ya tembo. Sura hii inazungumziakisa cha jeshi lenye tembo. Jeshi hili lilikuwa na nia ya kuvunja al qaaba
Soma Zaidi...Mada zipo katika makundi mawili ambayo ni madda far-iy na mdada twab-iy.
Soma Zaidi...Je unajuwa ni kwa nini unatakiwa usikose kusoma surat al Kahaf siku ya ijumaa. Makala hii itakujibu swali hili
Soma Zaidi...Hapa utajifunza kanuni za tajwid katika kusoma bismillah au basmalah.
Soma Zaidi...(x) Dai kuwa Muhammad (s.
Soma Zaidi...