image

Dai kuwa Muhammad Alitunga Qur-an ili Ajinufaishe Kiuchumi

)Dai kuwa Muhammad Alitunga Qur-an ili Ajinufaishe Kiuchumi

(ix)Dai kuwa Muhammad Alitunga Qur-an ili Ajinufaishe KiuchumiBaadhi ya watu wanasema kuwa Muhammad (saw) ndiye mtunzi wa Qur-an na alifanya ili ajinufaishe kiuchumi. Wanasema kuwa yawezekana kuwa Muhammad (s.a.w) aliitunga Qur-an lakini akasema imetoka kwa Allah ili ajipatie manufaa makubwa zaidi. Kama tunazungumzia uwezekano, ni kweli kuwa uwezekano kama huu unaweza kuwepo. Swali la kujiuliza ni hili:Ni manufaa gani hasa ambayo Muhammad (s.a.w) tuseme alikuwa akiyawania? Manufaa hayo yanaweza kuwa ni wasaa wa mali, mamlaka, au ufalme. Hebu tuyafuatilie zaidi madai haya.Muhammad hakuwa tajiri baada ya Utume
Kusema kuwa Muhammad (s.a.w) aliitunga Qur-an ili ajinufaishe maana yake ni kuwa Muhammad (s.a.w) alikuwa mrongo aliposema Qur-an inatoka kwa Allah (s.w). Madai kuwa Muhammad (s.a.w) alikuwa mwongo yanakwenda kinyume na ushahidi wa historia ya maisha yake. Hata hivyo kwa sababu za kutaka kuendeleza mjadala na utafiti wetu, hebu na tuuweke kando ukweli na uaminifu wa Muhammad (s.a.w) na tuchunguze alijinufaishaje kwa kudai kuwa Qur-an ni neno la Allah(s.w).


Tukianza na hali yake kiuchumi tunaona kuwa alikuwa na hali nzuri kabla kuliko baada ya kupata utume. Kabla ya kupata utume, alipokuwa na umri wa miaka 25 alimwoa bibi Khadija ambaye alikuwa ni mfanyabiashara tajiri sana. Muhammad (s.a.w) aliishi naye kwa wasaa mkubwa na pasi na dhiki yoyote. Baada ya kupata utume hali yake kiuchumi ilikuwa ngumu kwa kuwa karibu mali yote ilitumika kuwasaidia Waislamu wachache waliokuwa wakiteswa na kubughudhiwa na makafiri wa Makka. Na hata baada ya kusimama dola ya Kiislamu hali ya kiuchumi ya Muhammad (s.a.w) ilikuwa ndio ngumu zaidi.Baadhi ya mifano ya hali yake kiuchumi
Katika kitabu cha Hadith cha An-Nawawi, mmoja wa wakeze Mtume (s.a.w) Bibi Aisha (r.a) amesema kuwa wakati mwingine ulipita mwezi mzima au hata miezi miwili pasi na moto kukokwa katika nyumba ya Mtume (s.a.w) kwa sababu hakukuwa na cha kupika. Walikuwa wakiishi kwa kula tende na kunywa maji. Wakati mwingine walipata maziwa ya mbuzi kutoka kwa watu wa Madina.Katika kitabu cha maisha ya Muhammad (s.a.w) kilichoandikwa na Martin Lingas1 imeelezwa kuwa Mtume (s.a.w) na familia yake walikuwa wanaishi katika hali ngumu sana kiuchumi. Wakati mwingine hawakupata japo hizo tende za kutosha.Hali hii haikuwa ni matatizo ya kupita tu bali ilikuwa ndio mwenendo wa kudumu wa maisha. Mtume (s.a.w) aliishi katika hali hiyo wakati ambao angeweza kuishi kama mfalme kama angetaka. Kwa hakika ni kutokana na kuamua kwa makusudi kuishi maisha hayo pamoja na kuwa angeweza kuishi maisha ya anasa ndipo wakeze Mtume (s.a.w) wakaja juu. Kwa nini waendelee kuishi maisha ya dhiki na hali wanaweza kuishi kwa wasaa? Mtume alitatizwa na manung'uniko hayo ya wakeze.Allah(sw) akamteremshia wahyi uliomwamuru awaambie wakeze ama wamchague Allah(s.w) na Mtume wake au starehe ya kupita ya ulimwengu huu:


Ewe Mtume! Waambie wake zako. "Ikiwa mnapenda maisha ya (hii) dunia na uzuri wake, njooni, nitakupeni kitoka
nyumba, na kukuacheni muwachano mzuri. Na kama mnamtaka Allah na Mtume wake na nyumba ya Akhera, basi Allah amewaandalia wafanyao mema hayo, miongoni mwenu, malipo makubwa." (33:28-29)Kuhusiana na jinsi chumba cha Mtume kilivyokuwa Umar (r.a) anasema:
Niliona kuwa mali yote iliyokuwa chumbani mwake ilikuwa ni vipande vitatu vya ngozi na fungu dogo la shayiri lililokuwa katika koa. Nikaangaza huku na huko lakini sikuona kitu kingine chochote. Nikaanza kulia. Akaniuliza: Kwanini unalia? Nikajibu: 'Ewe Mjumbe wa Allah! Kwanini nisilie? Naona alama ya mkeka katika mwili wako, na naangalia pia mali yote uliyo nayo katika chumba hiki. Ewe, Mjumbe wa Allah! Mwambie Allah atuzidishie riziki, Waajemi na Warumi ambao hawana imani ya kweli na ambao hawamwabudu Allah bali wafalme wao - akina Kaizari - wanaishi katika mabustani yanayopita mito kati yao, lakini Mjumbe mteule na mja wa Allah akaishi katika umasikini kama huu!' Mtumealikuwa amejipumzisha hali ya kuwa amelalia mto, lakini aliponisikia nikisema hivyo, akaketi na kusema; 'Ewe Umar! Je, bado una shaka juu ya jambo hili? Raha na starehe za akhera ni bora kuliko raha na starehe za ulimwengu huu. Makafiri wanafaidi starehe zao zote hapa duniani na sisi tutakuwa na starehe zetu zote huko akhera.' Nikamwomba Mtume kwa kusema: 'Ewe Mjumbe wa Allah! Niombee msamaha kwa Allah. Kwa hakika nilikosea.'Alipoulizwa juu ya kitanda cha Mtume (s.a.w) kilivyo, Bibi Aisha alijibu: 'Ni ngozi iliyojazwa magome ya mitende.'
Ikumbukwe kuwa Muhammad (s.a.w) aliishi maisha ya namna hiyo kwa hiari yake kwa sababu kila alipopata zawadi aliigawa yote kwa mafakiri pasi na yeye mwenyewe kuchukua chochote. Safari moja alipewa na Chifu wa Fidak zawadi zilizobebwa na ngamia wanne, lakini alizigawa zote.Wakati wa kutawafu kwake Muhammad (s.a.w) hakuwa na hata senti moja mfukoni.Alikuwa na dinari saba karibu ya kufariki kwake lakini akazigawa kwa maskini kabla ya kufariki. Isitoshe alipofariki, pamoja na ushindi mkubwa alioupata katika vita na pamoja na kuwa alikuwa ndiye kiongozi wa dola ya Kiislamu, Muhammad (s.a.w) alikuwa akidaiwa na ngao yake ilikuwa mikononi mwa Myahudi mmoja wa Madina kama rehani ya deni hilo.Ipo mifano mingine mingi inayoonesha kuwa katika kipindi chake chote cha utume, Muhammad (s.a.w) aliishi katika maisha ya kujinyima. Kutokana na ushahidi huu unaotokana na historia ya maisha yake, ni wazi kuwa madai kuwa Muhammad (s.a.w) aliitunga Qur-an ili apate kujinufaisha kiuchumi hayana msingi.


1. Muhammad His Life Based on the Earliest Scurces


                   
           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 213


Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Hukumu ya Ikhfau katika tajwid
Ikh-fau ni moja ya hukumu za nun sakina na tanwin kwenye hukumu za Quran tajwid Soma Zaidi...

quran na sayansi
YALIYOMONENO LA AWALI1. Soma Zaidi...

HUKUMU ZA MADD
Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa Soma Zaidi...

Sababu za kushuka surat al-Fiyl
Al fiyl ni neno la Kiarabu lenye maana ya tembo. Sura hii inazungumziakisa cha jeshi lenye tembo. Jeshi hili lilikuwa na nia ya kuvunja al qaaba Soma Zaidi...

Ni nini maana ya Tajwid, na ni ipi nafasi yake kwenye uislamu
Hapa utajifunza maana ya Tajwid kilugha na kisheria. Pia nitakujuza jukumu ya kusoma tajwid. Soma Zaidi...

Maswali yanayohusu quran
Quran (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Fadhila za kusoma surat al Fatiha (Alhamdu)
Post hii inakwenda kufundisha fadhila na faida za kusoma Alhamdu. Soma Zaidi...

Saratul-humaza
Quran (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Fadhila za kusoma surat al Kahaf siku ya Ijumaa
Je unajuwa ni kwa nini unatakiwa usikose kusoma surat al Kahaf siku ya ijumaa. Makala hii itakujibu swali hili Soma Zaidi...

quran tahadhari
TAHADHARI KWA WASOMAJI WA QURAN Wasomaji wa qurani wawe na tahadhari katika usomaji wao. Soma Zaidi...

Sababu za kushuka surat Ikhlas
Surat Ikhlas ni katika sura za kitawhid ambazo zilishuka miaka siku za mwanzoni mwa utume. Sura hii imekuja kujibu maswali mengi kuhusu Allah ikiwemo, Allah ni nani? Soma Zaidi...

HUKUMU ZA IDGHAM
Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa Soma Zaidi...