(vi)Madai Kuwa Mtume (s.a.w) Aliandika Qur-an kwa Msaada wa Mayahudi na Wakristo:
Tunakutana na madai mengine kuwa Mtume (s.a.w) aliandika Qur-an baada ya kusoma Biblia au wengine wanadai kuwa alifundishwa na Mayahudi na Wakristo ndio naye akaandika Qur-an kwa kuzingatia wakati na watu aliokuwa nao. Makafiri wa karne hii sio tu walioanzisha madai haya bali madai haya ni makongwe kama ilivyo kongwe Qur-an yenyewe.
Pametolewa madai mengi ya namna hii kuanzia karne hizo za kushushwa Qur-an kwa Mtume (s.a.w) mpaka hivi leo. Hebu tuangalie dai hili la baadhi ya makafiri wa karne hizi za usoni ambalo limegawanyika katika sehemu zifuatazo:
(a)Dai la Kufundishwa na Padri Bahira:
(b)Dai la Kunakili Biblia
(c)Dai la Kufundishwa na Jabir na Yasir:
Kurasa zijazo tutakwenda kuona dai moja moja kati ya haya na udhaifu wake.