Sura hii inaonya vikali tabia ya kusengenya na kusambaza habari za uongo. Wameonywa vikali wenye tabia ya kujisifu kwa mali, kukusanya mali bila ya kuitolea zaka.
SURAT ALHUMAZAH
Sura hii imeteremshwa Maka na ina aya 10 pamoja na bismillah.
Wafasiri wengi wanakubaliana ya kuwa sura hii ilishuka Makka. Hali ya watu wa siku za Mtume s.a.w. waliokuwa wakiwaudhi Waislamu na wakijivuna kwa mali zao, imeelezwa katika sura hii.
Humazah, "Msingiziaji." Neno hili limetoka katika neno hamazah lenye maana ya
kusingizia; kukoneka; kupiga kwa kidole; kusukumu; kupiga; kuuma; kusengenya; kuvunja; kutia wasiwasi.
Lumazah (Msingiziaji) ni neno lililotoka katika lamazah, yaani kusingizia, kuaibisha; na ku- koneka.
Masahaba na watu wa baadaye wamehitilafiana katika maana ya Aya hii, na hakuna sababu yake nyingine isipokuwa ya kwamba maneno haya mawili humazah na lumazah yanakaribiana sana katika maana. Inasemekana ya kuwa Mughira, A'as bin Wail na Sharik walikuwa wakishughulika kila mara kumwudhi Mtume s.a.w. na masahaba kwa kuwasingizia na kuwaaibisha; basi Mwenyezi Mungu katika sura hii akawaonya ya kuwa waache mwendo wao huo waila wataangamizwa.
Lakini hakuna haki ya kusema ya kuwa watu hawa watatu tu ndio walioonywa, maana
wangekuwa ni hao watatu tu, basi wangetajwa majina yao. Lakini badala ya kutajwa majina yao Mwenyezi Mungu amesema, Maangamizo kwa kila msingiziaji, msengenyaji. Hili laonyesha ya kuwa watu wote wenye ada na mwendo wa namna hiyo wameonywa - wawe watu wa zamani, wa leo, hata na wa baadaye - wote watapata adhabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa dhambi zao za kuwasingizia, kuwaaibisha, kuwasengenya na kuwateta watu. Hivyo, Mwenyezi Mungu amewaonya
watu wote wa siku zote ili wasishike njia ya namna hii inayoleta machafuko makubwa kati ya jamii za watu na makabila, na watu wanatenguka nguvu zao na kuangamia kabisa.
Umeionaje Makala hii.. ?
Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa
Soma Zaidi...Kama tulivyoona kuwa id-ghamu ipo katika aina kuu mbili ambazo ni id-ghamu bighunnah na id-ghamu bighair ghumnah. Sasa hapa tutajifunza makundi mengine ya idhgamu.
Soma Zaidi...2:UUMBWAJI KWA MAJI YA UZAZIUumbwaji wa mwanadamu umepitia hatua mbalimbali na haya yote yamefanywa kwa sababumaalumu ili tipate mazingatio.
Soma Zaidi...Qalqala imegawanyika katika makundi mawili ambayo ni Qalqalatul qubra yaani qalqala kubwa na qalqalat as shughura yaani qalqala ndogo.
Soma Zaidi...Qurayh ni jina la kabila la Mtume Muhammad S.A.W. Sura hii itakwenda kukujulisha neema ambazo Maquraysh wamepewa na hawataoewa wao wowote baada ya wao.
Soma Zaidi...