Mambo anayofanyiwa maiti baada ya kufa

Mambo anayofanyiwa maiti baada ya kufa

Dhana ya faradh kwa muislamu (EDK form 2:dhana ya elimu ya uislamu)

Mambo anayofanyiwa mtu (maiti) mara tu baada ya kufa.

Baada ya mtu kufa inatuwajibikia tuseme: “Innalillah wainnailaihraaji’una”. Qur’an (2:156). Kisha kumfanyia maiti mambo yafuatayo:

 

  1. Kwa taratibu kurudishia mdomo wake usiwe wazi kwa kufunga kwa    kitambaa kutoka kidevuni na kuzungushia kichwani.

 

  1. Kufunga macho ya marehemu na huku ukisema; 

“Kwa jina la Allah na kwa kufuata mila ya Mjumbe wa Allah, Ewe Mola wetu mrahisishie mambo yake ya sasa na msahilishie mambo yake ya baadaye. Na jaalia anayokutanayo yawe bora kuliko aliyoyaacha.”

 

  1. Lainisha viungo vyake (miguu na mikono) kwa kukunja na kukunjua taratibu.

       -    Kama kuna ugumu maji ya uvuguvugu au mafuta yanaweza kutumika    kulaisha na kunyoosha viungo hivyo.

      -    Baada ya kulainisha viungo, miguu na mikono inyooshwe na kulazwa uso   ukielekezwa Qibla kwenye mkeka au kitanda kisicho na godoro.  

 

  1. Maiti avuliwe nguo zote alizokufa nazo na kisha kufunikwa kwa shuka kubwa

-    Ni vyema afunwe kitambaa tumboni au kuwekewa kitu kizito ili tumbo lisifutuke.

 

  1. Marashi na ubani vitumike kwa wingi ili kuzima harufu ya uvundo wa maiti.

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Tawhid Main: Post File: Download PDF Views: 2481

Share On:

Share follows: 1 | Unique share links followed: 1
Sponsored links
👉1 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     👉2 ai web app     👉3 Bongolite - Game zone - Play free game     👉4 Kitabu cha Afya     👉5 Madrasa kiganjani     👉6 Dua za Mitume na Manabii    

Post zinazofanana:

Mwanadamu hawezi kuishi bila dini kutokana na vipawa alivyooewa na Allah

Je ni kwa nini mwanadamu hawezi kuishi bila ya kuwa na dini?. Vipawa alivyopewa na Allahni jibu tosha juu ya swali jilo

Soma Zaidi...
Muumini ni yule ambaye anazungumza ukweli

Ukweli ni katika sifa za waumini. Siku zote hakuna hasara katika kusema ukweli. Kinyume chake uongo ni katika madhambi makubwa sana.

Soma Zaidi...
Kujiepusha na kukaribia zinaa

Si zinaa tu iliyoharamishwa bali hata yale yote yanayotengeneza mazingira na kuchochea kufanyika kwa zinaa nayo pia yameharamishwa.

Soma Zaidi...