Yale waumini wanayowajibika kujiepusha nayo kwa mnasaba wa aya tulizozipitia (17:23-40) ni haya yafuatayo:
(a) Kujiepusha na kumshirikisha Allah (s.w)
Kumshirikisha Allah (s.w) ni kujaalia kuwa Allah (s.w) anao washirika wake wanaomsaidia katika kuendesha masuala mbali mbali katika mchakato mzima wa maisha ya dunia. Allah (s.w) hushirkishwa kinadharia na kiutendaji.
Allah (s.w) hushikirishwa kinadharia kwa kujaalia kiumbe kisicho na uwezo wowote, kama vile sanamu, jiwe kubwa, mti mkubwa, majini, malaika, n.k.; kuwa ni mungu na kukielekea kwa maombi na kukitegemea kama apasavyo kuombwa na kutegemewa Allah (s.w). Hii ni shiriki katika Dhati ya Allah (s.w). Pia Allah (s.w) hushirikishwa kinadharia, kwa kumnasibisha na kiumbe au kukipachika kiumbe sifa anazostahiki kusifiwa kwazo. Hii ni shiriki katika sifa za Allah (s.w).
Allah (s.w) hushirikishwa kiutendaji kwa kutiiwa kanuni na sharia na kufuatwa miongozo ya maisha iliyotungwa na watu kinyume na mwongozo wa maisha wa Allah (s.w) kupitia kwa Mitume wake na Vitabu vyake. Kumtii yeyote kinyume na kanuni na sharia za Allah (s.w) ni kumshirikisha Allah (s.w) katika Mamlaka yake. Na kupitisha hukumu yoyote kinyume na alivyohukumu Allah (s.w) ni kumshirikisha katika Hukumu zake. Shirk ndio kiini na chanzo kikuu cha maovu yote duniani na ndio msingi mkuu wa dhuluma (rejea Qur-an 31:13)
Umeionaje Makala hii.. ?
Dhana ya faradh kwa muislamu (EDK form 2:dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Kwenye kipengele hichi tutajifunza mitazamo ya kikafiri juu ya dini.
Soma Zaidi...Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Ndoto za kweli ni moja kati ya njia ambazo Allah huwasiliana na wanadamu.
Soma Zaidi...Huwaoni wale wanaodai kwamba wameamini yale yaliyoteremshwa kwako na yaliyoteremshwa kabla yako?
Soma Zaidi...Nguzo za Imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...