picha

Python somo la 56: Kuongeza Data Katika Database kwa Kutumia Django Admin na Django Shell

Katika somo hili tutajifunza njia mbili muhimu za kuongeza data kwenye database katika project yetu ya pybongo (app: menu). Njia hizi ni: Kutumia Django Admin Kutumia Django Shell Utafahamu pia jinsi ya kusajili models kwenye admin, jinsi ya kuingia admin panel, na namna ya kutengeneza entries mpya za MenuItem.

Utangulizi

Baada ya kutengeneza models na kufanya migrations, hatua inayofuata ni kujaza database kwa data. Django hutupatia njia rahisi na salama za kufanya hivyo. Somo hili litakuongoza hatua kwa hatua jinsi ya kuongeza taarifa za vyakula, bei, muda wa upatikanaji na maelezo kwenye database.


Sasa tuingie kwenye somo letu…

1. Kutumia Django Admin

1.1 Kuanza Admin

Django Admin ni paneli ya kusimamia database bila kuandika SQL yoyote. Lakini ili uitumie:

Hatua ya Kwanza: Tengeneza Superuser

Kwenye terminal:

python manage.py createsuperuser

Utaulizwa:

Hizi ndiyo utatumia kuingia admin panel.


1.2 Kusajili Model Katika Admin

Ili model ionekane kwenye Django Admin, lazima usajili ndani ya admin.py.

Faili: menu/admin.py

from django.contrib import admin
from .models import MenuItem

admin.site.register(MenuItem)

Sasa Django Admin itahusisha model yetu ya MenuItem.


1.3 Kuingia kwenye Admin Panel

Endesha server:

python manage.py runserver

Kisha kwenye browser fungua:

http://localhost:8000/admin/

Ingia kwa username na password ulizounda.

Sasa utaona sehemu ya MenuItem ikiwa ndani ya app menu.


1.4 Kuongeza Data Kupitia Admin