PHP - somo la 18: Jinsi ya kusoma data kutoka kwenye database kwa kutumia PHP
Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kusoma data kutoka kwenye database kwa kutumia PHP.
KUSOMA DATA KUTOKA KWENYE DATABSE KWA KUTUMIA PHP
katika somo liliopita umejifunza jinsi ya kuingiza data kwenye databse. Sasa somo hili nitakujuza namna ya kuzisoma data hizo kwnye ukurasa wa php. hii ni hatuwa muhimu, kwani huwezi ktengeneza blog kama hujui jinsi ya kusoma database kwenye ukurasa wa wavuti.
Maandalizi:
Kma kawaida kwanza tunandaa variable muhimu kwa ajili ya ku connect databse. variable hizo ni servername, database name, username na password. Hivyo variable hizo zitakuwa hizi:
<?php
$servername = "localhost";
$username = "root";
$password = "";
$dbname = "hotel";
$conn = mysqli_connect($servername, $username, $password, $dbname);
?>
Hapo nimekukusanyia variable sa database, server, user na password, pia kuna variable $conn kwa ajili ya ku connect database. Kwa ufupi hapo umesha connect kilichobakia ni kuzisoma data.
Kumbuka tumejifunza SQL ya kusoma daata ni SELECT FROM kisha utaweka jina la table. Mfano wa SQL hii itakuwa ‘SELECT * FROM menu’. kumbuka hiyo * inamaanisha All, yaani data zote.
Hatuwa inayofata ni kutengeneza $sql variable ambayo itahisika kuwakilisha SQL statement ya ku select data (kuzisoa data) kutoka kwenye table menu. hivyo variable hiyo ni kama tulivyotangulia kuiona inaweza kuwa hivi:-
$sql = mysqli_query($conn, "SELECT * FROM `menu` ");
Kinacchofuwata ni kuzinyakuwa hizo data zilizosomwa na php yaani fetching data. Hapa tutatumia method inayoitwa $fetch kwa pamoja hii inakuwa hivi while($fetch = mysqli_fetch_array($sql)){ Tutakuja jifunza zaidi kuhusu while inavyotumika ila kwa ufupi ni kuwa while ni ndugu na if statement. Hapo imetumika kuselect row zote zilizopo kwenye hiyo table. Hii ya mysqli_fetch_array($sql) Hii function hapa imetumika ili kuunganisha $sql variable iliyosoma data na kuzileta kwenye php. Kwa pamoja hapa inatengeneza code hii
<?php
$sql = mysqli_query($conn, "SELECT * FROM `menu` ");
while($fetch = mysqli_fetch_array($sql)){
?>
Hii ndio sasa hutumika kuzisoma data zote za kwenyetable yako. Hiyo SELECT FROM m...
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Dua za Mitume na Manabii 👉2 kitabu cha Simulizi 👉3 Kitau cha Fiqh 👉4 web hosting 👉5 Simulizi za Hadithi Audio 👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
Post zinazofanana:
PHP - somo la 42: Jinsi ya kufanya encryption na de cryption kwa kutumia PHP
Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kufanya encryption na decryption kwa kutumia PHP. hii itakusaidia kuongeza usalama kwenye taarifa za watu
Soma Zaidi...PHP somo la 92: Jinsi ya kuunganisha php na database ya sqlite
Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kutumia database ya sqlite kwa kutumia PHP.
Soma Zaidi...PHP somo la 54: PHP OOP class constant
Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kutumia constatnt kwenye class.
Soma Zaidi...PHP - somo la 27: aina za variable kwenye PHP
Katika somo hili utakwenda kujifunza aina kuu 3 za variable katika PHP mabzo ni local variable, global variable na static variable.
Soma Zaidi...PHP somo la 102: Cron job
atika somo hli tutakwenda kujifunza kuhusu kitu kinachitwa cron job. ni moja ya teknolojia zinazotumika kufanya kazi zinazofanyika automatic
Soma Zaidi...PHP somo la 98: Library za PHP ambazo unaweza kutumia ORM
Somo hili litakwenda kukutajia baadhi ya library za php ambazo hutumika kwa matumizi ya ORM
Soma Zaidi...