Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kuzungumza na server ili kutengeneza mafaili, mafolda, kufuta na ku edit kwa kutumia PHP.
Katika somo hili utakwenda kujifunza jnsi ya kucheza na mafaili.hapa utajifunza kutengeneza mafaili kwenye server kwa kutumia php. Pia utajifunza kuyafuta na ku edit. Zaidi utajifunza kuhusu kuyalinda mafaili haya, na tutajifunza mengi zaidi. Somo hili kwakuwa nalo ni lefu nitaligawa kwenye vipengele:-
Kutengeneza folda kwenye server
Kutengeneza faili
Kupata orodha ya mafaili kwenye folda
Kufuta folda
Kufuta faili
Ku edit faili
Kusoma faili
Kutenfeneza folda:
Tunapozungumzia server sio kitu ambacho utaweza ku access kama ilivyo kompyuta yako. Hivyo tutahitajika tujuwe lugha ya kuzungumza na server ili iweze kufanya kile ambacho tunakitaka. Somo hili utaweza kuliona la kawaida ila lina umuhimu mkubwa sana kwa programa.
Ili kutengeneza folda tunatumia function inayoitwa mkdir(). Function hii itakuwa na parameta moja ambayo ni ya lazima ambayo ni jina la hilo folda. Kwa mfano unaweza kusema unataka kutengeneza folda linaloitwa bongoclass. Hivyo utaweka hivi mkdir(‘bongoclass’). Unaweza ku echo hiyo function ama kufanya uanavyotaka
echo mkdir('bongoclass');
?>
Pia unaweza kutumia if else ili uweze kupata majibu kama faili limetengenezwa ama laa. Kufanya hivi tutatumia alama ya ! kuamaanisha kama function imefeli iseme failed vinginevyo iseme created
if (!mkdir('mafunzo')){
echo "failed";
}else echo "created";
Kutengeneza sub folder
Ili uweze kutengeneza subfolder utatumia alama ya / mbele ya folda lako. Kwa mfanoi folda letu linaitwa ,afunzo na tunataka kutengeneza folda linaloitwa php ndani ya folda mafunzo. Hivyo tutaweka alama ya slash kisha jina la sub folda letu mfano mkdir(mafunzo/php)
if (!mkdir('mafunzo/php')){
echo "failed";
}else echo "created";
Hivyo hivyo unaweza kuongeza folda lingine ndani ya subfolda. Mfano
if (!mkdir('mafunzo/php/level-3/lesson-1')){
echo "failed";
}else echo "created";
Kutengeneza faili
Ili kutengeneza mafaili kwenye server tutatumia function ya php inayoitwa fopen() au kwa kutumia fwrite(). Mfano tunatka kutengeneza faili linaloitwa bongoclass.html, bongo.txt, bongoit.mp3. Hivyo tutatumia function hii kufanya hivyo.
Function hii ya kutengeneza mafaili ina para,meter mbili ambazo ni lazima. Moja ni jina la faili lenye extension yake, na la pili ni namna ambavyo hilo faili litatumika. Kwa mfano ukiweka W hiyo ni kwa ajili ya kuandika faili tu, nyingine ni kama:-
w. Kuandika faili tu, hutengeneza faili kama halipo
r . kusoma faili tu, husoma kuanzia mwanzo
Nyingine utazipata hapa
Kiutaratibu unatakiwa ufanye hivi, kwanza utatumia fopen() ili kufunguiwa faili kisha utatumia fwrite() ili kuandika taarifa kwenye faili, kisha utatumia fclose() ili kufunga hilo faili ulilolifunguwa. Kuwa makini sana ni jambo linalisisitizwa kufunga faili lolote baada ya kulitumia.
Pia kuna functio nyingine ya die() ni kama tulivyotumia function hii kwenye database. Hivyo hapa napo endapo code zitashindwa kufunguwa hilo file lamda pengine halipo basi itastop. Wacha tuine mifano hapo chini:-
Mfano 1:
echo fopen("upload/bongoclass.html", "w");
echo fopen("upload/bongo.txt", "w");
echo fopen("upload/bongoit.mp3", "w");
?>
Sasa utaona ukifunguwa hayo mafaili hayana data ndani yake. Hivyo sasa ni wakati wa kutumia fwrite() ili kuandika data kwenye hayo mafaili. Sasa tutakwenda lkutengeneza mafaili mengine matatu ambayo tutaandika data. Tutayapa jina web.html, somo.txt, funzo.doc.
Kwanza tutatengeneza variable za kuwakilisha function za kutemnheneza hayo mafaili kisha ndipo tutakwenda kuweka data kwenye mafaili hayo. Kwa kuwa mfaili hayo yapo kwenye format tofauti basi kila m moja hapo itabidi awe na variable yake na data zake.
Mfano 2:
$a = fopen("upload/bongoclass.html", "w");
$b = fopen("upload/bongo.txt", "w");
$c = fopen("upload/bongoit.doc", "w");
echo fwrite($a,"
haloo bongoclass
");
echo fwrite($b,"Habari ya muda huu Bongoclass");
echo fwrite($c,"Hili ni faili la PDF kutoka bongoclass");
fclose($a);
fclose($b);
fclose($c);
?>
Utaona hapo ukirun kuna namba zinatokea. Hiyo ni idadi ya character zilizopo kwenye hilo faoli. Kwa namna hiyo unaweza kutengeneza faiuli na kuweka data hata kutoka kwenye database. Unaweza pia kuweka hayo mafaili kwenye folda unalotaka. Hata kwenye subfolda.
Hatuwa inayofuata ni kuyasoma hayo mafaili. Sasa katika kusoma data kuna namna nyingi hapa nitakwenda kukutajia namna 4, ambazo ni kusoma lote kwa pamoja kwa kutumia fread() au kusoma msatri wa kwanza tu. hapa tutatumia fgets(), namna ya pili ni kusoma mstari wa mwisho hapa tutatumia feof(), na namna ya mwisho ni kusoma mistari yote mmoja baada ya mwingine. Hapa tutatumia !feof() hii ni sawa na hiyo ya ,mwanzo ila tofauti ni kjuwa hii tutaifanyia programming.
Sasa tutatumia faili moja katika mfano huu. Tutaongeza mstari wa data ili tuweze kupata mistari kadhaa. Sasa tutakachokifanya ni ku edit moja ya mafaili yetu. Ku edit maana yake data ambazo zipo hatuziondoi ila tunaongeza nyingine. Ili tuweze ku edit tutatakiwa tutumie read mode ya “a”. Katika mfano unaofuata pia tutatumia function ya die() ili ku stop kama kuna kitu hakipo sawa. Pia nitatumia alama ya ili kuruka mstari. Hii ni sawa na ,kutumia
kwenye html
Mfano 3:
$file = fopen("upload/bongo.txt", "a") or die("kuna tatizo");
$txt1 = "karibu bongoclass ";
fwrite($file, $txt1);
$txt2 = "upate elimu bure ";
fwrite($file, $txt2);
$txt3 = "website yetu ni www.bongoclass.com ";
fwrite($file, $txt3);
$txt4 = "wasiliana nasi muda wowote ";
fwrite($file, $txt4);
fclose($file);
?>
Sasa kwa kuwa tunalo faili letu ambalo lipo hapo lina mistari 6 na kila msatari tgu aona nini kimeandikwa. Sasa tunakwenda kusoma mistari hiyo kwa kutumia php. Utaweza kufanya hivi pia kwa mafaili mengine.
Kabla ya kusoma hayo mafaili kuna kitu nataka ukifahamu kwanza. Nacho ni kujuwa ukubwa wa faili. Tulisha jifunza kuhusu filesize kwenye POST sasa hapa tunakwenda kujuwa ukubw awa faili kw akutum ia filesize(). Hii itatupa ukubwa wa faili kwa byte. Hivyo kwanza nataka tujuwe hilo faili letu hapo juu lina ukubwa gani?
Mfano 4:
$file = fopen("upload/bongo.txt", "r") or die("Unable to open file!");
echo filesize("upload/bongo.txt");
fclose($file);
?>
Sasa tunakwenda kusoma faili letu kwa kiutu mia fread(). Function hii itabeba parameta 2 am bazo n i jina la faili ambalo limesha funguliwa hapa tutatumia fopen, na parameta ya pili ni filesize. Hivyo itakuwa hivi
Mfano 5:
$file = fopen("upload/bongo.txt", "r") or die("Unable to open file!");
echo fread($file,filesize("upload/bongo.txt"));
fclose($file);
?>
Sasa tunakwenda kusoma mstari wa kwanza tu. hapa tutatumia fgets(). Function hii nayo itabeba parameta moja ambayo ni jina la faili ambalo limesha finguliwa.
$file = fopen("upload/bongo.txt", "r") or die("Unable to open file!");
echo fgets($file);
fclose($file);
?>
Kuna changamoto utaipata kwenye fread() ni kuwa faili limefunguka lote. Na mistari imeungaa tofauti na tulipotengeneza tuliruka mstari kwa . Sasa kutatuwa cgangamoto hiyo tutatumia function hii feof() hii kazi yake ni kuangalia kama faili limefika mwsho. Hivyo basi tutasoma mstari baada ya mstari mpaka mwisho. Hivyo kila m stari utakaa mahala pake.
Tutahitajika hapa kutumia condition statement, ili tuweze kufanya looping kutolka mwanzo mpaka mwisho. Hapa tutatumia while loop. Ni matumaini yangu kuwa unafahamu kuhusu while loop. feof() hii huangalia je tumefika mwisho. Sasa nitafanya hivi !foef() hii ni negative yake, hivyo tutasema endapo hatujafika mwsho basi iendelee kusoma faili letu mstari baada ya mstari. Hivyo tutaitumia tena fgets().
Mfano 6:
$file = fopen("upload/bongo.txt", "r") or die("Unable to open file!");
while(!feof($file)) {
echo fgets($file) . "
";
}
fclose($file);
?>
Wacha nikuekekeze namna nyingiune ya kusoma faili, namna hii ni kusoma faili kwa character mojo moja, au herufi moja moja. Yaani inasoma character mpoja, kisha inayofuata. Na kila moja inakaa kwenye mstari wake kama uta break line. Functio itakayotumika hapa ni fgetc().
Mfano 7:
$file = fopen("upload/bongo.txt", "r") or die("Unable to open file!");
while(!feof($file)) {
echo fgetc($file) . "
";
}
fclose($file);
?>
Ila endapo utaondoa hiyo
faili litakuwa na muonekano ule ule tuliouzoea. Ila sentensi hazitajipanga kwe nye mistari ila zitakuwa kama ni mstari mmoja.
Sasa je kama ninataka kusoma baadhi tu ya mistari. Wa mfano faili letu hapo juu tunataka kusoma mistari mitatu ya kwanza. Hivyo basi kwanza itatakiwa kujuwa idadi ya mistari iliyopo kwenye hilo faili. Kufanya hivi tutatujmia coutn(file(()) function. Utaona hapo ni function ya count() ambao ndani yake kuna function ya file(). Sasa hiyo ya file() ndio ambayo inahesabiwa. Yenyewe ina irray kulingana na idadi ya mistari. Kwa mfano faili la mistari 6 itakuwa na array 5. Kumbuka array huhesabiwa kuanzia 1.Kisha baada ya hapo tutatumia condition ">...
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: PHP Main: Masomo File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 291
Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh
👉2 Kitabu cha Afya
👉3 kitabu cha Simulizi
👉4 Madrasa kiganjani
👉5 Simulizi za Hadithi Audio
👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
PHP somola 69: jinsi ya kutuma email kwa watu zaidi ya mmoja kwa kutumia PHPMailer
Katika somo il utajifunza kutuma email kwa watu wengi kwa kutumia PHPMailer. Pia utajifunza jinsi ya kuweka Carbon Copy na Blind Carbon Copy Soma Zaidi...
PHP somo la 57: class traits kwenye PHP
Katika somo hili utakwenda kujifunza concept ya traits kwenye OOP. hii itakusaidia ku solve baadhi ya changamoto zinazotokana na inheritance Soma Zaidi...
PHP somo la 89: Jinsi ya kutumia data za json kwenye program ya php na html
Katika somo hili utakwend akujifunza ni kwa namna gani utaweza kuzitumiadata za jsonkwenye program yako Soma Zaidi...
PHP somo la 58: static method kwenye PHP
Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu static method na inavtotumika kwenye OOP Soma Zaidi...
PHP somo la 79: Custom header
Katika somo hili utakwenda kuhifunza kuhusu Custom header na aina zake Soma Zaidi...
PHP somo la 52: Aina za access modifire na zinavyotofautiana.
Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu access modifier ili kuweza kuthibiti nama ya kuzitumia properties kwenye class. Soma Zaidi...
PHP somo la 77: aina za http redirect
Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu http redirect header Soma Zaidi...
PHP - somo la 35: Jinsi ya ku upload mafaili kwa kutumia PHP
Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya ku upload mafaili kwenye server kwa kutumia PHP Soma Zaidi...
PHP - somo la 27: aina za variable kwenye PHP
Katika somo hili utakwenda kujifunza aina kuu 3 za variable katika PHP mabzo ni local variable, global variable na static variable. Soma Zaidi...
PHP - somo la 21: Jinsi ya kutafuta kitu kwenye database kwa mutumia PHP
Katika somo hili utakwenda kujifundisha jinsi ya kutafuta taarifa maalumu kwenye database kwa kutumia PHP Soma Zaidi...
PHP somo la 68: Jinsi ya kutuma email kwa kutumia PHPMailer
Katika somo hili utakwenda kujifunza jisniya kutuma email kwa kutumia PHPMailer kwenye project ya PHP. Katika somo hili tutakwend akutuma email kwa kutumia localhost. Soma Zaidi...
Jinsi ya kutuma Email kwa kutumia PHP
Katika post hii utakwenda kujifunza jinsi ya kutuma email kwa kutumia php function ya email() Soma Zaidi...