Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu http header, maana yake na jinsi ya kusoma taarifa zilizopo kwenye http header.
Karibu kwenye course mpya ya PHP mabayo itakwenda kuzungumzia kuhusu HTTP header na jinsiambavyo inavyofanya kazi. Course hii ni moja ya misingi ya course zinazofuata.
Nini utakwenda kujifunza?
Maana ya http header
Jinsi ya kupata header information
Jinsi ya kuweka header information Yako mwenyewe.
Jinsi ya kulinda usalama wa header information
Matumizi ya header information
Http header ni Nini?
Haoa tunazungumzia zile taarifa ambazo zinahusu request inayotokea kwneye server na inayoingia.
Request ni like ombi linalofanywa browser ya mtumiaji hii tunaita client request. Mfano wewe umeandika link https://bongoclass.com. Sasa browser Yako itaomba server ambayo inamaudhui yaink husika kuletabmaudhui hayo. Kisha server itajibu kwa kukupa maudhui hayo kama ni habari, hadithi, audio n k. Haya majibu ambayo server inatia yanaitwa server response.
Sasa wakati wewe unatumia client request kwa kuandika hiyo link Yako, hiyo link inapokwenda kuomba maudhui kwenye server husika, inakwenda na baadhi ya taarifa maalumu zinazohusu hiyo link.
Mfano link hiyo itabeba taarifa inayoonyesha kabla ya kubofya link hiyo unetojea kwenye link Gani, pia taarifa nyingine kama IP address, jina la domain, n k
Taarifa hizi huwezi kuziona kwenye link yenyewe mpaka uziombe kwenye server. Sasa njia ambazo taarifa hizi hulitishwa ni kwa kupitia http header.
Http header ni sehemu muhimu ya data ambayo inatumiwa katika mawasiliano ya mtandao kati ya mtandao wa mteja na mtandao wa seva. Ina maelezo yanayoelezea ombi la HTTP au jibu, kama vile aina ya data inayotumwa au kupokelewa, lugha inayotumiwa, kuki za mtumiaji, na maelezo mengineyo muhimu.
Baadhi ya yaarifa kwenye httpheader::
Hapa nakuletea tu orodha ya taarifa zinazoweza kupatikana kwenye http header. Katika somo linalofuata tutakwenda kuziangalia taarifa hizi kwa undani zaidi.:-
1.Host: Jina la seva inayotakiwa kushughulikia ombi.
2.User-Agent: Maelezo kuhusu programu ya mteja inayofanya ombi.
3.Accept: Aina za media zinazotakiwa kukubaliwa na mteja.
4.Content-Type: Aina ya data inayotumwa kwa seva au inayopokelewa kutoka kwa seva.
5.Content-Length: Urefu wa data inayotumwa kwa seva au inayopokelewa kutoka kwa seva.
6.Authorization: Msimbo wa uthibitishaji wa mteja.
7.Cookie: Habari za kuki za mtumiaji zinazotumwa kwenye seva.
8.Location: Anwani ya URL ya kuelekeza kwa mteja (hasa katika majibu ya kuelekeza).
9.Cache-Control: Maelezo kuhusu jinsi ya kushughulikia caching ya data.
10.Server: Maelezo kuhusu seva inayojibu ombi.
11.Date: Tarehe na saa ambayo ombi au jibu lilifanyika.Connection: Hali ya uhusiano wa mtandao, kama vile "close" au "keep-alive".
12.Content-Encoding: Aina ya kubadilisha iliyoitumika kwa data iliyotumwa au kupokelewa.
13.Referer: URL ya rasilimali iliyosababisha ombi la sasa.
14.Accept-Language: Lugha za makala zinazopendelewa na mteja.
14.ETag: Alama ya utambulisho wa kipekee kwa rasilimali, kutumika kwa udhibiti wa caching.
15.If-Modified-Since: Tarehe ya mwisho ya mabadiliko ya rasilimali, kutumiwa katika udhibiti wa caching.
Zipo tarifa nyinginezo ambazo tutaziona huko mbeleni kadiri somo linavyoendelea. Kwa sasa unachotakiw akujuwa ni kuwa ndani ya http header kuna taarifa nyingi sana.
Jinsi ya kusoma taarifa za http header:
Kuna njia kadhaa ambazo tutakwenda kuzitumia ili kusoma data kwenye http header. Njia hizo ni kama:-
Kwa kutumia global variable $_SERVER
<?php
echo $_SERVER['REQUEST_METHOD']; // Outputs the request method (GET, POST, etc.)
echo "<br>";
echo $_SERVER['REMOTE_ADDR']; // Outputs the IP address of the client
echo "<br>";
echo $_SERVER['HTTP_USER_AGENT']; // Outputs the user agent string of the client's browser
echo "<br>";
echo $_SERVER['SCRIPT_FILENAME']; // Outputs the absolute pathname of the currently executing script
echo "<br>";
echo $_SERVER['SERVER_ADDR']; // Outputs the IP address of the server
echo "<br>";
echo $_SERVER['SERVER_PORT']; // Outputs the port number to which the request was sent
echo "<br>";
echo $_SERVER['DOCUMENT_ROOT']; // Outputs the document root directory under which the current script is executing
echo "<br>";
echo $_SERVER['HTTP_ACCEPT_LANGUAGE']; // Outputs the languages the client can accept, based on the Accept-Language HTTP header
echo "<br>";
echo $_SERVER['PHP_SELF'];
echo "<br>";
echo $_SERVER['SERVER_NAME'];
echo "<br>";
echo $_SERVER['HTTP_HOST'];
echo "<br>";
echo $_SERVER['HTTP_REFERER'];
...
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Katika somo hili utakwenda kujifunza Jinsi ya kutumia ORM kwa kutumia library ya RedBeanPHP
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu access modifier ili kuweza kuthibiti nama ya kuzitumia properties kwenye class.
Soma Zaidi...Katika somo hilibutajifunza maana ya cURL pamoja na matumini yake
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu Cookie Headers
Soma Zaidi...Katika somo hili utajwenda kujifunza jinsi ya kuzuia hacking kwenye website yako
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya ku update na kufuta data kwenye database kwa kutumia PHP
Soma Zaidi...atika somo hli tutakwenda kujifunza kuhusu kitu kinachitwa cron job. ni moja ya teknolojia zinazotumika kufanya kazi zinazofanyika automatic
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifundisha jinsi ya kutafuta taarifa maalumu kwenye database kwa kutumia PHP
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kutuma email ambayo ina HTML, pia utajifunza kutuma email yenye picha na attachment nyinginezo kama pdf
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kuandika constant kwenye PHP. Pia utajifunza utofauti wake na variable
Soma Zaidi...