PHP - somo la 12: Jinsi ya kufanyia kazi taarifa zilizokusanywa kutoka kwa mtumiaji
Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kutumia taarifa ambazo zimekusanywa kutoka kwa mtumiaji ili kuweka kutatuwa hoja mbalimbali
PROJECT KULINGANA NA COURSE HII.
Kama ulivyokwiisha kutambuwa kuwa katika kila baada ya kumaliza course tunaleta poject. Project hizi zitakusaidia mshiriki wa mafunzo haya kuweza kuelewa zaidi na kufanyia kazi kile ambacho kime fundhishwa. Hapa nitakuletea project tano ambazo ni:-
1.Kikokotoo cha hesabu (Simple calculator with php and html)
2.Kikokotoo cha umri (age calculator with php)
3.Code playground (HTML, CSS and JAVASCRIPT code playground with php)
4.Dodoso la usajili (databaseless registration form).
5.Kuhesabu idadi ya maneno kwenye sentensi ama paragraph
Project hizi ni program fupifupi ambazo zina msingi mzuri kwa mwenye kuanza. Uzuri wa project hizi zote ni za level ya chini ssana kiasi kwamba kama ulishiriki kwenye mafunzo yetu hazitakushinda. Kama ukipata ugumu tafadhali rudia somo lililotangulia la 11 katika mafunzo haya.
1.KIKOKOTOO CHA HESABU
Program hii itakuwa inafanya kaz ka ma kikokotozi yaani calculator. Yenyewe itahusika na matendo manne ya hesabu yaani kujumlisha, kuzidisha na kugawanya. Mtumiaji atahitajika kuingiza namba, tendo (+, *, - au /) kisha ataingiza namba nyingine, atabofya submit kisha atapata majibu.
Program itakusanya data zake kwa kutumia HTML form kisha itatuma namba atakazoingiza mtu kwenye variable za php. Kwa kutumia switch case utaweza kuchaguw tendo. Tafadhali pitia somo la 10 kwenye mafunzo haya upate kujifunza zaidi kama hujaelewa kuhusu switch case.
CODE ZA PROGRAM NI HIZI:-
<html>
<form method="post" action="">
<label>KIKOKOTOZI:</label><br>
<input type="number" name="a" placeholder="0"><br>
<input type="text" name="b" placeholder=""><br>
<input type="number" name="c" placeholder="0"><br>
<br><br><input type="submit">
</form></html>
<?php
$a=$_POST['a'];
$b=$_POST['b'];
$c=$_POST['c'];
$result = "";
switch ($b) {
case "+":
$result = $a + $c;
break;
case "-":
$result = $a - $c;
break;
case "*":
$result = $a * $c;
break;
case "/":
$result = $a / $c;
}
?>
<p>
<input readonly="readonly" name="result" value="<?php echo $result; ?>">
</p>
2.DODOSO LA USAJILI
Katika program hii mtumiaji ataweza taarifa zake kisha zitakuja kama alivyoziweka. Program hii itakusaidia utakapokuja kujifunza namna ya kudisplay taarifa kutoka kwenye database. Kwa sasa hatutatumia database ila somo litakalofata taarifa hizi moja kwa moja zitatola kwenye database baada ya mtu kujiajili.
Program hii itatumia mafaili mawili. Moja ni la HTML kwa ajili ya kukusanya madodoso. Kisha faili lingine litakuwa ni kwa ajili ya kudisplay taarifa zilizojazwa. Katika faili la HTML kwenye action utakuta kuna link ya faili linalofata ambalo ndilo litakalopelekewa taarifa zilizojazwa kwa ajili ya kuchakatwa.
Ijapokuwa unaweza kuchanganya mafaili haya sehemu moja ;akini nimependelea kuyatengenisha kwa ajili ya kujifunza zaidi. Hivyo kama ndio na wewe unaanza weka mafaili mawili. Kisha faili m,oja ni la htm;l code na la pili ni kwa ajili ya php code.
Katika program hii faili la kwanza nimeliita p2.php ambalo litabeba php code na la pili p.php ambalo litabeba hyml code
P.pph
<html>
<form method="post" action="p2.php">
<label>Sensa ya watu na makazi</label><br>
<input type="text" name="a" placeholder="Weka jina lako hapa"><br>
<input type="text" name="b" placeholder="Umri"><br>
<input type="text" name="c" placeholder="Jinsia"><br>
<input type="text" name="d" placeholder="Unapoishi"><br>
<input type="text" name="e" placeholder="Hali ya ndoa"><br>
<input type="text" name="f" placeholder="Elimu"><br>
<br><br><input type="submit"...
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 web hosting 👉2 Simulizi za Hadithi Audio 👉3 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉4 Madrasa kiganjani 👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉6 Bongolite - Game zone - Play free game
Post zinazofanana:
PHP - somo la 23: Jinsi ya kutumia condition statement kwenye database kwa kutumia PHP
Katika somo hili utakwenda kuona namna ya kutuia if else kwenye data zilizopo kwenye database kwa kutumia PHP
Soma Zaidi...PHP somo la 81: Cross - Orgn Resource Sharing - CORSE header
Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu Cross - Orgn Resource Sharing ama inafupishwa kama CORSE header
Soma Zaidi...PHP - somo la 8: jinsi ya kuandika constant kwenye PHP
Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kuandika constant kwenye PHP. Pia utajifunza utofauti wake na variable
Soma Zaidi...PHP - somo la 7: Jinsi ya kaundika function yakwako
Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kuandika function yako mwenyewe yaani user defined function
Soma Zaidi...PHP - 9: Jinsi ya kuandika array kwenye PHP na kuzifanyia kazi
Katika somo hili tutakwenda kujifunza kuhusu array kwenye php, na jinsi zinavyoweza kufanya kazi
Soma Zaidi...PHP somo la 53: class inheritance kwenye PHP Object Oriented Programming
Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu class inheritance kwenye object oriented programming.
Soma Zaidi...