Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kukusanya taarifa za watumiaji kwa kutumia html form.
HTML FORM
Ili uweze kujaza madodoso kwa kutumia fomu ya HTML utahitaji sehemu ya kwenda hayo madodoso baada ya kujazwa. Kwa kutumia HTML utaweza kutuma na kupokea taarifa zilizokazwa kutoka katika fomu ya html.
Angalia fomu hiyo hapo chini.
<html>
<form method="post" action="">
<label>first name</label>:<br>
<input type="text" name="firstname">
<br>
<label>last name</label><br>
<input type="text" name="lastname">
<input type="submit" name="">
</form>
</html>
Ukiingalia vyema fomu hii utagunduwa ipo katika namna hii:-
1.Kuna tag ya fomu <form kuonyesha kuwa hapa ndipo fomu inaanzia.
2.Katika tag ya form kuna attribute ambayo ni method <form method attribute hii kazi yake ni kueleza kuwa hizi taarifa za humu kwenye hii fomu baada ya kujazwa zitatumwa kwa njia ipi.
3.Katika attribute method value yake ni post. Hii ina maana njia itakayotumika kutuma taarifa hizi ni njia ya post.
4.Kisha kuna attribute nyingine ndani ta tag ya <form ambayo ni action, hii kazi yake ni kueleza je action zote katika fomu hii zitachakatwa katika faili lipi. Mfano kama utahitaji michakato ifanyikie kwingine kwa sababu za kiulinzi basi utaweka faili unalotaka kwenye value ya attribute action. Katika mfano wetu hapo juu ipengele hili kimeachwa wazi.inamaana action zote zitafanyika hapahapa.
5.Kuna lebo ya firstname na ya last name
6.Kisha kuna input type. Input type hapa ni taarifa ambazo unahitaji huyo mjazaji wa dodoso aweke. Kama unataka aweke email, hpo utaweka email. Katika mfano wetu huu input type ni text, yaani anachotakiwa ajaze mtu ni text ambazo ni herufi, namba na symbils.
7.Mwisho kuna batani ya kusabmit. Hii ndio batani ya kutumia dodoso. Yaani ukiibofya batani hii dodoso litakuwa limetumwa.batani hii yenyewe input type yake ni submit.
FORM METHODS
Kama nilivyogusia hapo juu ni kuwa method zipo mbili katika kutuma na kupokea madodoso kutoka kwenye html form moja ni POST na nyingine ni GET. Tunatumia post tunapotuma taarifa za siri, na tunatumia GET tunapotuma ama kupokea taarifa zisizo za usiri. Tutajifunza mengi zaidi kwenye mafunzo ya mbele">...
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Katika course hii utakwenda kujifundisha jinsi ya lutengeneza blog kutoka mwanzo hadi mwisho.
Soma Zaidi...Faili la env ni moja kati ya mafaili ambayo ni muhimu kwa usalama wa project. Fili hili hutumika kuhifadhi data za siri
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza concept ya iteration kwenye PHP OOP hapa tutakwenda kuiona jinsi inavyofanya kazi pamoja na foreach loop
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu Cookie Headers
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kutumia taarifa ambazo zimekusanywa kutoka kwa mtumiaji ili kuweka kutatuwa hoja mbalimbali
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu static method na inavtotumika kwenye OOP
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu access modifier ili kuweza kuthibiti nama ya kuzitumia properties kwenye class.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu http redirect header
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwend akujifunza jinsi ya kubadili json data na kuwaphp array ama php object. Kwa ufupi tunakwend aku decode json data kuwa phparray amaobject
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu Aina za cache header
Soma Zaidi...