Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za parachichi
Palachichi (avocado)
Hili ni katika matunda yenye fat (mafuta). Itambulike kuwa si kila mafuta ni hatari ndani ya miili yetu. Tunahitaji vyakula vya fat yaani mafuta kwa ajili ya kutupatia joto kwenye miili yetu. Pia fati husaidia kuipa miili yetu nguvu. Katika tunda hili palachichi mafuta yake ni aina ya oleic acid yaani yapo katika aina flani ya asidi ambayo husaidia katika kupunguza uvimbe mwilini na kusaidia kuboresha afya ya moyo.
Palachici pia hutambulika kitaalamu kuwa lina lina madini ya potassium na magnesium kwa wingi sana. Pia ni katika vyakula vyenye kambakamba yaani fiber. Vyakula hivi vyenye fiber husaidia katika kuweka usalama wa tumbo yaani kuhakikisha chakula kinatembea ipasavyo ndani ya tumbo kutoka sehemu moja mpaka sehemu nyingine mpaka kufika kwenye njia ya haja kubwa.
Pia tunda hili husaidia kupungusa hatari za kupata maradhi ya stroke yaani kupalalaizi kutokana na kiwango kikubwa cha madini ya magnessium ambayo husaidia katika kupunguza shinikizo kubwa la damu. Hivyo palachichi husaidia katika kudhibiti afya ya moyo. Palachichi moja linaweza kutoa 28% ya mahitaji ya mwili ya madini haya.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
kuhusu vitamini C, kuanzia chanzo chake, maana yake, upungufu wake na kazi zake kwenye miili yetu.
Soma Zaidi...Post hii itakufundisha aina za vyakula ambavyo vinaweza kuongeza damu kwa haraka.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula biringanya eggplant)
Soma Zaidi...Zijuwe sababu kuu za kuwepo kwa maumivu ya tumbo baada ya kula chakula
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi faida za majani ya mstafeli,ni majani ambayo utibu magonjwa mbalimbali hasa saratani, kwa hiyo tunapaswa kuyatumia ili tuweze kupata matibabu ya kansa mbalimbali.
Soma Zaidi...Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu vyakula vya kuoambana na mafua
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi kazi za tunda la mpapai katika kurekebisha homoni.ni tunda ambalo ufanya kazi yake kwa sababu ya kuwepo kwa virutubisho muhimu ndani ya tunda hili.
Soma Zaidi...Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote
Soma Zaidi...