Fahamu vitamini A na kazi zake, vyakula vya vitamini A na athari za upungufu wake

Vitamini A ni katika vitamini fat soluble vitamin akama vile retinol, retinal, retinoic acid na beta-carotene.

Fahamu vitamini A na kazi zake, vyakula vya vitamini A na athari za upungufu wake

VITAMINI A

Vitamini A ni katika vitamini fat soluble vitamin akama vile retinol, retinal, retinoic acid na beta-carotene. Vitamini A ni moja kati ya vitamini vingi. Vitamini vingine ni viamini b, C, D, E, K. unaweza kupata vitamini A sana kwenye mboga za majani za kijani, maini, mayai, maziwa, karoti na spinach. Katika makala hii tutakwenda kuona mengi kuhusu vitamini A, kazi zake, vyakula vya vitamini A pamoja na athari za upungufu wake mwilini:



Yaliyomo:
1.Maana ya vitamini A
2.Kazi za vitamini A
3.Vyakula vya vitamini A
4.Upungufu wa vitamini A
5.Athari za kuzidi kwa vitamini A



Maana ya vitamini A


Vitamini ni aina ya fat soluble vitamini ambayo ni kampaind ogania (organic compound) inayopatikana katika makundi kama retinol, retinal, retinoic acid na provitamin ambazo ni beta-carotene. Vitamini A ni muhimu katika ukuaji, uboreshwaji wa mfumo wa kinga na kuboresha afya ya macho.



Ugunduzi wa vitamini A umeanza toka miaya ya 1816 na Mwanasayansi aliyejulikana kwa jina la Francois Magendie alipokuwa akimfanyia uchunguzi mbwa mgonjwa. Baada ya hapo tafiti mbalimbali zikafata mwaka 1912, 1913, 1918, 1920 na 1939 na 1947. vitamini A vimepewa jina hili katika tafiti za mwaka 1920.



Kazi za vitamini A


1.Husaidia katika afya ya macho yaani kuona
2.Husaidia katika ukuaji
3.Husaidia katika kuboresha mfumo wa kinga mwilini
4.Husaiia katika ukuaji wa mimba na mtoto aliye tumboni
5.Husaidia katika afya ya mifupa
6.Husaidia katika afya ya ngozi
7.Husaidia katika afya ya meno
8.Husaidia katika utengenezwaji wa uteute mwilini.



Vyakula vya vitamini A


1.Maini
2.Karoti
3.Viazi vitamu
4.Spinachi
5.Maboga
6.Pilipili
7.Maembe
8.Njegere
9.Maziwa
10.Mayai
11.Mboga za majani za rangi ya kijani


Upungufu wa vitamini A


Tafiti zinaonyesha kuwa upungufu wa vitamini A huathiri watoto wanaokadiriwa kufikia 670,000 waliochini ya umri wa miaka mitano kila mwaka. Pia inakadiriwa kuwa watoto katika ya 250,000 na 500,000 wanakuwa vipofu katika nchi zinazoendelea kila mwaka. Tafiti zinathibitisha kuwa chanzo kikuu cha upofu kwa watoto ni upungufu wa vitamini A.



Athari za vitamini A kupitiliza


Endapo mtu atakuwa na vitamini A vingi ndani ya mwili hata vikapitiliza kiwango ambacho mwili unaweza kudhibiti, athari zifuatazo zinaweza kutokea:-
1.Mkusanyiko wa sumu mwilini
2.Kichefuchefu
3.Kuwshwa
4.Kukosa hamu ya kula
5.Kutapika
6.Kuona maluelue
7.Maumivu ya kichwa
8.Kupotea kwa nywele na misuli
9.Maumivu ya tumbo na uchovu



                   

Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Vyakula Main: Afya File: Download PDF Views 3011

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya    👉2 Bongolite - Game zone - Play free game    👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉4 Madrasa kiganjani    👉5 Kitau cha Fiqh    👉6 Simulizi za Hadithi Audio   

Post zinazofanana:

Faida kula fenesi

Somo hili linakwenda kukuletea faida za kiafya za kula fenesi

Soma Zaidi...
Faida za kula kachumbari

Posti hii inahusu zaidi faida mbalimbali ambazo anaweza kuzipata mtu anayetumia kachumbari, tunajua wazi kwamba kachumbari ni mchanganyiko wa nyanya, vitunguu maji,kabichi,na pilipili kidogo.

Soma Zaidi...
Vyakula vya kuongeza nguvu za kiume

Vijuwe vyakula vya kyongeza nguvu za kiume na mambo yanayopunguza nguvu za kiume

Soma Zaidi...
Fahamu Vitamini E na nz kazi zake, vyakula vya vitamini E na athari za upungufu wake

Katika makala hii nitakwenda kukupa somo linalohusu vitamini E, kazi zake, chanzo chake na madhara ya upungufu wake

Soma Zaidi...
Majani ya mstafeli dhidi ya bakteria na fangasi

Posti hii inahusu zaidi kazi ya majani ya mstafeli dhidi ya bakteria na fangasi, pamoja na kutibu saratani mbalimbali na upambana na fangasi na bakteria kama tutakavyoona.

Soma Zaidi...
VYAKULA VYA MADINI

Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote

Soma Zaidi...