Posti hii inahusu zaidi dalili za ugonjwa wa Bawasili, ni Dalili ambazo ujitokeza kwa mgonjwa ambaye ana ugonjwa wa Bawasili.
1. Dalili ya kwanza ni maumivu wakati wa kujisaidia.
Kwa sababu ya kuwepo kwa Maambukizi kwenye sehemu ya haja kubwa au tayari mishipa midogo kwenye haja kubwa ishapasuka Mgonjwa uhisi maumivu makali wakati wa kujisaidia haja kubwa.
2. Kutokwa na damu wakati wa kujisaidia.
Kwa sababu mishipa ya sehemu ya haja kubwa ishapasuka kwa hiyo Mgonjwa anapojisaidia damu utoka wakati wa kujisaidia.
3. Kuwepo kwa miwasho kwenye sehemu ya haja kubwa.
Kwa sababu ya kuwepo kwa Maambukizi kwenye sehemu ya haja kubwa miwasho inakuwepo mingi na kunakuwepo na kishawishi cha kujikuna mara kwa mara hali inayosababisha kuenea kwa magonjwa mengine kama vile minyoo na Typhoid.
4. Kuwepo na uvimbe na kinyama kwenye sehemu za siri,
Hali hiyo Usababishwa na kupasuka kwa mishipa midogo sehemu ya haja kubwa hali inayopelekea kuota vinyama au uvimbe kwenye sehemu mbalimbali za haja kubwa.
5. Haja kubwa kujitokeza kwa mda wowote.
Kuna wakati mwingine haja kubwa uja mara kwa mara kwa sababu ya kuwepo nafasi ndogo sehemu ya kuhifadhiwa haja kubwa kwa sababu ya kuota kwa vinyama au uvimbe sehemu hizo.
6. Choo juwa kigumu au mara nyingine kukosa kabisa kwa siku tatu na pia uambatana na Maumivu makali ya kiuno na mgongo.
7. Tumbo kujaa gesi mara kwa mara kwa sababu ya kuwepo kwa Maambukizi.
8. Kuhisi njaa mara kwa mara, hali hii utokea kwa sababu ya kutoa haja kubwa mara kwa mara au wakati mwingine kwa sababu ya kuwepo kwa Maambukizi.
9. Baada ya kuona dalili kama hizi ni vizuri kabisa kuhakikisha kuwa matibabu ya mapema ni lazima ili kuepuka madhara makubwa zaidi.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Post yetu Leo inaenda kuzungumzia Maumivu ya nyuma ni malalamiko ya kawaida. Kwa upande mkali, unaweza kuchukua hatua za kuzuia au kupunguza matukio mengi ya maumivu ya mgongo. Ikiwa kinga itashindikana, matibabu rahisi ya nyumbani na mbinu sahihi za m
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi madhara ya ugonjwa wa madonda ya koo usipotibiwa, ugonjwa huu usipotibiwa unaweza sababisha madhara mbalimbali kama ifuayavyo.
Soma Zaidi...Malaria husababishwa na vimelea (parasite) ambavyo husambazwa ama kubebwa na mbu aina ya anopheles.
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia kuhusiana na maumivu ya shingo na ndani yake kunasababu zinazopelekea shingo kupata maumivu.
Soma Zaidi...Swali hili limeulizwa na mdau mmoja. Kuwa endapo mtu atafanya ngono zembe na akapata virusi je ataweza kuambukiza.
Soma Zaidi...Ugonjwa wa pumu ni moja katika magonjwa hatari yanayoweza kutokea kwa ghafla, na endapo itacheleweshwa kudhibitiwa inaweza sababisha athari mbaya zaidi
Soma Zaidi...Katika post hii utakwend akujifunza kuhusu tatizo la kuwa na vijiwe kwenye ini vijiwe hivi hufahamika kama intrahepatic stones.
Soma Zaidi...Saratani ya uke ni Saratani adimu inayotokea kwenye uke wako mrija wa misuli unaounganisha uterasi na sehemu zako za siri. Saratani ya uke mara nyingi hutokea katika seli zilizo kwenye uso wa uke wako, ambao wakati mwingine huitwa njia ya uzazi. Wan
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi adhari za ugonjwa wa Homa ya inni, hizi ni athari ambazo zinaweza kutokea ikiwa ugonjwa huu wa inni haujatibiwa, zifuatazo ni athari za ugonjwa wa inni
Soma Zaidi...