Posti hii inahusu zaidi huduma anayopaswa kupata mgonjwa wa ndengue, kwa sababu tunafahamu wazi Ugonjwa huu hauna dawa ila kuna huduma muhimu ambayo anaweza kupata na akaendelea vizuri.
1.Kwa hali ya kawaida Ugonjwa ambao unasababishwa na virusi huwa hauna dawa lakini kuna huduma mbalimbali ambazo utolewa na mgonjwa anaweza kupona na kuendelea na hali yake ya kawaida na pengine huwa tiba inayotolewa kuendana na dalili iliyopo kama Mgonjwa anaumwa kichwa dawa ya maumivu utolewa au kama anaharisha dawa ya kuzuia kuharisha utolewa na mambo kama hayo hatimaye Mgonjwa anapata nafuu na kuendelea na shughuli zake kama kawaida.
2. Kwa sababu mgonjwa wa Dengue anakuwa na maumivu makali ya kichwa kwa kawaida anapewa dawa ya maumivu na kwa wakati mwingine anapewa maji ambayo yamependekezwa na wizara ya afya ni lingers na pengine Mgonjwa kama ana uwezo wa kunywa maji ya kawaida anaweza kunywa na pia kuna wakati mwingine hali ikiwa imefikia pabaya mgonjwa huwa anatoa damu kwa hiyo kuna hatari ya kupungukiwa damu kwa hiyo anaongezea damu na anapewa dawa ya kusaidia damu iache kutoka mara kwa mara.
3. Vile vile Tunapaswa kuzuia Ugonjwa huu kwa kwa kuwapatia watu elimu kuhusu kuwepo kwa ugonjwa huu na kuwapatia mbinu za kujikinga na ugonjwa huu kwa kutumia neti wakati wa usiku kukata vichaka na mazalia ya mbu na kwa wakati mwingine kutumia dawa za kujipaka ili kuweza kupunguza kiwango cha kuenea kwa mbu.
4. Kwa hiyo baada ya kujua Ugonjwa huu jamii pia inapaswa ielezwe wazi pale Ugonjwa huu unapotokea ili kuweza kuwafahamisha watu wajue namna ya kujikinga na hasa kuwakinga watoto wadogo na wazee ambao wapo kwenye hatari kubwa ya kupata matatizo zaidi, kwa hiyo na mila na desturi potovu zinapaswa kuepukwa wakati wa kipindi hiki cha Ugonjwa huu ili kuepuka madhara na matatizo yatokanayo na Ugonjwa ambao hauna dawa
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowSomo hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za vidonda vya tumbo
Soma Zaidi...Posti hii inaelezea kuhusiana na kujikinga au kuzuia virusi vya ukimwi.
Soma Zaidi...Post hii itakwenda kuangalia mlo sahihi wa mwenye vidonda vya tumbo. Hata utajifunza ni vyakula vipi hapaswi kula na vipi ana paswa kula.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi madhara ambayo yanaweza kutokea ikiwa Ugonjwa huu wa ukimwi ukishasmbaa kutoka sehemu moja kwenda nyingine na kuleta madhara makubwa kama ifuatavyo.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi maambukizi kwenye uume, maambukizi hata utokea kwenye kichwa Cha uume kwa kitaalamu huitwa Balanitis, zifuatazo ni sababu za kuwepo kwa ugonjwa huu.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi dalili za ugonjwa wa Bawasili, ni Dalili ambazo ujitokeza kwa mgonjwa ambaye ana ugonjwa wa Bawasili.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi sababu za maambukizi kwenye nephroni, ni vitu vinavyosababisha mabukizi kwenye nephroni.
Soma Zaidi...Posti hii inaonyesha mambo mbalimbali yanayoweza kusababisha Ugonjwa wa kifua kikuu kwa watoto chini ya miaka mitano.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi njia za kutambua Dalili za macho makavu, kama tulivyotangulia kuona kubwa macho kuwa makavu Usababishwa na sehemu ya kuzalisha maji kwenye jicho kushindwa kufanya kazi na jicho hilo huwa kavu na Dalili zake ni kama ifuatavyo.
Soma Zaidi...Mbu ni katika wadudu wanaopatikana maeneo yenye joto hususan maeneo ynye hali ya hewa ya kitropik.
Soma Zaidi...