Elimu yenye Manufaa
Elimu yenye manufaa ni ile ambayo: Kwanza, humuwezesha mja kufikia lengo la kuumbwa kwake. Tumeona kuwa elimu imekuwa faradhi ya kwanza kwa waumini kwa kuwa elimu ndio nyenzo kuu ya kuwawezesha binaadamu kufikia lengo la kuumbwa kwao ambalo ni kumuabudu Allah (s.w), ipasavyo
katika kila kipengele cha maisha yao. (Qur-an 51:56). Pia elimu ndio nyenzo kuu ya kuwawezesha waumini kuwa viongozi wa jamii (makhalifa wa Allah) katika ardhi. (Qur-an 2:30 - 31).
Elimu itakayotafutwa kinyume na kumuwezesha mtu kumuabudu Mola wake ipasavyo na kusimamisha ukhalifa wa Allah (s.w) katika ardhi itakuwa si elimu yenye manufaa bali elimu yenye kuhasirisha kama tunavyojifunza katika hadithi zifuatazo:
Abu Hurairah (r.a) amesimulia kuwa Mtume (s.a.w)
amesema: โAnayetafuta elimu isiyokuwa kwa ajili ya
kutafuta radhi za Allah (s.w), hasomi kwa lengo lolote
lile ila la kupata maslahi ya hapa duniani tu. Huyo
siku ya kiyama hatapata hata harufu ya Pepo.โ
(Ahmad, Abu Daud, Ibn Majah).
Pia Mtume (s.a.w) ametuasa kuwa mwenye kutafuta elimu ili awazidi wasomi wengine au ili kuitumia katika biashara za kijahili au ili kujionesha kwa watu kuwa naye ni msomi, Mwenyezi Mungu atamuingiza motoni. (Tirmidh).
Pili, elimu yenye manufaa kwa binaadamu hapa ulimwenguni na huko akhera ni ile ambayo pamoja na mtu binafsi kuitumia katika kumuabudu Allah (s.w) ipasavyo katika maisha yake ya kila siku, huifundisha au huifikisha kwa wengine pia kwa ajili ya kutafuta radhi za Allah (s.w).
Ni vibaya mno mbele ya Allah (s.w) mtu kukataa au kuacha kufikisha kwa wengine kila anachokijua kama tunavyojifunza katika hadithi ifu atayo:
โAbu Hurairah (r.a) amesimulia kuwa Mtume (s.a.w) amesema: โAtakayeulizwa juu ya jambo alilojifunza kisha akaficha (akakataa kutoa elimu ile) atavalishwa mshipi wa moto katika siku ya Kiyamaโ. (Ahmad, Ibn Majah, Tirmidh na Abu Daud).
Katika hadith nyingine iliyosimuliwa na Abu Hurairah Mtume (s.a.w) amesema:
โMfano wa elimu isiyonufaisha ni sawa na mfano wa mali iliyokusanywa bila ya kutumiwa katika njia ya Allah โ. (Ahmad, Darini).
Kutokana na hadith hizi tunajifunza kuwa elimu yenye kunufaisha ni ile iliyofundishwa kwa wengine kinadharia na kiutendaji. Kwa kufundisha watu unachokijua bila ya wewe mwenyewe kutenda ni mfano mbaya mno kwa wale wanaofundisha na chukizo kubwa mno mbele ya Allah (s.a.w):
โEnyi mlioamini mbona mnasema msiyoyatenda?) Ni chukizo kubwa mbele ya Allah (s.w) kusema msiyoyatenda.โ (61:2-3)
******************************
Umeionaje Makala hii.. ?
Kwa hakika binaadamu ameumbwa, hali ya kuwa mwenye pap atiko.
Soma Zaidi...Allah hutumia maandishi kuwafundisha wanadamu. Mfano mzuri ni nabii Musa ambaye alipewa vibao vya maandishi.
Soma Zaidi...ุนููู ุฃูุจูู ุฐูุฑูู ุฌูููุฏูุจู ุจููู ุฌูููุงุฏูุฉูุ ููุฃูุจูู ุนูุจูุฏู ุงูุฑููุญูู ููู ู ูุนูุงุฐู ุจููู ุฌูุจููู ุฑูุถููู ุงูููููู ุนูููููู ูุงุ ุนููู ุฑูุณูููู ุงููู...
Soma Zaidi...Mtazamo wa uislamu juu ya ibada (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Kwenye mada hii tutajifunza shahada mbili,tafsiri ya shahada kstika maisha ya kila siku.
Soma Zaidi...Ni kipi chanzo cha Elimu, na ni kwa namna gani Allah hufundisha Elimu kwa wanadamu?
Soma Zaidi...Waumini wanawajibika kuwatunzia mayatima mali zao na kuwakabidhi wanapofikia baleghe yao baada ya kuwajaribu na kuthibitisha kuwa wanao uwezo wa kutunza mali zao - Rejea Qur-an (4:5-6).
Soma Zaidi...Si zinaa tu iliyoharamishwa bali hata yale yote yanayotengeneza mazingira na kuchochea kufanyika kwa zinaa nayo pia yameharamishwa.
Soma Zaidi...Hawamuogopi au kumtegemea yeyote kinyume na Mwenyezi Mungu.
Soma Zaidi...