Masiku ya Tashiq, kuchinja na kufanya tawafu ya kuaga

8.

Masiku ya Tashiq, kuchinja na kufanya tawafu ya kuaga

8.Siku ya Kuchinja (10 Dhul-Hija)



Mwezi 10 Dhul-Hija, siku ya kuchinja na siku ya Idd ni siku yenye shughuli nyingi kwa mwenye kuhiji. Siku hii Haji analazimika kutekeleza matendo manne ya nguzo za Hija kwa utaratibu ufuatao:



Kutupa mawe kwenye Mnara Mkubwa - Jamaratul Aqaba Kuchinja mnyama kwa wenye kuhiji Hija za Al-tamatta na Al-Qiran. Kunyoa kichwa na Kutufu tawaful ifadha (Tawaf ya nguzo).


Huu ndio utaratibu alioufuata Mtume (s.a.w) katika Hijja ya kuaga, lakini endapo kwa sababu moja au nyingine Haji hakuweza kufuata utaratibu huu, hapatakuwa na ubaya wowote. Kwa mujibu wa Hadith kadhaa jambo muhimu ni kutekeleza vitendo vyote vinne katika siku hiyo hiyo ya 10 Dhul Hija.
9.Siku za Tashriq (Ayyamut Tashriq)



Siku za Tashriq ni siku za mwezi 11, 12 na 13 Dhul Hija. Katika siku hizi Hajj hubakia Mina kwa madhumunni ya kumkumbuka na kumtukuza sana Allah (s.w) na kutupa mawe kwa kulenga minara yote mitatu - Mnara wa kwanza, Mnara wa kati na Mnara Mkubwa. Kila mnara hulengwa vijiwe saba kwa kila siku. Haji akitupa kila kijiwe husema: ALLAHU AKBAR. kipindi kinachojuzu kutupa mawe ni baada ya kuingia Adhuhur mpaka kuchwa jua.



Na mtajeni Mwenyezi Mungu katika zile ziku zinazohisabiwa. Lakini afanyaye haraka katika siku mbili (akarejea) basi si dhambi juu yake, na mwenye kukawia pia si dhambi juu yake kwa mwenye kumcha Mw enyezi Mungu. Na mcheni Mw enyezi Mungu na jueni kw amba nyinyi mtakusanywa kwake. (2:203).
Katika aya hii tunajifunza kuwa endapo Haji atakuwa na haraka ya kurejea nyumbani basi anaruhusiwa kuondoka siku moja kabla, yaani anaweza kuondoka mwezi 12 Dhul Hija baada ya kulenga mawe katika minara mitatu.



Khutuba katika siku za Tashriq ni jambo muhimu. Mtume (s.a.w) katika siku hizi za Tashriq alitoa khutuba za kuwakumbusha Waislamu mambo mbali mbali ya msingi juu ya Uislamu.



10 Tawaful Widaa (Tawaf ya Kuaga)
Baada ya Haji kukaa Mina siku tatu za Tashriq au siku mbili kama atakuwa na haraka ya kuondoka, atarejea Makka na kufanya Tawaful Widaa (Tawafu ya Kuaga). Tawaf hii hufanywa baada ya Haji kuwa tayari kuondoka na ni tendo la wajibu lakini si nguzo. Tawaf hii kama ilivyokuwa Tawaful ifadha haina “Ramal” wala “Iztibaa”. Baada ya Tawaf hii hapana Sai. Kwa wale waliofanya Hija ya aina ya Ifraad (walionuia Hijja tu), baada ya kurejea Makka kutoka Mina wanaweza kuvaa Ihram tena na kunuia ‘Umra. Baada ya kufanya ‘Umra ndio watafanya Tawaful Wadaa iwapo watakuwa tayari kuondoka.



Kama tunavyojifunza katika Hadith, wanawake wenye hedhi, iwapo watakuwa wamekamilisha matendo yote ya nguzo za Hija, wanaruhusiwa kuondoka bila ya kufanya Tawaful-Wadaa.




                   


Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Fiqh Main: Dini File: Download PDF Views 1145

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi    👉2 Simulizi za Hadithi Audio    👉3 Kitabu cha Afya    👉4 Kitau cha Fiqh    👉5 Madrasa kiganjani    👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)   

Post zinazofanana: