Hukumu ya Muislamu Aliyeacha Kufunga kwa Makusudi
Japo kadha ya Ramadhani inaruhusiwa kwa yule aliyeruhusiwa kutofunga kutokana na udhuru wa kisheria, kadha haitajuzu kwa mtu aliyeacha makusudi, kwani hata akifunga mwaka mzima hawezi kuilipia siku hiyo moja aliyoacha kufunga pasi na udhuru kwa ushahidi wa Hadith ifu atayo:
Abu Hurairah (r.a) amesema kuwa Mtume (s.a.w) amesema: Mwenye kula siku moja ya Ramadhani bila ya ruhusa iliyotolewa na Mwenyezi Mungu, basi Swaum hiyo hailipiki hata akifunga mwaka mzima. (Abu, Daud, Ibn Majah n a Tirm idh).
Fundisho kubwa tunalolipata hapa ni kuwa kuacha makusudi kutekeleza amri ya Allah katika wakati wake uliowekwa ni jambo baya sana hata kama utatekeleza amri hiyo wakati mwingine. Ikumbukwe kuwa anachokiangalia Allah (s.w) si utekelezaji wa vitendo tu, bali huangalia na kumlipa mja kutokana na utii na unyenyekevu katika kufanya kitendo alicho kiamrisha.
Umeionaje Makala hii.. ?
Hapa utajifinza uharamu wa riba na sababu za kuharamishwa kwake.
Soma Zaidi...Fahamu darsa mbalimbali za fiqh kama swala, twahara, zaka pamoja na funga. Zijuwe sharti za swala, funga na zaka.
Soma Zaidi...Maana ya elimuElimu ni ujuzi ulioambatanishwa na utendaji.
Soma Zaidi...Yajuwe mambo ambayo yanapendeza kuyafanya wakati ukiwa umefunga Ramadhani.
Soma Zaidi...Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Sunnah za SwalaSunnah za Swala Vipengele vya sunnah katika swala ni vile ambavyo mwenye kuswali akivitenda husaidia sana kukuza daraja ya swala yake na kuipa nguvu na msukumo mkubwa wa kuiwezesha kufikia lengo lililokusudiwa kwa urahisi zaidi.
Soma Zaidi...