KUAMINI MITUME WA ALLAH (S.W)
Mtu hawi Muumini wa kweli mpaka awe na yakini juu ya Mitume wa Allah (s.
KUAMINI MITUME WA ALLAH (S.W)
Mtu hawi Muumini wa kweli mpaka awe na yakini juu ya Mitume wa Allah (s.w) kama tunavyojifunza katika Qur-an:“Semeni nyinyi (Waislamu kuwaambia Mayahudi na Wakristo kuw a): “Tumemw amini Mw enyezi Mungu na yale tuliyoteremshiwa, na yale yaliyoteremshwa kwa Ibrahimu, na Ismail na Is-haqa na Yaaqubu na kizazi (chake Yaaqubu); na waliyopewa Manabii (wengine) kutoka kwa Mola wao; hatutafautishi baina ya yoyote katika hao.
(Wote tunawaamini), na sisi tumenyenyekea kwake.” (2:136)Kuamini baadhi ya Mitume wa Mwenyezi Mungu na kuwakanusha wengine kama walivyo fanya mayahudi na Wakristo ni Ukafiri kama tunavyojifunza katika Qur-an:
“Hakika wale wanaomkanusha Mwenyezi Mungu na Mitume yake, na wanataka kutenga baina ya Mwenyezi Mungu na Mitume yake, kwa kusema: “Wengine tunawaamini na wengine tunawakataa, ” na wanataka kushika njia iliyo kati kati ya haya (si ya Kiis lam u kh as a w ala y a Kikafiri).
Hao ndio Makafiri kweli.Na tumewaandalia makafiri adhabu idhalilishayo.(4:150-151).
Na waliomwamini Mwenyezi Mungu na Mitume yake wala wasimfarikishe yoyote katika wao (bali wamewaamini wote), hao atawapa ujira wao. Na Mw enyezi Mungu ni Mw ingi w a kusamehe (na) Mw ingi wa kurehemu.” (4 :152).
“Na kwa yakini tuliwatuma mitume kabla yako (Muhammad). Wengine katika hao tumekusimulia (majina yao na habari zao) na wengine hatukukusimulia...” (40:78)
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Dua za Mitume na Manabii 👉2 Madrasa kiganjani 👉3 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉4 Kitabu cha Afya 👉5 ai web app 👉6 Kitau cha Fiqh
Post zinazofanana:
Njia anazotumia Mwenyezi Mungu (s.w) kuwafundisha na kuwasiliana na wanaadamu
Ni zipo njia wanazotumia Allah katika kuwasiliana na kuwafundisha wanadamu? (EDK form 1: Dhana ya elimu katika Uislamu).
Soma Zaidi...Kuamini vitabu vya mwenyezi Mungu (s.w)..
Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...