Masharti ya Kuoga
Masharti ya kuoga ni sawa tu na yale masharti ya udhu ila hapa yanahusu mwili mzima.
Nguzo za Kuoga
Kwanza, kutia nia moyoni kuwa unaoga kwa madhumuni ya kujitwaharisha, kutokana na janaba, hedhi, au nifasi. Mahali pa nia ni moyoni na wakati wa kunuiwa ni pale unapoanza kuosha kiungo cha kwanza.
Pili, kueneza maji mwili mzima. Ili kuhakikisha kuwa umeeneza maji mwili mzima ni vyema ufuate mafundisho ya Mtume (s.a.w). Mtume katika kuoga alikuwa akianza kwa kuosha sehemu za siri, kisha alikuwa akitia udhu, kisha alikuwa akijimiminia maji kichwani mara tatu, kisha alikuwa akieneza maji mwili mzima kwa kuanzia upande wa kulia na kumalizia upande wa kushoto, pote mara tatu tatu.
Umeionaje Makala hii.. ?
Aina za Swala za Sunnah.
Soma Zaidi...Hapa nitakujulisha kuhusu swala ya kuomba mvia, na taratibu za kuiswali.
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu lengo la funga na maana yake katika uislamu.
Soma Zaidi...