KutayammamuKutayammamu ni kujitwaharisha kwa kutumia udongo safi. Waislamu huruhusiwa kujitwaharisha kwa kutayammamu katika hali ya dharura ya:
(i)Ugonjwa usioruhusu kutumia maji.
(ii)Kuwa safarini na kukosa maji ya kutumia au kuwa katika mazingira ya safari yasiyoruhusu kutumia maji.
(iii)Kukosa maji.
Tunajifunza haya katika aya ifuatayo:


“Na mkiwa wagonjwa au mumo safarini au mmoja wenu ametoka chooni au mmeingiliana na wanawake, na hamkupata maji, basi, kusudieni udongo ulio safi (tayammamuni) kwa kuzipaka nyuso zenu na mikono yenu. Hapendi Mw enyezi Mungu kukutieni katika taabu; bali anataka kukutakaseni na kutimiza neema Yake juu yenu ili mpate kushukuru”. (5:6)Katika aya hii tunajifunza kuwa kutayammamu kumeruhusiwa kwa wakati wa dharura tu. Funzo hili tunalipata katika maneno ya Allah kuwa, “Hapendi Allah kukutieni katika taabu”Masharti ya KutayammamuTayammamu haitaswihi mpaka yatakapozingatiwa masharti yafuatayo:
1. Ipatikane dharura inayompelekea mtu kuruhusiwa kutayammarnu.
2. Pawe na hitajio la tayammamu kama vile kuswali, kutufu n.k.
3. Kama kusudio la kutayammarnu ni kutekeleza swala ya faradh, tayammamu hiyo ifanyilce baada ya kuingia wakati wa swala hiyo.
4. Pawe na udongo safe (ulio twahara na ulio katika asili yake) ulio mkavu na wenye vumbi vumbi.


Nguzo za Tayammam
Nguzo za tayammam zinabainishwa na aya ifuatayo:
`... Basi kusudieni udongo ulio safi na kupaka nyuso zenu nn mikono yenu..." (4:43)
Aya hii inabainisha kuwa nguzo za tayammam ni:(i)Nia (kukusudia udongo).
(ii)Kupaka uso.
(iii)Kupaka mikono.
(iv)Kufuata utaratibu huu.
Nampa ya Kutayammamu
(i)Kutia nia. Nia huwekwa pale Muislamu anapokusudia udongo na kuutayarisha kwa ajili ya tayammamu.
(ii)Kupaka uso. Piga udongo uliokusudia kwa viganja vyote viwili vya mikono, kisha puliza viganja iii takataka na vijiwe jiwe vilivyo juu yake vitoke. Kisha paka uso wako kwa kutumia viganja viwili kwa pamoja.(iii) Kupaka mikono. Anza kupaka mkono wa kulia kwa kiganja cha kushoto. Weka kiganja cha kushoto nyuma ya kiganja cha kulia. Paka mkono wa kulia kuanzia hapo kwa kurudisha kiganja cha kushoto kinyume nyume mpaka kwenye fundo kisha kupaka sehemu ya juu ya mkono wa kulia na kuishia kwenye kidole gumba bila ya kuugusa kiganja mkono wa kulia. Utarudia zoezi hilo kupaka mkono wa kushoto.Kutumia Ukuta kwa Ajili ya TayammamuMtume (s.a.w) aliwahi kutayammamu kwa kutumia ukuta wa nyumba kama inavyobainika katika hadith ifuatayo:
“Abu Juhaim Al-A nsary (r.a) amehadithia kuw a Mtume w a Allah (Rehema na amani ziwe juu yake) alikuja kutoka upande wa Bir-al-Jamal. Mtu mmoja alimuona akamsalimia. Lakini Mtume hakumjibu, bali alienda kwenye ukuta wa nyumba akapakaza viganja vyake vumbi la ukuta kisha akapaka uso wake wote, kisha mkono wa kulia na wa kushoto, ndipo akamrudishia salamu ”. (Bukhari na Muslim).Kutokana na hadithi hii tunajifunza kuwa vumbi kwa ajili ya tayammamu si lazima liwe la ardhini tu bali ukuta au jiwe au sehemu yoyote yenye vumbi vumbi iliyotwahara inafaa kutumika kwa ajili ya tayammamu. Kwa mfano wakati wa mvua ambapo udongo umelowana ukuta wa nyumba au ukuta wa chombo cha usafiri au sehemu yoyote yenye vumbi vumbi au iliyokavu na twahara, itakuwa aula kuitumia kwa tayammamu.