Post hii inakwenda kukufundisha jinsi ya kuoga josho kisheria.
Masharti ya Kuoga
Masharti ya kuoga ni sawa tu na yale masharti ya udhu ila hapa yanahusu mwili mzima.
Nguzo za Kuoga
Kwanza, kutia nia moyoni kuwa unaoga kwa madhumuni ya kujitwaharisha, kutokana na janaba, hedhi, au nifasi. Mahali pa nia ni moyoni na wakati wa kunuiwa ni pale unapoanza kuosha kiungo cha kwanza.
Pili, kueneza maji mwili mzima. Ili kuhakikisha kuwa umeeneza maji mwili mzima ni vyema ufuate mafundisho ya Mtume (s.a.w). Mtume katika kuoga alikuwa akianza kwa kuosha sehemu za siri, kisha alikuwa akitia udhu, kisha alikuwa akijimiminia maji kichwani mara tatu, kisha alikuwa akieneza maji mwili mzima kwa kuanzia upande wa kulia na kumalizia upande wa kushoto, pote mara tatu tatu.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu mambo ambauo ni haramu kwa mtu asiye na udhu.
Soma Zaidi...Lengo la Kusimamisha SwalaBila shaka swala imepewa umuhimu mkubwa kiasi cha kufanywa nguzo kubwa ya Uislamu kutokana na lengo lake.
Soma Zaidi...Hapa utajifunza njia ambazo nenk ya kiislamu hutumia ili kujiendesha
Soma Zaidi...Post hii itakufundisha faida na umuhimu wa kijenga uchumi katika jamii ya kiislamu.
Soma Zaidi...