image

MAMBO YANAYOBATILISHA (HARIBU) SWALA YAKO

Lugha ya Swala Lugha ya swala,kuanzia kwenye Takbira ya kuhirimia Swala mpaka kumalizia swala kwa Salaam, ni Kiarabu.

MAMBO YANAYOBATILISHA (HARIBU) SWALA YAKO

Lugha ya Swala Lugha ya swala,
kuanzia kwenye Takbira ya kuhirimia Swala mpaka kumalizia swala kwa Salaam, ni Kiarabu. Hekima yake iko wazi. Kiarabu ndio lugha ya Qur-an tukufu na kwa hiyo ndio lugha rasmi ya Kiislamu inayowaunganisha Waislamu wote ulimwenguni. Waislamu ni umma mmoja tu na Waislamu wote ni ndugu moja wasio baguana kwa lugha, rangi, taifa wala ubaguzi mwingine wa aina yoyote ile.Muislamu yeyote anaweza kuwa Imamu mahali popote ilimradi tu awe anatekeleza masharti ya Uimamu. Muislamu hana msikiti maalum. Misikiti yote ni yake na anaweza kuswali kwenye msikiti wowote ulimwenguni bila ya kupata tatizo lolote la lugha. Kwa sababu hii kila Muislamu inabidi ajifunze kiasi cha uwezo wake kutamka, kwa Kiarabu yale yote tuyasemayo katika swala.

Mambo yanayobatilisha Swala
Mtu akiwa katika swala yuko katika hali maalum na haruhusiwi kufanya kitu kingine nje ya swala hata vile vitendo vya kawaida alivyovizoea. Hivyo ukiwa ndani ya swala ukifanya au kukitokea moja ya mambo yafuatayo, swala yako itakuwa imebatilika na itabidi uanze upya.
(a) Kutoelekea Qibla kwa kifua pasi na dharura yoyote ya kisheria. (b) Kupatikana na hadathi kubwa, ndogo au ya kati na kati.
(c) Kufikwa na najisi mwilini, nguoni au mahali pa kuswalia.
(d) Kuvukwa na nguo ukawa uchi. Wanaume wanaovaa shati fupi wajihadhari sana hapa kwani,hasa wakati wa kurukuu na kusujudu, migongo yao (viuno vyao) chini ya usawa wa kitovu (panda za makalio) huwa wazi na hivi huhesabiwa kuwa wako uchi.
(e) Kusema au kutamka makusudi lau herufi moja yenye kuleta maana nje ya maneno ya swala.Mtume (s.a.w) amesema: gHakika ya hii swala, haifai ndani yake maneno ya watu kwani swala yenyewe ni Tasbih, Takbir na kusoma Qur-an. (Muslim)
(f) Kula au kunywa japo kwa kusahau. (g) Kufanya jambo lisilowiana na swala mfululizo mara tatu. (h) Kuiacha nguzo yoyote ya swala
(i) Ukizidisha nguzo yoyote ya swala makusudi.
(j) Kumtangulia Imam au kuchelewa kwa nguzo mbili za kimatendo kwa makusudi.
(k) Kutia nia ya kuikata swala au kujishauri moyoni kuwa uikate au usiikate swala.
(l) Kuwa na shaka kuwa umetimiza au hujatimiza sharti au nguzo yoyote ya swala.
(m) Kupotewa na akili au kulala ndani ya swala.
(n) Kutoa Salaam kwa makusudi kabla ya kwisha swala.
(o) Kuswalishwa na asiyekuwa Muislamu.
(p) Kukhalifu utaratibu wa nguzo za swala, yaani kutangulia kutekeleza nguzo ya swala kabla ya kutekeleza nguzo inayostahiki kutangulia katika utaratibu wa swala.
(q) Kuleta dua ya kuomba kitu haramu au muhali.
(r) Kumshirikisha Allah (s.w) katika kuleta dua yaani kuleta dua ya kuomba kitu cha halali lakini humuombi Allah (s.w) peke yake.

Dua na Dhikri Baada ya Swala
Ni vizuri mara Muislamu anapomaliza kuswali kama hana dharura yoyote asiondoke bila ya kuleta Dhikri na dua kama alivyofundisha Mtume (s.a.w), kwani zina umuhimu mno katika kumsaidia mja kufikia lengo la swala na lengo la kuumbwa kwake kwa ujumla iwapo atayafahamu na kuyazingatia yale anayoyatamka. Kutokana na Hadithi iliyosimuliwa na Samura bin Jandab(r.a) na kupokelewa na Bukhari(r.a), baada ya swala Mtume (s.a.w) aliwageukia Waislamu aliokuwa akiwaswalisha. Kisha aliomba maghfira (msamaha) mara tatu na kuongezea maneno yaliyoelezwa katika Hadithi zifuatazo: Thawban (r.a) amesimulia kuwa Mtume (s.a.w) alipomaliza swala aliomba maghfira (msamaha) mara tatu kwa kusema: Astagh-firullah (Mara tatu) Ninaomba msamaha kwa Allahh na kusema “Allahumma Antassalam waminkas-salaam Tabaarakta YaaDhal jallaali Wal-ikraam.” Ewe Allah, wewe ni Amani, na kwako ndiko iliko Amani. Wewe ndiye Mbariki Ewe Mwenye Utukufu na Heshima (Muslim)

Baada ya nyiradi hizi, ni vizuri pia kuomba dua yoyote kulingana na haja zako kwa lugha yoyote. Jambo hili la kuomba dua baada ya swala, umuhimu wake unadhihirika katika hadithi ifuatayo: Abu Umamah amesimulia kuwa: Iliulizwa: Ee Mtume wa Allah. ni dua gani ambayo hukubaliwa zaidi?h (Mtume) alijibu: (moja) ni ile ya katikati ya nusu ya pili ya usiku na (pili) kila baada ya swala ya faradhi. (Tirmidh)

Hivyo ni jambo la msingi mno kuomba dua yoyote kila baada ya swala na dua zilizo nzito zaidi ni zile zilizomo kwenye Qur-an na hadithi za Mtume (s.a.w). Kwa mfano ni vizuri kila baada ya swala, au baada ya dhikri zilizotajwa tuombe dua ifuatayo: Rabii ij’alnii muqiimas-swalaati wamindhurriyyatii Rabbana Wataqabbal du’aaai. Mola wangu! Nijaalie niwe msimamishaji swala, na kizazi changu! (Pia kiwe hivi). Mola wetu! Na upokee maombi yangu mengine... (14:40-41).


                   





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Fiqh Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 821


Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉4 Kitau cha Fiqh     👉5 Simulizi za Hadithi Audio     👉6 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Haya ndio yanayobatilisha Hija
Soma Zaidi...

Aina za talaka, sharti zake na taratibu za kutaliki katika uislamu
Maana: ni utaratibu wa kuvunja mkataba wa ndoa baina ya mume na mke mbele ya mashahidi wawili kwa kuzingatia sheria ya Kiislamu. Soma Zaidi...

ijuwe maawe maan ya kusimamisha swala
Soma Zaidi...

Sera ya uchumi katika Uislamu
4. Soma Zaidi...

Ni upi umuhimu wa kufunga katika uislamu
Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu umuhimu wa kufunga kiroho, kiafya na kijamii. Soma Zaidi...

Umuhimu na nafasi za hijjah katika uislamu
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Ni kwa nini riba imeharamishwa kwenye Uislamu
Hapa utajifinza uharamu wa riba na sababu za kuharamishwa kwake. Soma Zaidi...

Eda ya kufiwa na hukumu zake
Soma Zaidi...

Hii ndio namna ya kuswali kama alivyoswali Mtume s.a.w
Mtume (s. Soma Zaidi...

Ni mambo gani yanaharibu na kutengua udhu?
Soma Zaidi...

Funga za kafara
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Mafungu ya urithi katika uislamu
Hspa utajifunza viwango maalumu vya kutithi mirathi ys kiislamu. Soma Zaidi...