Hadathi Kubwa:Hadath kubwa huwapata wanawake tu wanapokuwa na Hedhi (damu ya mwezi) au Nifasi (damu ya uzazi).
Yafuatayo yameharamishwa kwa wenye hadath kubwa:(i)Kusali na Kutufu.
(ii)Kukaa Msikitini.
(iii)Kusoma Qur’an, kugusa na kuchukua msahafu (Qur-an)
(iv)Kufunga.
(v)Kufanya kitendo cha ndoa.
(vi)Kutalikiwa (kupewa talaka).Namna ya kujitwaharisha na hadath ya kati na kati na hadath kubwa ni kukoga kwa maji safi kwa kutekeleza masharti na nguzo za kukoga josho la wajibu.Masharti ya Kuoga
Masharti ya kuoga ni sawa tu na yale masharti ya udhu ila hapa yanahusu mwili mzima.