Hukumu ya Muislamu Aliyeacha Kufunga kwa MakusudiJapo kadha ya Ramadhani inaruhusiwa kwa yule aliyeruhusiwa kutofunga kutokana na udhuru wa kisheria, kadha haitajuzu kwa mtu aliyeacha makusudi, kwani hata akifunga mwaka mzima hawezi kuilipia siku hiyo moja aliyoacha kufunga pasi na udhuru kwa ushahidi wa Hadith ifu atayo:Abu Hurairah (r.a) amesema kuwa Mtume (s.a.w) amesema: Mwenye kula siku moja ya Ramadhani bila ya ruhusa iliyotolewa na Mwenyezi Mungu, basi Swaum hiyo hailipiki hata akifunga mwaka mzima. (Abu, Daud, Ibn Majah n a Tirm idh).


Fundisho kubwa tunalolipata hapa ni kuwa kuacha makusudi kutekeleza amri ya Allah katika wakati wake uliowekwa ni jambo baya sana hata kama utatekeleza amri hiyo wakati mwingine. Ikumbukwe kuwa anachokiangalia Allah (s.w) si utekelezaji wa vitendo tu, bali huangalia na kumlipa mja kutokana na utii na unyenyekevu katika kufanya kitendo alicho kiamrisha.