MAANA YA ZAKA NA SADAKA KULUNGA NA KISHERIA PAMOJA NA TOFAUTI ZAO.
MAANA YA ZAKA NA SADAKA KULUNGA NA KISHERIA PAMOJA NA TOFAUTI ZAO.
Maana ya Zakat
Kilugha: Katika lugha ya Kiarabu neno “zakat” lina maana ya utakaso (Purification). Neno “Zakat” limetumika katika Qur’an kwa maana hii katika aya zifuatazo:
“Bila shaka amefuzu aliyeitakasa (nafsi yake)” (91 :9).
“Hakika ameshafuzu aliyejitakasa (na mabaya)” (8 7:14).
Kisheria: Katika sheria ya Kiislamu “Zakat” ni sehemu ya mali ya tajiri (2.5% au 1/40) anayoitoa kwa kutekeleza amri ya Allah (s.w) na kuwapa wanaostahiki, baada ya kupindukia mwaka au baada ya mavuno iwapo mali hiyo imefikia Nisaab. Nisaab ni kima cha chini cha mali ambacho mtu akiwa nacho au zaidi yake analazimika kutoa Zakat.
Maana ya Sadaqa
Kilugha: Katika lugha ya Kiarabu neno “Sadaqa” linatokana na “Sidiq” lenye maana ya ukweli.
Kisheria: Katika sheria ya Kiislamu Sadaqat ni mali au huduma iinayotolewa au kupewa mtu yoyote anayehitajia kwa ihsani tu bila ya kutarajia malipo yoyote kutoka kwake. Maana ya “Sadaqat” inabainishwa vizuri katika Hadithi zifuatazo:
1.Jabir na Hudhaifa (r.a) wameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: Kila kitendo kizuri ni Sadaqat”. (Bukhari na Muslim).
2.Abu Hurairah (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: Katika kila kiungo cha mtu kuna Sadaqat. Kuna Sadaqat katika kila mtu. Kufanya uadilifu kati ya watu wawili ni sadaqat; kumsaidia mtu kupanda mnyama wake anayesafiri naye au kumsaidia mtu kutwika mzigo wake ni sadaqat; neno zuri ni sadaqat na kila hatua mtu anayotembea kwenda kwenye swala ni sadaqat na kuondoa kitu kibaya njiani ni sadaqat”. (Bukhari na Muslim).
TOFAUTI YA ZAKA NA SADAKA
1. Zaka ni nguzo ya Uislamu na ni lazima, lakini dadaka si lazima
2. Zaka hutolewa kwa kiwango maalumu, lakini sadaka haina kiwango maalumu
3. Zaka hutolewa mali, lakini sadaka sio lazima iwe mali
4. Zaka hutolewa ndani ya muda maalumu, lakini sadaka haina muda maalumu
5. Zaka inatolewa kwa watu maalumu, lakini sadaka haijaelezewa watu maalumu wa kuwapatia.
Umeionaje Makala hii.. ?
Je inapoonekana sehemu moja tufunge duania nzima ama tufunge kwa kuangalia mwandamo katika maenro tunayoishi.
Soma Zaidi...Posti hii itakufundisha masharti yanayohitajika kwa mwenye kutaka kutia udhu.
Soma Zaidi...Dhana ya uchumi wa kiislamu imejegwa jui ya ukati na kati. Dhana hii imetofautiana sana na dhana nyinginezo kama ubepari na ujamaa.
Soma Zaidi...Nguzo za uislamu,kutoa zakat na sadaqat (EDK form 2; dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...