Navigation Menu



image

namna ya kuswali swala ya msafiri, nguzo zake na hukumu zake

namna ya kuswali swala ya msafiri, nguzo zake na hukumu zake

Swala ya Msafiri



Kutokana na umuhimu wa kusimamisha swala hata mtu akiwa safarini analazimika kusimamisha swala. Lakini Allah (s.w) kwa Rehma yake ametuhafifishia swala tukiwa safarini kama ifuatavyo:-



Kwanza, tunaruhusiwa kutayammamu tukiwa safarini ili tuweze kusimamisha swala kama hatutapata maji au hatutaweza kutumia maji ndani ya chombo tunachosafiria. Ruhusa hii tunaipata katika aya ifu atayo:-


“.. Na mkiwa wagonjwa au mmo safarini, au mmoja wenu ametoka chooni au mmeingiliana na wanawake, na hamkupata maji, basi kusudieni (tayammam u) udongo safi na kupaka nyuso zenu na mikono yenu. Hapendi Mw enyezi Mungu kukutieni katika taabu, bali anataka kukutakaseni na kutimiza neema yake juu yenu ili mpate kushukuru” (5:6)



Pia inawezekana udongo usipatikane ndani ya chombo tunachosafiria. Ikiwa ni hivyo tunaruhusiwa kutumia kuta au dari ya chombo. Kwa maana nyingine tunaruhusiwa kupiga viganja vyetu juu ya ukuta au dari ya chombo au juu ya kitu chochote ndani ya chombo chenye vumbi vumbi na kupaka uso kwa pigo la kwanza kisha kupaka


mikono kwa pigo la pili kama kawaida ya kutayammamu. Mtume (s.a.w) alitumia ukuta kutayammamu kama tunavyofahamishwa katika Hadithi:
Amesimulia Abu Juhaim Al-Ansaari, Mtume (s.a.w) alitokea upande wa Bir Jamal. Mtu mmoja alikutana naye na akamsalimu. Lakini (Mtume) hakuitikia salaam hii mpaka alipokwenda kwenye ukuta na kupaka vumbi lake mikononi na usoni mwake (alipotayammamu) ndipo akarudishia salaam ile. (Bukhari).



Pili, msafiri anaruhusiwa kupunguza swala kama ilivyo katika aya ifuatayo:


“:Na mnaposafiri katika ardhi, si vibaya kwenu kama mkifupisha swala, iwapo mnaogopa ya kw amba wale w aliokufuru watakutaabisheni. Bila shaka makafiri ni maadui zenu dhahiri” (4:101)



Swala zinazofupishwa ni swala za rakaa 4 - Adhuhuri, Al-’asr na Al-Ishaai. Magharibi yenye rakaa 3 na subhi yenye rakaa 2 zinaswaliwa kwa ukamilifu. Ifahamike wazi kuwa kufupisha swala katika safari si lazima bali ni tahfifu tu iliyotolewa kwa wasafiri. Lakini ukiwa msafiri ni bora kutumia tahfifu hii kwani ni neema kutoka kwa Allah (s.w).
Ya-’Al bin Umayyah (r.a) amesimulia. “Nilisema kwa Umar bin Al-Khattab (r.a), Allah (s.w) amesema, “Mnaweza kufupisha swala iwapo mnahofia kuwa makafiri watawabughudhi”. Watu sasa wako katika amani. Umar akasema:“Nami pia ninashangaa kama wew e ”. Kisha nilimuuliza Mtume wa Allah alisema (Mtume): “Hii ni zawadi (neema) aliyokupeni Allah. Kw a hiyo pokeeni zaw adi yake ” (Muslim)



Ilikuwa ni kawaida ya Mtume (s.a.w) kufupisha swala kila alipokuwa safarini kama tunavyojifuna katika Hadithi zifuatazo:
Abdullah bin Umar (r.a) amehadithia kuwa alisafiri na Mtume (s.a.w), Abu Bakr (r.a), Umar (r.a) na Uthman (r.a) na kamwe hakuwaona kabisa kuswali zaidi ya rakaa mbili katika swala za rakaa nne ndani ya safari. (Muslim)


Anas (r.a)ametuhadithia kuw a Mtume w a Allah alisw ali dhuhuri akiwa Madina kwa rakaa nne na aliswali Asr akiwa Zul-Hulaifah kwa rakaa mbili (Bukhari na Muslim)
Kuhusiana na masafa ambayo mtu anaruhusiwa kupunguza swala ni vyema tunukuu maelezo yaliyoandikwa na Sheikh Sayyid Sabiq katika Kitabu chake Fiqhus-Sunnah yaliyo chini ya mlango aliouita swala ya Msafiri:



“Hitimisho tunalolipata kutokana na aya ya Qur-an ni kuwa safari yoyote ile, iwe ndefu au fupi maadamu inakubalika katika maana ya kilugha ya safari basi inatosha kwa mtu kupunguza sala, kuchanganya sala au kutokufunga.Katika Sunnah (hadith) hakuna chochote kilichoripotiw a kuhusisha maana hii ya jumla na maana maalum ”.
Ibn Al-Mundhir na wanazuoni wengine wametaja zaidi ya wapokezi ishirini kuhusiana na jambo hili.



Vile vile kuna suala la muda gani mtu anaruhusiwa kupunguza swala akiwapo safarini. Katika hadithi zifuatazo tunajifunza kuwa msafiri atafupisha swala kwa muda wote atakaokuwa safarini hadi atakaporejea kwao.



Anas (r.a) amehadithia; Tulisafiri na Mtume (s.a.w) kutoka Madinah kwenda Makka. Alikuwa akiswali kila swala kwa rakaa mbili, mpaka aliporejea Madina. Waliulizwa, mlikaa Makka kwa muda kid ogo? Alijibu. Tulikaa pale kwa siku kumi” (Bukhari).



Ibn Abbas(r.a) amesimulia kuwa Mtume (s.a.w) alisafiri na alikaa humo safarini (ugenini) kwa muda wa siku kumi na tisa akiswali rakaa mbili mbili. Ibn Abbas amesema, kwa hiyo tuliswali rakaa mbili kila w akati tukiw a tunaelekea Makka kwa siku 19. Tulipokaa zaidi ya muda huo tuliswali rakaa nne.(Bukhari)



Imraan bin Husain (r.a) ameeleza: Nilikuwa pamoja na mtume (s.a.w) katika vita vya Jihad na kushuhudia ushindi tukiwa pamoja naye. Alikaa Makka siku 18 akiswali kila swala kwa rakaa mbili, akisema “Nyinyi w enyeji swalini rakaa nne. Sisi tu wasafiri”. (Abu Daud).



Kutokana na hadithi hizi tunajifunza kuwa hapana muda maalum uliowekwa kwa msafiri kupunguza swala. Pia tunajifunza kuwa mtu anaye swali swala ya safari anaweza kuwa Imamu ila ni vyema awafahamishe wale wanaomfuata ili yeye akitoa salaam baada ya rakaa mbili wale wakazi wa mji waendelee na kuikamilisha swala kwa rakaa nne. Lakini msafiri akiamua kumfuata Imamu mkazi itabidi akamilishe swala kwa rakaa nne kama Imamu.



Tatu, msafiri pia amepewa tahfifu katika swala kwa kupewa ruhusa ya kukusanya swala mbili za faradhi na kuziswali kwa wakati mmoja kama tunavyojifunza kutokana na Hadithi zifuatazo:



Ibn Abbas(r.a) amehadithia kuwa Mtume wa Allah alikuwa akichanganya Dhuhur na Asr w akati akitoka safarini, pia alichanganya Magharibi na Isha. (Bukhari).



Mua ’dhi bin Jabal (r.a) amesimulia kuwa Mtume (s.a.w) alikuwa katika vita vya Tabuk. Jua lilipopinduka kid ogo aliswali Dhuhuri pamoja na Asr. Kama alianza safari kabla ya jua kupinduka (kabla ya wakati wa dhuhur) aliakhirisha Dhuhur mpaka wakati wa Asr. Hali kadhalika kwa swala ya Magharibi, jua lilipotua kabla hajaanza safari, aliswali magharibi pamoja na isha, na kama alianza kusafiri kabla ya jua kutua; aliakhirisha Magharibi mpaka wakati wa isha na kuzisw ali pamoja. (Abu Daud, Tirmidh).



Kutokana na Hadithi hizi msafiri anaruhusiwa kuchanganya Adhuhuri na Asr kuziswali wakati mmoja, pia anaruhusiwa kuswali Magharibi na Isha kwa wakati mmoja, ila swala ya Alfajiri haichanganyiki na swala yoyote na wakati wake ni ule ule wa kawaida.



Kuna aina mbili za mkusanyo na zote zinajuzu. Aina ya kwanza huitwa Jam-’u Taqdym. Katika aina hii unazikusanya swala mbili katika wakati wa swala ya mwanzo. Yaani kwa kuswali Adhuhuri na ‘Asr pamoja katika wakati wa Adhuhuri kwa adhana moja na Iqama mbili. Hivyo hivyo utaswali magharibi na isha katika wakati wa Magharibi.
Aina ya pili huitwa Jam ’u Ta-akhir. Katika aina hii unazikusanya swala mbili katika wakati wa swala inayofuatia. Yaani msafiri ataswali Adhuhuri na Asr pamoja katika wakati wa Al-’Asr kwa adhana moja na Iqama mbili. Hali kadhalika ataswali Magharibi na Ishaa kwa pamoja katika wakati wa Ishaa.



Namna ya kuswali swala za mkusanyo wa Adhuhuri na al-’Asr, ukisha-adhini na kukimu utaanza kuswali rakaa mbili za Adhuhuri. Baada ya kutoa Salaam utasimama na kukimu tena kisha utaswali rakaa mbili za Al-’Asr.



Kama unaswali Jam-’u Ta-akhir ya mkusanyo wa Magharibi na Ishaa, baada ya kuadhini na kukimu, utaanza kuswali rakaa tatu za Magharibi kama kawaida. Baada ya kutoa salaam utasimama na kukimu tena na kisha utaswali rakaa mbili za Isha.


Kama tunavyojifunza katika Hadithi uamuzi wa kukusanya swala katika wakati wa swala ya mwanzo (Jam-’u Taqdym) au katika wakati wa swala inayofuatia (Jam’uta-Akhr) utategemeana na hali ya safari kama tunavyojifunza katika Hadithi ifuatayo:-



Abdullah ibn Abbas(r.a) amesema: “Mwenendo wa Mtume (s.a.w) ulikuwa kabla hajaanza safari akiona kuw a jua limepindukia (wakati w a Adhuhuri umeingia) alikuwa akisw ali Adhuhuri na al-Asr na kisha huanza safari yake vinginevyo akiona, kuwa bado jua halijapinduka, basi huianza safari yake na mbele ya safari akiswali Adhuhuri na al-’Asr katika wakati wa Al-’Asr. Hivyo hivyo akiona jua limeshazama alikuwa akiswali Magharibi na Ishaa wakati huo wa Magharibi kabla ya kuanza safari, na kama jua bado halijazama basi huanza safari yake kisha huswali Magharibi na Ishaa wakati wa Isha. (Ahmad)



Nne, msafiri pia amefanyiwa wepesi wa kusimamisha swala, kwa kuruhusiwa kuswali huku anatembea au anaendelea na safari juu ya kipando au chombo anachosafiria. Ruhusa hii tunaipata katika aya zifu atazo:-



Hifadhini swala na swala ya kati na kati. Na simameni kwa unyenyekevu katika kumuabudu Mwenyezi Mungu. Na kama mkiwa na khofu (basi swalini) na hali ya kuwa
mnakwenda kwa miguu au mmepanda vipando. Na mtakapokuwa katika amani, basi mkumbukeni Mwenyezi Mungu (swalini) kama alivyokufunzeni yale mliyokuw a hamyajui”. (2:238-239)



Pia Hadithi ifuatayo inatufahamisha juu ya swala ya Mtume (s.a.w) juu ya kipando:
Ibn Umar (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah alipokuwa safarini alikuwa akisw ali Ishaa juu ya ngamia katika upande wow ote ule atakapoelekea, akiswali kwa ishara wakati wa usiku ila kwa swala za faradhi na alikuw a akisw ali witri juu ya ngamia anayetembea. (Bukhari, Muslim)



Ilivyo ni kwamba msafiri anaruhusiwa kuswali juu ya kipando huku anaendelea na safari. Namna ya kutekeleza swala hii ni kwamba, baada ya msafiri kutawadha au kutayammamu, ikiwa anasafiri kwa mguu au


kwa mnyama na anaona hofu ya kuvamiwa na maadui au wanyama, atafunga swala akiwa ameelekea Qibla, kisha ataendelea na swala huku anatembea akiwa ameelekea kule anakokwenda. Ataswali kwa ishara tu. Ikiwa msafiri anasafiri, kwa chombo kama vile gari, meli, ndege n.k atatawadha au atatayammamu, kisha atakaa na kuelekea popote pale kiti chake kinavyomruhusu, kisha ataadhini na kukimu na kuswali kwa ishara kama vile kuinamisha kichwa na kuinua katika kuashiria visimamo, rukuu, itidali, sijda na vikao. Inapendekezwa kuwa mtu ainamishe kichwa zaidi kwa sijda kuliko vile anavyoinamisha katika kuashiria rukuu.




                   







           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Fiqh Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 8035


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉4 Madrasa kiganjani     👉5 kitabu cha Simulizi     👉6 Simulizi za Hadithi Audio    

Post zifazofanana:-

sadaka
Soma Zaidi...

Tofauti kati ya fiqh na sheria
Kipengele hichi tutajifunza tofauti kati ua fiqh na sheria. Soma Zaidi...

Fadhila za kufunga mwezi wa ramadhani
Soma Zaidi...

Hijjah
Nguzo za uislamu (EDK form 3:dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Miiko au Mambo yanayoharibu/kubatilisha funga
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Ufumbuzi wa tatizo la riba.
Uislamu ndio dini pekee ambayo inatoa ufumbuzi juu ya suala la riba. Soma Zaidi...

Watu wanaolazimika kufunga mwezi wa Ramadhani
Hapa utajifunza watu ambao wanalazimika kufunga mwezi wa Ramadhani. Soma Zaidi...

Fadhila za usiku waalylat al qadir
Zijuwe fadhila za usiku wenye cheo kuliko nyusiku ya miezi 1000. Soma Zaidi...

Taratibu za kutaliki katika uislamu.
Hapa utajifunza taratibu zinazofuatwa wakati wa kukusudia kumuacha mke. Pia utajifunza sababu za kiwepo kwa eda baada ya kuachwa mwanamke. Soma Zaidi...

Nini maana ya Kushahadia nguzo ya kwanza ya uislamu
Soma Zaidi...

Eda ya kufiwa na hukumu zake
Soma Zaidi...

kanunu na sheria za biashara katika islamu
Soma Zaidi...