picha

namna ya kuswali swala ya vitani

namna ya kuswali swala ya vitani

Kusimamisha Swala Vitani



Muislamu haruhusiwi kuswali swala ya faradhi nje ya wakati wake hata akiwa katika vita vya kupigania Dini ya Allah(s.w). Bali Allah (s.w) ametuhafifishia swala, tukiwa vitani na kutuelekeza tuswali ifuatavyo:


โ€œNa unapokuwa pamoja nao (Wa is lamu katika vita) ukawaswalisha, basi kundi moja miongoni mwao wasimame pamoja nawe (waswali) na washike silaha zao. Na watakapomaliza sijda zao basi na wende nyuma yenu (kulinda); na lile kundi jingine ambalo halijaswali lisw ali pamoja naw e, nao washike hadhari yao na silaha zao (humo ndani ya swala, maana) wale waliokufuru wanataka mghafilike na silaha zenu na vitu vyenu ili wakuvamieni mvamio wa mara moja. Wala si vibaya kwenu ikiwa mnaona udhia kwa sababu ya mvua au mnaona ugonjwa, kuondoa silaha zenu,.


Na mshike hadhari yenu. Hakika Mwenyezi Mungu amewaandalia makafiri adhabu itakayowadhalilishaโ€. (4:102)
Namna ya kusimamisha swala katika uwanja wa vita kutokana na maelekezo ya aya hii ni kwamba, askari wagawanyike katika makundi mawili ambayo yataswalishwa na Imamu mmoja na swala itafupishwa kama ilivyo katika swala ya safari. Kundi moja litaanza kuswali na Imamu wakiwa na silaha zao na kundi lingine litabaki katika ulinzi. Imamu ataswali rakaa moja na hili kundi la kwanza na watakaponyanyuka kuswali rakaa ya pili Imamu atabakia pale akiendelea kusoma Qur-an na kila mtu katika wale wanaomfuata, atamaliza upesi upesi rakaa ya pili na baada ya kutoa Salaam atarudi nyuma upesi kuchukua nafasi ya ulinzi. Baada ya kundi la pili kupokelewa nafasi zao, watakwenda kujiunga na Imamu ambaye bado anaendelea na rakaa yake ya pili. Wote watakapojiunga na swala, Imamu atamalizia swala yake ya rakaa mbili. Baada ya Imamu kutoa salaam kila mmoja katika wale wanaomfuata atasimama na kumalizia rakaa yake ya pili.



Aya hii ya (4:102) inayotuelekeza namna ya kuswali tukiwa katika vita vya kupigania Dini ya Allah (s.w) inafuatiwa na aya inayotoa amri ya kusimamisha swala kwa nyakati zake kama tunavyosoma:


Mwishapo kuswali kuweni mnamkumbuka Mwenyezi Mungu - msimamapo na mkaapo na (mlalapo) ubavu. Na mtakapopata amani, basi simamisheni swala (kama kawaida). Kwa hakika swala kw a Waislamu ni faradhi iliyow ekewa nyakati maalumu. (4:1 03)



Hebu fikiri: Kama askari wa Allah (s.w) aliyejitoa muhanga kwa mali yake, ahli zake na nafsi yake kwa ajili ya kupigania dini ya Allah (s.w) hakuruhusiwa kuiacha swala au kuiswali nje ya wakati wake, je wewe uliyezama kwenye shughuli nyingine ndio utegemee kusamehewa kwa kupitisha wakati wa swala ukaswali wakati unapojiona kuwa huna shughuli. Aya hii inatufahamisha kwa uwazi kuwa swala tano zimefaradhishwa kwetu pamoja na nyakati zake makhsusi.



Tukiondoa ruhusa tulizopewa kuziswali swala kidharura tunapokuwa vitani, na tukiondoa udhuru wa kusahau na kupitiwa na usingizi hapana ruhusa yoyote iliyotolewa katika Qur-an au Hadithi inayokubalika kuswali kadha kama wengi wafanyavyo. Je, mtindo huu wa kuswali kadha tunauiga kwa nani? Je, huku sio kupuuza swala? Kama tunapuuza swala kwa nini tusitarajie kupata ghadhabu za Allah (s.w) badala ya kujidanganya na kujipa matumaini ya kupata malipo mema kutoka kwake kutokana na kadha zetu hizo. Ujira wa wapuuzaji wa swala unabainishwa katika Qur-an:


Basi, adhabu itawathibitikia wanao swali. Ambao wanapuuza zao. (10 7:4-5).




                   


Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Fiqh Main: Post File: Download PDF Views 2793

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
๐Ÿ‘‰1 ai web app     ๐Ÿ‘‰2 Madrasa kiganjani     ๐Ÿ‘‰3 Dua za Mitume na Manabii     ๐Ÿ‘‰4 web hosting     ๐Ÿ‘‰5 Kitau cha Fiqh     ๐Ÿ‘‰6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    

Post zinazofanana:

Ufafanuzi kuhudu mgogoro wa mwezi ni muda gani mtu aanze kufunga.

Je inapoonekana sehemu moja tufunge duania nzima ama tufunge kwa kuangalia mwandamo katika maenro tunayoishi.

Soma Zaidi...
Ni nini maana ya uchumi katika uislamu

Katikabuislamu dhana ya uchumi imetofautiana na dhana ya kidunia hivi leo ambapo kamari na riba ni moja ya vitu muhimu katika uchumi.

Soma Zaidi...
Zijuwe aina kuu 6 za talaka katika uislamu

Talaka zimegawanyika katika makundi mengi. Katika somo hili utakwenda kukifunza aina kuu za talaka katika uislamu.

Soma Zaidi...
hukumu ya ombaomba katika uchumi wa kiislamu

Suala la omba-ombaTukiliangalia suala la omba-omba kwa upana kidogo, ambalo hivi sasa linaongelewa katika vikao mbalimbali vya kitaifa na kimataifa, tutaona kuwa ni Uislamu pekee unaotoa namna bora ya kulishughulikia suala hili.

Soma Zaidi...