picha

Nyakati za swala za dharura swala ya mgonjwa na mafiri

Nyakati za swala za dharura swala ya mgonjwa na mafiri

Swala tano za Faradh katika Nyakati za Dharura



Amri ya kusimamisha swala tano imeambatana na nyakati makhususi kama tunavyojifunza katika aya ifuatayo:


“Basi simamisheni swala Kwa hakika swala kwa waislamu ni faradhi iliyowekewa nyakati makhsusi” (4:103)
Hivyo swala ya mja haitakubaliwa iwapo ataiswali nje ya wakati wake makhsusi. Hapana “kadha” katika swala.



Pamoja na amri ya kuiswali kila swala ya faradhi katika wakati wake makhsusi, Allah (s.w) aliye Mwingi wa Rehma haikalifishi nafsi yoyote katika kuipa amri zake ila huitaraji kila nafsi itekeleze amri hizo kwa kadiri ya uwezo aliyoijaalia kuwa nao. Mara kwa mara katika kutufahamisha huruma zake juu yetu, Allah(s.w.) anakariri:



“Mwenyezi Mungu haikalifishi nafsi yoyote ila yaliyosawa na uwezo wake...” (2:286)
Baada ya kutoa ruhusa ya kutofunga wagonjwa na wasafiri, wakati wa mwezi wa Ramadhani na badala yake walipe “kadha” siku walizokula anatudhihirishia Rehma zake kwa kutufahamisha:


“... Mw enyezi Mungu anakutakieni yaliyo m epesi, w ala hakutakieni yaliyo mazito...” (2:185)
Pia baada ya kutoa ruhusa ya kutayammam, baada ya kukosa maji, au kwa ajili ya maradhi au mtu anapokuwa safarini, katika Sura ya 5 aya ya 6, Allah (s.w) anamalizia kwa kusema:-


“... Hapendi Mwenyezi Mungu kukutieni katika taabu, bali anataka kukutakaseni na kutimiza neema yake juu yenu ili mpate kushukuru”. (5:6)



“.. .Na ka m a m kiw a w agonjw a (mm eka tazw a ku tumia m aji) a u mm o safarini au mmoja wenu ametoka msalani (chooni) au mmewagusa(mmewajamii), wanawake - na msip ate maji basi ukusudieni (tayamamuni) udongo safi, mpake nyuso zenu na mikono yenu. Hakika Mw enyezi Mungu ni Mwenye kusamehe (na) Mw enye kughufiria ”. (4:43)



“... Na mkiwa wagonjwa au mmo safarini, au mmoja wenu ametoka chooni au mmeingiliana na wanawake, na hamkupata maji, basi kusudieni (tayammamuni) udongo ulio safi na kuupaka nyuso zenu na mikono yenu. Hapendi Mwenyezi Mungu kukutieni katika taabu, bali anataka kukutakaseni na kutimiza neema Yake juu yenu ili mpate kushukuru”. (5:6)



(2) Iwapo mgonjwa hajimudu na hana wa kumtwaharisha kwa maji au kwa udongo itabidi atayammamu kifikra na kuswali hivyo hivyo. Hili ni sahali kwa kauli ya Allah (s.w):


“Hapendi Allah kukutieni katika taabu, bali anataka kukutakaseni na kutimiza neema Yake juu yenu”. (5:6)



(3)Mgonjwa anaruhusiwa kuswali akiwa amekaa na kuelekea Qibla iwapo ana uwezo huo, vinginevyo ataelekea popote pale kwa kadiri ya uwezo wake. Atarukuu na kusujudu katika hali hiyo ya kukaa iwapo anaweza, vinginevyo atarukuu na kusujudu kwa ishara tu.
(4)Iwapo mgonjwa hawezi hata kukaa ataswali akiwa amelala kwa ubavu huku akiwa ameelekea Qibla kama ana uwezo wa kufanya hivyo, vinginevyo ataelekea popote pale. Pia kama hawezi kulala kwa ubavu atalala chali. Kama hawezi kulala chali ataswali kwa ishara akiwa amelala vyovyote vile awezavyo.


(5) Pia mgonjwa anaruhusiwa kuchanganya swala kama msafiri (rejea swala ya msafiri) kama hivyo ndivyo hali ya mazingira ya ugonjwa inavyotaka.
Kutokana na tahfifu hizi, ugonjwa si udhuru wa kumruhusu mtu asiswali swala ya faradh kwa wakati wake hata kama mgonjwa huyo atakuwa mahututi kitandani akiwa nyumbani au hospitalini maadamu bado ana akili timamu.




                   


Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 2018-08-01 Topic: Fiqh Main: Dini File: Download PDF Views 2280

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    👉2 web hosting    👉3 Kitabu cha Afya    👉4 Bongolite - Game zone - Play free game    👉5 Dua za Mitume na Manabii    👉6 Kitau cha Fiqh   

Post zinazofanana:

Swala ya kuomba mvua swalat istiqaa na jinsi ya kuiswali.

Hapa nitakujulisha kuhusu swala ya kuomba mvia, na taratibu za kuiswali.

Soma Zaidi...
MALI ZISIZORUHUSIWA KUTOLEWA ZAKA

*Suala la kumilikiwa binaadam (utumwa), japokuwa linaendelea kutajwa kwenye Sharia (katika vitabu), ni suala ambalo haliko.

Soma Zaidi...
Maandalizi kwa ajili ya kifo

Mwanadamu anatakiwa aishi huku akikumbuka kuwa ipo siki atakufa. Hivyo basi inatupata lujiandaa mapema kwa ajili ya kifo.

Soma Zaidi...
Aina za twahara na aina za najisi

Katika post hii utakwenda kuzijuwa aina za twahara katika uislamu. Utaviona vigawanyo vya twahara kulingana na maulamaa wa Fiqh

Soma Zaidi...
Maana ya sadaqat

Nguzo za imani, maana ya sadaqat (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...