haya ndiyo mambo yanayaribu swala na yanayobatilisha swala
Mambo yanayobatilisha Swala
Mtu akiwa katika swala yuko katika hali maalum na haruhusiwi kufanya kitu kingine nje ya swala hata vile vitendo vya kawaida alivyovizoea. Hivyo ukiwa ndani ya swala ukifanya au kukitokea moja ya mambo yafuatayo, swala yako itakuwa imebatilika na itabidi uanze upya.
(a) Kutoelekea Qibla kwa kifua pasi na dharura yoyote ya kisheria. (b) Kupatikana na hadathi kubwa, ndogo au ya kati na kati.
(c) Kufikwa na najisi mwilini, nguoni au mahali pa kuswalia.
(d) Kuvukwa na nguo ukawa uchi. Wanaume wanaovaa shati fupi wajihadhari sana hapa kwani,hasa wakati wa kurukuu na kusujudu, migongo yao (viuno vyao) chini ya usawa wa kitovu (panda za makalio) huwa wazi na hivi huhesabiwa kuwa wako uchi.
(e) Kusema au kutamka makusudi lau herufi moja yenye kuleta maana nje ya maneno ya swala.Mtume (s.a.w) amesema: gHakika ya hii swala, haifai ndani yake maneno ya watu kwani swala yenyewe ni Tasbih, Takbir na kusoma Qur-an. (Muslim)
(f) Kula au kunywa japo kwa kusahau. (g) Kufanya jambo lisilowiana na swala mfululizo mara tatu. (h) Kuiacha nguzo yoyote ya swala
(i) Ukizidisha nguzo yoyote ya swala makusudi.
(j) Kumtangulia Imam au kuchelewa kwa nguzo mbili za kimatendo kwa makusudi.
(k) Kutia nia ya kuikata swala au kujishauri moyoni kuwa uikate au usiikate swala.
(l) Kuwa na shaka kuwa umetimiza au hujatimiza sharti au nguzo yoyote ya swala.
(m) Kupotewa na akili au kulala ndani ya swala.
(n) Kutoa Salaam kwa makusudi kabla ya kwisha swala.
(o) Kuswalishwa na asiyekuwa Muislamu.
(p) Kukhalifu utaratibu wa nguzo za swala, yaani kutangulia kutekeleza nguzo ya swala kabla ya kutekeleza nguzo inayostahiki kutangulia katika utaratibu wa swala.
(q) Kuleta dua ya kuomba kitu haramu au muhali.
(r) Kumshirikisha Allah (s.w) katika kuleta dua yaani kuleta dua ya kuomba kitu cha halali lakini humuombi Allah (s.w) peke yake.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉2 Kitau cha Fiqh 👉3 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉4 Dua za Mitume na Manabii 👉5 ai web app 👉6 Bongolite - Game zone - Play free game
Post zinazofanana:
Mambo Yanayobatilisha Swala Katika Uislamu
Swala ni nguzo ya pili ya Uislamu na ni ibada muhimu sana kwa Muislamu. Ili swala ikubalike mbele ya Mwenyezi Mungu, lazima itekelezwe kwa kufuata masharti na nguzo zake. Kuna mambo mbalimbali ambayo yakitokea wakati wa swala yanaweza kuibatilisha na kuifanya isikubalike. Katika makala hii tutajifunza mambo yanayobatilisha swala, sababu zake, na jinsi ya kujiepusha nayo.
Soma Zaidi...Namna ya kuswali hatuwa kwa hatuwq
Post hii itakufundisha jinsi ya kuswali hatuwa kwa hatuwa.
Soma Zaidi...Sura zinazosomwa katika Swala ya Dhuha
Swala ya Dhuha ni swala ya sunna inayosaliwa wakati wa asubuhi baada ya jua kuchomoza na kupanda angalau kiasi cha mkuki (takribani dakika 15 baada ya jua kuchomoza) mpaka kabla ya adhuhuri. Ingawa hakuna sura maalum zilizowekwa kisheria, Mtume ï·º alisoma baadhi ya sura zenye maana ya kuhimiza kheri na shukrani.
Soma Zaidi...