picha

Mifumo ya benki na kazi zake

Hapa utajifunza kazi za benki.

7. Mfumo wa benki
Mabenki ni taasisi za fedha ambazo ni muhimu sana katika uchumi. Benki husaidia uchumi kwa kutoa huduma kuu zifuatazo:

 


Kwanza, Benki hutoa huduma ya kuhifadhi akiba za watu na kuhifadhi mali zenye thamani kubwa kama vile dhahabu, na mfano wake.

 


Pili, kutokana na akiba inazozikusanya, benki hujikuta kila wakati ina fedha nyingi zisizo na shughuli yoyote. Benki hukopesha fedha hizi kwa watu wanaozihitajia ili ziwe mtaji wa kuendeleza biashara, viwanda, kilimo na sekta nyingine mbali mbali za uchumi na utoaji huduma.

 


Tatu, benki hutoa huduma ya kurahisisha malipo kwa njia ya hundi (cheque) kuwalipa Wafanyakazi kupitia benki zao au kwa hundi, huwaepusha walipaji na hatari ya ku ib iwa.

 


Nne, pia benki hutoa huduma ya kutoa malipo ya mbali popote pale penye matawi yake nchini au ulimwenguni. Huduma hii ni muhimu sana kwani huwapunguzia watu mzigo wa kusafiri na fedha nyingi mkononi.

 


Badala yake benki huidhinisha malipo kwa simu au kwa njia yoyote ya mawasiliano ya haraka katika tawi la Benki hiyo popote lilipo nchini au ulimwenguni kupitia kwenye Account ya huyo anayestahiki kulipwa.

 


Huduma hizi muhimu na nyinginezo nyingi ambazo hatukuzitaja hapa zinatudhihirishia umuhimu wa kuwepo taasisi hii ya fedha katika jamii. Hivyo ni dhahiri kwamba Uislamu ukiwa ni mfumo kamili wa maisha unaojitegemea kwa kila kitu, hautarajiwi ukapinga au ukaharamisha kuwepo kwa mabenki katika jam ii.Bali Uislamu u n ah aram is ha m ab en ki yanayoendeshwa kwa kipato cha riba.

 

Mabenki ya Riba
Mabenki ya kitwaghuti (yasiyokuwa ya Kiislamu) sehemu kubwa ya kipato chake hutokana na riba.
Mabenki ya Riba hukopesha watu wenye miradi mbali mbali ya uchumi na kuwatoza riba kubwa katika mfumo wa malimbikizo (compound interest). Sehemu ndogo ya riba inayokusanywa na Benki za Riba, hutumiwa katika kuwalipa wateja walioweka akiba zao ambao ndio hasa matajiri walioifanya Benki iwepo.

 


Ni kutokana na unyonyaji wa namna hii utakuta, wakati wakulima na Wafanyakazi wa ngazi za chini ambao ndio wanaovuja jasho ili kuchangia riba, hawajimudu katika kujipatia chakula, mavazi, na makazi bora, wenye mabenki wanagawa “bonus ” kwa wafanya kazi wao na wao wenyewe wanaponda starehe na anasa zilizopindukia kutokana na riba ambayo hawakuitoleo jasho lolote.

 

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Fiqh Main: Post File: Download PDF Views 1714

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 ai web app     👉2 Simulizi za Hadithi Audio     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Madrasa kiganjani     👉5 Dua za Mitume na Manabii     👉6 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    

Post zinazofanana:

Je manii ni twahara au najisi?

Post hii itakwenda kukufundisha hukumu ya manii kuwa ni twahara ama ni najis

Soma Zaidi...
Ni ipi hukumu ya muislamu anayekula mwezi wa Ramadhani bila ya sababu ya kisheria

Endapo muislamu hatafunga mwezi wa Ramadhani bila ya ruhusa je atatakiwa afanye nini. Je ataweza kuilipa funga hiyo?

Soma Zaidi...
Hili ndio lengo la kufunga.

Ni kwa nini Allah ametutaka tugunge. Je kuna lengo gani hasa katika kufunga.

Soma Zaidi...
Jinsi ya kumuandaa maiti baada ya kufa

Haya ni maandalizi ya kumuandaa maiti baada ya kufariki.

Soma Zaidi...