Mtume (s.
Mtume (s.a.w) ametuagiza katika Hadith maarufu kuwa tuswali kama alivyokuwa akiswali. Hivyo katika sehemu hii tutajitahidi kuonesha utekelezaji wa swala hatua kwa hatua kwa kurejea Hadith Sahihi za Mtume (s.a.w):
1. Nia na Takbira ya kuhirimia
Nia ni kudhamiria moyoni kuwa unaswali, swala unayoikusudia kisha unaanza swala kwa kusema: âAllaahu Akbarâ Allah ni Mkubwa kwa kila haliâ. Wakati wa kuhirimia swala ni sunnah kuinua viganja vya mikono,mkabala na mabega. Kuhusu unyanyuaji wa mikono mkabala na mabega imeripotiwa kuwa Mtume (s.a.w) alikuwa akifanya hivyo katika sehemu nne tofauti:
1. Wakati wa kuhirimia swala (kuanza swala).
2. Wakati anaposema Allaahu Akbar kwa ajili ya rukui.
3. Wakati anaposimama kutoka kwenye rukuu.
4. Wakati anaposimama kutoka kwenye tahiyyatu ya kwanza ili kuendelea na rakaa ya tatu.
Hii tunaipata katika Hadith aliyosimulia Abdullah bin âUmar kuwa: âMtume (s.a.w) aliposimama kwa ajili ya swala alinyanyua mikono yake mkabala na mabega yake na kisha kuhirimia (kusema Allahu Akbar). Alipotaka kurukuu alinyanyua mikono kama alivyofanya kwanza na aliposimama kwa ajili ya itidali alifanya hivyo hivyo na alisema Allah anamsikia yule anayemsifu. (Bukhari, Muslim na Bayhaqi). Nafaâa(r.a) ameeleza kwamba Ibn âUmar (Abdullah)(r.a) aliposimama kwa ajili ya rakaa ya tatu alikuwa akinyanyua mikono; jambo ambalo alilihusisha na Mtume (s.a.w). (Bukhari, Abu Dawud, Nasai).
Baada ya kuhirimia swala mwenye kuswali hushusha mikono yake na kuiweka kifuani, mkono wa kulia ukiwa juu ya mkono wa kushoto kwa mujibu wa Hadith zifuatazo: Hulab At-Tai(r.a) amesimulia: âNilimuona Mtume (s.a.w) akiswali hali ameweka mkono wake wa kulia juu ya mkono wa kushoto juu ya kifua chake.â (Ahmad na At-Tirmidh)
Naye Wail bin Hijr (r.a) ameripoti: âNiliswali pamoja na Mtume (s.a.w) na aliweka mkono wake wa kulia juu ya mkono wa kushoto juu ya kifua chakeâ. (Ahmad na At-Tirmidh).
Imamu Abu Dawud na Nasai wamepokea kutoka kwa Ibn Khuzaimah kuwa Mtume (s.a.w) alipokuwa akiswali alikuwa akiweka mkono wake wa kulia juu ya kiwiko (wrist) cha mkono wa kushoto na sehemu ya mkono inayofuatia kiganja
2.Kusoma Dua ya Kufungulia Swala
Kusoma dua ya kufungulia swala ni sunnah. Katika Hadithi ya Bukhari na Muslim iliyosimuliwa na Abu Hurairah (r.a), baada ya kuhirimia swala Mtume (s.a.w) alikuwa akileta dua ifuatayo: âwajahtu wajhi lilladhi fatwaras-samaawat wal-ardha hanifam-muslima wamaa ana minal-mushrikina. Inna swalatiy wanusukii, wamah-haya, wamaamatiy, lillahi rabil-alamiina laa sharikalahu wabidhalika umirtu wa-ana minal-muslimiina.ââNimeuelekeza uso wangu kwa yule aliyeziumba mbingu na ardhi. Nimeacha dini za upotovu. Mimi si miongoni mwa washirikina. Hakika swala yangu (na ibada zangu zote) na uzima wangu na kufa kwangu (yote) ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, bwana (Rabbi) wa walimwengu wote. Hana mshirika wake. Na haya ndio niliyoamrishwa na mimi ni wa kwanza walio jisalimisha kikamilifu kwa Mwenyezi Mungu. (6:79, 162-163)
3. Kupiga Audhu Billah Kabla ya kuanza kusoma Qur-an ni amri ya Allah (s.w) kujikinga na sheitwani kama inavyodhihirika katika aya ifuatayo: 109 âNa ukitaka kusoma Qur-an piga Audhu billah (jikinge) kwa Allah (akulinde) na Sheitwani aliyefukuzwa (kwenye Rehema). (16:98) Hivyo tuanze kusoma Qur-an kwa kusema âAâudhu-billahi minash-shaytwanir- Rajiimâ Najikinga kwa Allah na sheitwan aliyefukuzwa-kwenye Rehma yako
4. Kusoma Suratul-Fatiha Kusoma Suratul-Fatihah ni nguzo ya tatu ya swala na ndio nguzo kubwa ya swala. Tunasoma suratul-Fatiha kama ifuatavyo:- Bismillahir Rahmaanir Rahiim (1) Alhamdu liLLahi rabbil-âAalamiin (2). Rrahmaanir Rahiim (3) Maaliki yaumiddiin (4) Iyyaakana âabudu waiyyaaka nastaâiin (5) Ih dinasw-swiraatwal mustaqiim (6) Swiraatwa lladhiina an âamta âalaihim; ghairil maghdhuubi âalaihim wala dhw-dhwaaliin (7)
Tafsri:
(1) Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema na mwenye kurehemu: (2) Shukrani zote anastahiki Mwenyezi Mungu, Mola wa Walimwengu wote: (3) Mwingi wa Rehema mwenye kurehemu (4) Mwenye kumiliki siku ya malipo: (5) Wewe tu ndiye tunayekuabudu, na wewe tu ndiye tunaye kuomba msaada: (6) Tuongoze njia iliyonyooka: (7) Njia ya wale uliowaneemesha; siyo (ya wale ) waliokasirikiwa, wala ya wale waliopotea
5. Kusoma Qur-an baada ya Suratul-Fatiha Katika rakaa ya kwanza na ya pili ni Sunnah baada ya kusoma Suratul-Fatiha kuleta Surah au aya nyingine za Qur-an
6.Kurukuu
Baada ya kusoma Suratul-Fatiha na Surah nyingine, au baadhi ya aya katika sura nyingine unasema Allahu-akbar kisha unarukuu (kuinama). Rukuu ni nguzo ya swala pamoja na kujituliza humo. Katika rukuu ni sunnah kumsabihi Allah (s.w) kwa kusema kimya kimya mara tatu au zaidi âSubhana RabbiyalâAdhiimâ âUtukufu ni wako Ee Bwana (Mlezi) wangu Uliye mkuuâ
7.Kuitidal
Kuitidali ni kusimama wima kutoka kwenye rukuu, ni sunnah kusema wakati wa kunyanyuka maneno haya:âsamiâa llahu liman hamidahuâ Mwenyezi Mungu anamsikia kila mwenye kumhimidi. Na baada ya kusimama sawa ni sunnah kusema ârabbanaa walakal-hamduâewe mola wetu sifa zote za ukamilifu ni zako. Pia ni sunnah kusema maneno haya ârabbanaa walakal-hamdu mil-as-samaawati wamil-al-ardhi wamil-amashi-ita minshai-in baâadahâ Ewe Mola wetu sifa zote za ukamilifu ni za kwako, kutoka mbinguni, kutoka ardhini na katika vitu vyote vilivyo baina yao (mbingu na ardhi) na kutoka katika vinginevyo unavyo viridhia
8.Kusujudi
Ni nguzo pamoja na kujituliza katika sujudi. Mkusujudi ni kuvituliza chini viungo saba kwa utaratibu wa swala. Vingo hivyo ni , paji a uso, viganya viwili vya mikono, magoti mawili na matumbo ya nyayo za vidole vya miguuni.viungo vyote hivi vinatakiwa vielekee kibla. Paji la uso ni pamoja na pua iguse chini.utasema kwenye sijda âsubhaana rabbiyal-aâalaaâ utukufu ni wa kwako Mola uliye tukuka.
9.kukaa baina ya sijda mbili
Hiki ni kitako kinachopatikana baada ya kutoka kusujudi. Sifa ya kikao hiki ni kukalia unyayo wa mguu wa kushoto na kuweka mikono miwili juu ya mapaja. Ni sunnah kusema maneno haya: ârabbigh-firliy warhamnii waâafinii warzuqniyâEwe Mola wangu nisamehe, na unirehemu, na unipe afya na uniruzuku
10.kikaa tahiyyatu
Katika kukaa Thiyyatu mtume alikuwa akikalia futi la mguu wa kushoto na kusimamisha futi la mguu wa kulia na katika tahiyyatu ya mwisho alikaa chini na kuulaza mguu wa kushoto katika uvungu wa mguu wa kulia na alisimamisha futi la mguu wa kulia, katika vikao vyote hivyo viwili,
Mtume (s.a.w) alivilaza viganja vyake juu ya mapaja karibu na magoti kama tunavyoelezwa katika hadith ifuatayo: Abdullah bin Jubair(r.a) ameeleza kuwa wakati Mtume (s.a.w) alipokaa tahiyyatu, alikuwa akiweka kiganja chake cha mkono wa kulia juu ya paja lake la kulia na kiganja cha mkono wa kushoto juu ya paja la mguu wa kushoto na alikuwa akinyoosha kidole chake cha shahada (wakati wa k u s e m a , â A s h - h a d u anllaaillaha illallah) na kukiegemeza juu ya kidole gumba na alikuwa akiweka kiganja chake cha mkono wa kushoto juu ya goti lake (la mguu wa kushoto). (Muslim).
11.Kusoma Tahiyyatu
Kusoma tahiyyatu ni nguzo ya swala. âTahiyyatuâ ina maana ya âMaamkiziâ, ukiwa umekaa kikao cha tahiyyatu unaleta maamkizi kama ifuatavyo: âAttahiyyaatu lillaah, wasw-swalawaatu, watwa-yyibaatu, assalaamu âalaika ayyuhannabiyyu, warahmatullaahi wabarakaatuhu, assalaamu âalay-naa wa-âalaa âibaadillaahi swswaalihiina. Ash-hadu an-llaailaaha illallaahu wa-ash-hadu anna Muhammadan âabduhuu warasuuluhuâ. âMaamkizi yote ni ya Allah, na swala zote na yote mazuri, Amani iwe juu yako, ewe Mtume na Rehma na Baraka za Allah. Na amani iwe juu yetu na juu ya waja wema wa Allah. Ninashuhudia kuwa hapana Mola ila Allah. Na ninashuhudia kuwa Muhammad ni Mja na, ni Mtume wakeâ. (Muslim).
12. Kumswalia Mtume (s.a.w).
Kumswalia Mtume (s.a.w) ni nguzo ya swala inayofuatia baada ya kusoma Tahiyyatu. Kumswalia Mtume si faradhi katika swala tu bali pia ni faradhi kumswalia kila anapotajwa kwa jina lake. Msisitizo wa amri ya kumswalia Mtume unaonekana katika aya ifuatayo:
âHakika Mwenyezi Mungu anamteremshia Rehema Mtume; na Malaika wake (wanamuombea dua). Basi; enyi Mlioamini msalieni (Mtume, muombeeni Rehema) na amaniâ. (33:56)
Pia hadithi zifuatazo zinasisitiza umuhimu wa kumswalia Mtume (s.a.w) kila atajwapo na kila mtu apatapo wasaa. Ali (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: Bakhili ni yule anayesikia nikitajwa, lakini haniswalii. (hanitakii rehma). (Tirmidh).
Abu Hurairah amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: âAnayenitakia Rehma (anayeniswalia) mara moja, Allah humrehemu mara kumiâ. (Muslim).
âIbn Masâud amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: Atakayekuwa kipenzi changu katika watu, katika siku ya Kiama atakuwa ni yule aliye mbele kuliko wote katika kunitakia Rehma (kuniswalia). (Tirmidh).
Namna ya kumswalia Mtume (s.a.w) imeelezwa katika Hadithi nyingi lakini iliyomashuhuri katika hizo ni ile iliyosimuliwa na Abdur- Rahman bin Ubaidillah(r.a) na kupokelewa na Maimamu wote wa Hadithi kuwa Mtume (s,.a.w) ametufundisha tumswalie (tumtakie Rehma) kama ifuatavyo;
âAllahumma swalli âalaa muhammad waâalaa aliy Muhammad kamaa swallaita âalaa ibraahima waâalaa ali ibraahim innaka hamiidum-majid. Wabaaik âalaa muhammad waâalaa ali muhammad kamaa barakta âalaa ibraahima waâalaa ali ibraahima innaka hamiidum-majidâ
Ewe Mola mrehemu Muhammad na wafuasi wake kama ulivyomrehemu Ibrahim na wafuasi wake hakika wewe ni mtukufu na msifiwa wa haki. Ewe Mola mbariki Muhammad na wafuasi wake kama ulivyombariki Ibraahim na wafuasi wake hakika wewe ni wewe ni mtukufu na msifiwa wa haki.
12.Dua kabla ya salamu
Ni sunnah kuleta dua kabla ya salamu. Dua hizi ni nyingi ila miongoni mwanzo ni
Dua aliyotufundisha Mtume (s.a.w) kwa msisitizo mkubwa kama tunavyofahamishwa katika Hadithi ya Muslim, iliyosimuliwa na Ibn Abbas, ni hii ifuatayo: Allahumma Inni-audhubika min-âadhaabi-lqabri,Wa-auudhubika min fitnatil masiihi-ddajjaal, Wa-auudhubika min fitnatil-mahyaa wal-mamaati, âEe Allah najikinga kwako kutokana na adhabu ya kabr, na najikinga kwako kutokana na fitina za masiihi Ddajjaal na najikinga kwako kutokana na matatizo ya maisha na mauti.
Sijidat-Sah-wi (Sijda ya kusahau)
Sijdat Sah-wi ni sijidah anayoileta mtu kabla ya kutoa salaam ili kufidia kitendo cha sunnah alicho kisahau kwa mfano kusahau kukaa tahiyaatu ya kwanza.Vile vile mtu akisahau au akikosea jambo lolote ambalo halibatilishi swala kwa mfano akaswali rakaa tano badala ya rakaa nne kwa swala ya Adhuhuri. Kabla hajamaliza swala alete sijidat Sahau. Hivi ndivyo tunavyojifunza kutokana na Hadithi zifuatazo: Abdullah bin Masâud (r.a) amesimulia: Mtume wa Allah alituswalisha Adhuhuri rakaa tano.Tukamuuliza kama pameamrishwa na Mwenyezi Mungu kurefushwa swala akajibu, La! Tukamuambia: âUmetuswalisha rakaa tano. Akasema (Mtume): Mimi ni binaadamu kama nyinyi, nakumbuka kama mnavyokumbuka na nasahau kama mnavyosahau. Kisha akasujudu sijdah mbili zikawa ni fidia kwa kusahau. (Bukhari na Muslim).
Muhimu:
Kumbuka kuwa sijda hii Mtume (s.a.w) aliileta baada ya kutoa salaamu na baada ya kukumbushwa. Abdullah bin Buhaymah (r.a) amesimulia kuwa Mtume (s.a.w) aliswalisha swala ya adhuhuri, akasimama baada ya rakaa mbili, alipomaliza swala akasujudu mara mbili huku akisema: âAllah Akbarâ katika kusujudu na katika kuinuka, wakati amekaa kabla ya kutoa salaam, na watu wakasujudu pamoja naye. Hii ilikuwa ni kufidia ile tahiyyatu ya mwanzo aliyoisahauâ. (Muslim)
14. kutoa salamu.
Kutoa salamu ni nguzo katika nguzo za swala. Ukamilifu wa kutoa salamu ni kusema âas-salaamu alykum warahmatullahi wabarakaatuhâ salamu zipo mbili yakwanza utatoa upande wa kulia na ya pili utatoa upande wakushoto. Sifa ya kugeuka kwa kutoa salamu ni kuwa utageuka mpaka mashavu yawze kuonekana kwa mtu aliye nyuma.
Lugha ya Swala Lugha ya swala,
kuanzia kwenye Takbira ya kuhirimia Swala mpaka kumalizia swala kwa Salaam, ni Kiarabu. Hekima yake iko wazi. Kiarabu ndio lugha ya Qur-an tukufu na kwa hiyo ndio lugha rasmi ya Kiislamu inayowaunganisha Waislamu wote ulimwenguni. Waislamu ni umma mmoja tu na Waislamu wote ni ndugu moja wasio baguana kwa lugha, rangi, taifa wala ubaguzi mwingine wa aina yoyote ile.Muislamu yeyote anaweza kuwa Imamu mahali popote ilimradi tu awe anatekeleza masharti ya Uimamu. Muislamu hana msikiti maalum. Misikiti yote ni yake na anaweza kuswali kwenye msikiti wowote ulimwenguni bila ya kupata tatizo lolote la lugha. Kwa sababu hii kila Muislamu inabidi ajifunze kiasi cha uwezo wake kutamka, kwa Kiarabu yale yote tuyasemayo katika swala..
Dua na Dhikri Baada ya Swala
Ni vizuri mara Muislamu anapomaliza kuswali kama hana dharura yoyote asiondoke bila ya kuleta Dhikri na dua kama alivyofundisha Mtume (s.a.w), kwani zina umuhimu mno katika kumsaidia mja kufikia lengo la swala na lengo la kuumbwa kwake kwa ujumla iwapo atayafahamu na kuyazingatia yale anayoyatamka. Kutokana na Hadithi iliyosimuliwa na Samura bin Jandab(r.a) na kupokelewa na Bukhari(r.a), baada ya swala Mtume (s.a.w) aliwageukia Waislamu aliokuwa akiwaswalisha. Kisha aliomba maghfira (msamaha) mara tatu na kuongezea maneno yaliyoelezwa katika Hadithi zifuatazo: Thawban (r.a) amesimulia kuwa Mtume (s.a.w) alipomaliza swala aliomba maghfira (msamaha) mara tatu kwa kusema: Astagh-firullah (Mara tatu) Ninaomba msamaha kwa Allahh na kusema âAllahumma Antassalam waminkas-salaam Tabaarakta YaaDhal jallaali Wal-ikraam.â Ewe Allah, wewe ni Amani, na kwako ndiko iliko Amani. Wewe ndiye Mbariki Ewe Mwenye Utukufu na Heshima (Muslim)
Baada ya nyiradi hizi, ni vizuri pia kuomba dua yoyote kulingana na haja zako kwa lugha yoyote. Jambo hili la kuomba dua baada ya swala, umuhimu wake unadhihirika katika hadithi ifuatayo: Abu Umamah amesimulia kuwa: Iliulizwa: Ee Mtume wa Allah. ni dua gani ambayo hukubaliwa zaidi?h (Mtume) alijibu: (moja) ni ile ya katikati ya nusu ya pili ya usiku na (pili) kila baada ya swala ya faradhi. (Tirmidh)
Hivyo ni jambo la msingi mno kuomba dua yoyote kila baada ya swala na dua zilizo nzito zaidi ni zile zilizomo kwenye Qur-an na hadithi za Mtume (s.a.w). Kwa mfano ni vizuri kila baada ya swala, au baada ya dhikri zilizotajwa tuombe dua ifuatayo: Rabii ijâalnii muqiimas-swalaati wamindhurriyyatii Rabbana Wataqabbal duâaaai. Mola wangu! Nijaalie niwe msimamishaji swala, na kizazi changu! (Pia kiwe hivi). Mola wetu! Na upokee maombi yangu mengine... (14:40-41).
Umeionaje Makala hii.. ?
Haki na uadilifu katika uislamu (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukufundisha sunnah 9 za swala. Sunnah hizi ni zile ambazo ukiziwacha swala yako haibatiliki.
Soma Zaidi...Nguzo za uislamu (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Sharti za SwalaSharti za Swala Sharti za swala ni yale mambo ya lazima anayotakiwa Muislamu ayachunge na kuyatekeleza kabla hajaanza kuswali.
Soma Zaidi...Posti hii inakwenda kukufundisha kuhush swala za sunnah.
Soma Zaidi...Hapa utajifunza taratibu zinazofuatwa wakati wa kukusudia kumuacha mke. Pia utajifunza sababu za kiwepo kwa eda baada ya kuachwa mwanamke.
Soma Zaidi...Je jamii inachukuliaje swala la kuoa mke zaidi ya mmoja.
Soma Zaidi...