Sunnah za Swala
Vipengele vya sunnah katika swala ni vile ambavyo mwenye kuswali akivitenda husaidia sana kukuza daraja ya swala yake na kuipa nguvu na msukumo mkubwa wa kuiwezesha kufikia lengo lililokusudiwa kwa urahisi zaidi. Ama mwenye kuswali akiacha kipengele chochote katika vipengele vya sunnah, swala yake itakamilika iwapo atatekeleza vipengele vyote vya nguzo. Katika Hadith tumeona kuwa Mtume (s.a.w) katika swala yake pana vipengele vya ziada ya nguzo kama ifuatavyo:
1.Kuinua viganja vya mikono mkabala na mabega, usawa wa vigingi vya masikio wakati wa kuhirimia swala, kwenda kwenye rukuu, baada ya rukuu na baada ya kutoka kwenye Tahiyyatu ya kwanza.
2.Kusoma dua baada ya takbira ya kuhirimia.
3.Kuanza na a ’udhubillaah (kumlaani Shetani) kabla ya kuanza kusoma suratul-Fatiha.
4.Kuitikia “Aamin”baada ya kumaliza Suratul Fatiha.
5.Kusoma aya za Qur-an baada ya Suratul-Fatiha katika rakaa mbili za mwanzo.
6.Kuleta Tasbih, Tahmid na dua katika rukuu, itidali na s ijda.
7.Kutoa takbira katika kubadilisha kitendo kimoja kuendea kingine isipokuwa tu kutoka kwenye rukuu kwenda kwenye itidali ndipo tunaposema: “Sami’Allahu liman hamidah - Rabbanaa lakal-hamdu”.
8.Kukaa na kusoma Tahiyyatu kila baada ya rakaa mbili, kwa swala zenye rakaa zaidi ya mbili.
9.Kusoma dua baada ya kumswalia Mtume na kabla ya kutoa S a la am.
Umeionaje Makala hii.. ?
Katika post hii utakwenda kujifunza jinsi ya kutawadha kama vile ambavyo alitawadha Mtume
Soma Zaidi...Mambo ya faradh kwa maiti ya muislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Kwenye kipengele hiki tutajifunza maana ya swala ni nin?. Na masharti ya swala.
Soma Zaidi...Uchumi wa uislamu umeweka taratibu mbalimbali katika kuchuma mali.
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukufundisha maana ya kusimamisha swala kama inavyotumika kisheria.
Soma Zaidi...Ugawaji wa mirathi-Mume ana nusu (1/2) = 1/2 -Mama ana sudusi.
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukufunza kuhusu swala ya dhuha, faida zake wakati wa kuiswali swala ya dhuha na jinsi ya kuiswali.
Soma Zaidi...