11. Swala ya Kupatwa kwa Jua na MweziSwala ya kupatwa kwa mwezi au jua ni sunnah iliyokokotezwa ambayo huswaliwa katika jamaa. Jua au mwezi unapopatwa Waislamu wanatakiwa waitane na kuswali swala ya Suunah ya kupatwa jua au mwezi kama alivyokuwa akifanya Mtume wa Allah:Aisha (r.a) ameeleza kuwa jua lilitokea kupatwa wakati wa Mtume (s.a.w). Alisimama kuswali na alirefusha kisimamo (kiasi cha kumaliza kusoma Suratul-Baqara). Kisha alirukuu na kurefusha sana rukuu yake. Kisha aliinuka kutoka kwenye rukuu na akarefusha kisimamo lakini kilipungua kidogo kuliko kile cha kwanza. Kisha alirukuu tena na kurefusha rukuu lakini kupungua kidogo kuliko ile rukuu ya kw anza. Kisha alisujudu na kisha akasimama tena lakini kwa kitambo kilichopungua kidogo kuliko kisimamo kilichotangulia. Kisha alirukuu tena kw a kitam bo kilichopungua kidogo kuliko kile cha rukuu iliyotangulia. Kisha aliinuka kutoka kw enye rukuu na kurefusha kisimamo lakini kupungua kidogo kisimamo kilichotangulia. Kisha alirukuu tena na kurefusha rukuu yake lakini kupungua kidogo kuliko ile iliyotangulia. Kisha alis ujudu. Kisha ligeuka (aligeukia watu) na wakati huo jua lilikwisha kuwa jeupe na akawahutubia watu. Alimshukuru (alimhimidi) Allah na akasema: Jua na mwezi ni alama mbili za Allah (s.w). Havipatwi kutokana na kifo cha mtu yeyote, wala kutokana na kuzaliwa kwa mtu yeyote. Enyi Ummah wa Muhammad, hapana yeyote mwenye kupata ghadhabu kuliko Allah anavyomghadhibikia mja wake pindi anapozini. Enyi watu wa Muhammad, naapa kwa Allah kuwa kama mngelikuwa mnajua, mngelicheka kidogo na kulia sana ”. (Muslim)Kutokana na Hadithi hii tunaona kuwa swala ya kupatwa jua na mwezi ina visimamo (au visomo) vinne, rukuu nne na sijda nne. Visimamo na rukuu hutofautiana urefu kama ilivyo oneshwa katika Hadithi.Imamu Shafii na Maimamu wengine wanashikilia kuwa swala ya kupatwa jua na mwezi haina budi kuswaliwa katika muundo huu ulioelezwa katika hadithi hii. Lakini Imamu Abu Daud, anashikilia kuwa swala ya kupatwa kwa jua na mwezi iswaliwe kama swala ya kawaida kwani kutokana na hadithi hiyo Mtume (s.a.w) aliwahi pia kuswali swala hiyo kwa kufuatia muundo wa swala za kawaida.


Kwa ujumla wanachuoni wengi wanasisisitiza kuwa pamoja na kwamba swala ya kupatwa kwa jua na mwezi inaweza kuswaliwa kwa kufuata muundo wa kawaida wa swala, ni vizuri zaidi kama swala hiyo itaswaliwa kwa kufuata muundo ulioelezwa katika Hadithi hii wa kuwa na visimamo (visomo) vinne, rukuu nne na sijda nne.Lengo la swala hii ni kumkumbuka Allah(s.w) kwa kuzingatia alama zake. Hivyo ni vyema Imamu baada ya swala awawaidhi Waislamu kuwakumbusha wajibu wao kwa Allah(s.w) na kuwakumbusha marejeo yao ya akhera. Hivyo swala ya kupatwa jua (Swalatul-Kusuf) au swala ya kupatwa mwezi (swalatul-Khusuf) hufuatiwa na khutuba mbili kama ilivyo katika khutuba ya Idd. Katika swala hizi Imamu atasoma kwa sauti.