Zakatul-Fitri
Zakatul-Fitri ni zakat inayomlazimu kila Muislamu mwanamume na mwanamke,mdogo na mkubwa, ambayo hutolewa baada ya funga ya Ramadhani kabla ya kuswali swala ya Iddil-Fitri. Watoto, wanawake, wazee, na wengine wasio na uwezo wa kulipa zakatul-fitr watalipiwa na mawalii wao. Kwa mfano mume atamtolea mkewe na watoto ambao hawajaweza kujitegemea; pia atawatolea wazazi wake kama hawana uwezo wa kujilipia; vile vile baba atalazimika kuwalipia Zakatul-fitr wale wote wengine ambao ni Waislamu walio chini ya uangalizi wake. Mtoto mchanga aliyezaliwa dakika chache kabla ya kuandama mwezi wa Shawwal atatolewa Zakatul-Fitri.
Umuhimu wa Zakatul Fitri
Zakatul Fitri ni faradhi iliyoambatanishwa na faradhi ya funga ya Ramadhani. Mtume (s.a.w) ameamrisha Zakatul-Fitri kutolewa na kila Muislamu mwanamume na kila Muislamu mwanamke na amebainisha wazi kuwa Swaumu ya mja haipokelewi endapo hajajitolea Zakatul Fitri na kuwatolea wote wale walio chini ya uangalizi wake. Msisitizo wa utoaji Zakatul-Fitr tunaupata katika Hadith ifuatayo:
Ibn Umar (r.a) amesema kuwa Mtume wa Allah ameamrisha ulipaji wa Zakatul-fitr baada ya Ramadhan kwa kila Muislamu muungwana na mtumwa, mume na mke, (Mkubwa na mdogo) kwa (kila mtu) kutoa sai moja ya tende zilizokaushwa au sai moja ya shairi (Barley).(Bukhari na Muslim).
Nisaab ya Zakatul-Fitri
Zakatul Fitri inamlazimu yeyote yule mwenye kupata chakula cha kumtosha yeye mwenyewe na wale walio chini ya uangalizi wake kwa siku ya Idd na Usiku wake na akawa na ziada. Ziada hiyo ataitoa zakatul fitri kwa viwango vinavyostahiki.
Kiwango cha Zakatul-Fitri
Kwa mujibu wa hadithi ya Ibn Umar (r.a) kiwango cha Zakatul-Fitri kwa kila kichwa ni Saβi moja ya chakula kinacholiwa kwa wingi katika sehemu husika. Kwa mfano chakula kinachopendelewa sana na watu wa mikoa ya pwani ya Tanzania ni mchele na kile kinachopendelewa sana na mikoa ya bara ni mahindi, uwele na mtama.
Saβi iliyotumika wakati wa Mtume (s.a.w) imelinganishwa na pishi inayotumika katika mazingira ya Tanzania. Pishi moja ya vyakula hivyo vilivyotajwa ni sawa na kilo mbili na nusu (2.5kg). Pia inajuzu kuthaminisha pishi ya chakula husika na fedha taslimu. Kihalisia ni vizuri zaidi kutoa fedha taslimu ili kumuwezesha huyo anayepewa zakatul-fitri aweze kununua chakula husika pamoja na viungo mbali mbali vitakavyo kifanya chakula hicho kiwe kizuri na cha kuvutia kwa ajili ya kusherehekea Idd.
Muda unaofaa kutolewa Zakatul-Fitri
Muda wa kutoa Zakatul fitri umebainishwa katika Hadith ifuatayo:
Ibn Umar (r.a) ameeleza kuwa Mtume (s.a.w) aliwaamuru watu kuwa walipe zakatul fitri kabla ya swala (ya Iddil-Fitri) (Muslim).
Kulipa Zakatul Fitri mapema kabla ya kuswali Idd au mapema zaidi ya hapo, kutawawezesha maskini na mafakiri kufurahia Idd pamoja na Waislamu wengine. Ikitokea sababu ya msingi, kama vile kusahau, mtu akachelewa kutoa Zakatul-fitri mpaka Idd ikaswaliwa, hana budi kuitoa baada ya swala. Lakini jambo la kuzingatia ni kwamba, amri ya kutoa Zakatul-fitri kabla ya swala imetolewa na Mtume (s.a.w), hivyo, mtu akiivunja amri hii makusudi au kwa uzembe ajue kuwa kutoa kwake huko hakutamnufaisha chochote.
Watu wanaostahiki kupewa Zakatul-Fitri
Zakatul-Fitri si malipo ya maimamu wa Tarawehe kama wengi wanavyoichukulia bali ni chakula cha maskini na wale wote wasiojiweza kujipatia chakula pamoja na wale walio chini ya uangalizi wao kwa siku ya Idd na usiku wake ili nao wajisikie na wafurahie Idd pamoja na Waislamu wenzao wenye uwezo. Kama ilivyo katika Zakatul-Mal, akipewa Zakatul-Fitri asiyestahiki itakuwa ni kudhulumu haki ya wale wanaostahiki na mtoaji na mpokeaji wa zakatul-fitri hiyo watakuwa ni mad ha lim u.
Ili kuhakikisha kuwa katika jamii au katika mtaa wa Waislamu kila anayestahiki kupewa zakatul fitri amepata na kuzuia uwezekano wa mtu mmoja kulundikiwa zakatul-fitri kiasi kikubwa sana, na mwingine kukosa au kupata kiasi kidogo sana kisichotosheleza mahitaji yake ya siku ya Iddi, ni vyema Waislamu wa mtaa mmoja au wa sehemu moja waikusanye Zakatul-Fitri kwa pamoja, na kisha waigawanye kwa wote wanaostahiki katika mtaa au sehemu hiyo wakizingatia mahitajio yao kulingana na majukumu ya kifamilia waliyo nayo.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 2371
Sponsored links
π1 Madrasa kiganjani
π2 kitabu cha Simulizi
π3 Simulizi za Hadithi Audio
π4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
π5 Kitabu cha Afya
π6 Kitau cha Fiqh
Kitabu Cha Dua 120
Sifanjema zinamstahikia Allah Mola wa viumbe vyote. Soma Zaidi...
Swala ya Kuomba Toba (tawbah) na namna ya kuiswali
Soma Zaidi...
MAANA YA HADITHI SUNNAH
Maana ya SunnahKilugha: Neno sunnah katika lugha ya Kiarabu lina maana ya mwenendo au mila. Soma Zaidi...
UANDISHI WA HADITHI WAKATI WA MASWAHABA
Wakati wa Masahaba wa Mtume (s. Soma Zaidi...
Presha ya kupanda (hypertension) dalili zake, na njia za kukabiliana nayo
Soma Zaidi...
Madai ya Makafiri Dhidi ya Qurβan na Udhaifu Wake
i. Soma Zaidi...
Maharimu ni wanawake na wanaume walioharamishwa kuoana
Soma Zaidi...
swala ya witri na namna ya kuiswali
3. Soma Zaidi...
DARSA ZA TAWHID
Jifunze tawhid yaani kumpwekesha Allah subhaanah wata'aala Soma Zaidi...
fadhila za sura kwenye quran
FADHILA ZA BAADHI YA SURA Umuhimu na ubora wa baadhi ya sura na aya. Soma Zaidi...
fadhila za kusoma quran
Fadhila na umuhimu wa kusoma quran 1. Soma Zaidi...