Menu



Nguzo 6 za iman ya dini ya kiislamu kwa mafundisho ya quran na sunnah

Nguzo za Imani.

Nguzo 6 za iman ya dini ya kiislamu kwa mafundisho ya quran na sunnah

Nguzo za imani ya dini ya kiislamu

Nguzo za Imani.
1.Kumuamini Mwenyezi Mungu.
2.Kuamini Malaika wake.
3.Kuamini Vitabu Vyake.
4.Kuamini Mitume Wake.
5.Kuamini siku ya Mwisho.
6.Kuamini Qadar ya Mwenyezi Mungu.



1.Kumuamini Mwenyezi Mungu (s.w).
- Imani juu ya kuwepo Mwenyezi Mungu ni jambo la kwanza kabisa kwa kila mwenye akili timamu kupitia ishara na maumbile mbali mbali yanayotuzunguka.
Rejea Qur’an (3:190).



- Baada ya kumtambua, ni kumuabudu ipasavyo na kutomshirikisha katika sifa na majina yake matukufu na kiumbe yeyote.
Rejea Qur’an (18:109), (31:27), (57:1-7), (59:22-24).
Rejea Kitabu cha 2, EDK, Shule za Sekondari; Uk.8-16.



2.Kuamini Malaika wa Mwenyezi Mungu.
- Malaika ni viumbe wa Mwenyezi Mungu walioumbwa kutokana na nuru kwa lengo la kumtumikia Mwenyezi Mungu (s.w).

- Ni viumbe wa kiroho, wasio na jinsia, wenye mabawa na wenye uwezo wa kujimithilisha na kitu (kiumbe) chochote.

- Hawana matashi ya kibinaadamu kama kula, kulala, kunywa, kuchoka, kuugua na hawana hiari kwa kila wanachoamrishwa na Mwenyezi Mungu (s.w).
Rejea Qur’an (16:49-50), (7:206) na (21:26-27).



3.Kuamini Vitabu vya Mwenyezi Mungu (s.w).
- Kuamini vitabu vya Allah (s.w) ni lazima kwa kila muumini wa kweli kama vilivyoainishwa katika Qur’an, ambavyo baadhi ni;
a)Suhufi – aliyoteremshiwa Nabii Ibrahim (a.s) na Nabii Musa (a.s).
b)Taurat – aliyoteremshiwa Nabii Musa (a.s)
c)Zaburi – aliyoteremshiwa Nabii Daud (a.s)
d)Injili – aliyoteremshiwa Nabii Isa (a.s) na
e)Qur’an – aliyoteremshiwa Nabii au Mtume Muhammad (s.a.w).



- Vitabu hivi vimeteremshwa kwa lengo la kuwaongoza wanaadamu katika njia sahihi na iliyonyooka ya maisha yao ili kufikia lengo la kuumbwa kwao.
Rejea Qur’an (57:25) na (5:46).



Sababu ya Vitabu Vilivyotangulia kutajwa ndani ya Qur’an:
1. Qur’an ndiyo Kitabu cha mwisho kilichoteremshwa kwa ajili ya kuwaongoza walimwengu wote.
2. Vimetajwa ili kuwafahamisha waislamu juu ya uwiano, usahihi na upotofu wa mafundisho hayo na yale ya Qur’an.
3. Mwenyezi Mungu (s.w) kutaka kuonyesha nafasi na utata wa vitabu hivyo kutumika zama hizi kama mwongozo wa maisha.
4. Mwenyezi Mungu (s.w) kutaka kuonyesha upungufu, mabadilisho na upotofu uliofanywa ndani ya Vitabu hivyo.
Rejea Qur’an (6:92), (2:75), (4:14), (5:15), (5:48) na (16:64).



4.Kuamini Mitume wa Mwenyezi Mungu (s.w).
- Mitume ni wanaadamu wanaume walioteliwa ili kuwaongoza na kuwa mifano bora ya kuigwa kwa watu (ummah) wao katika kutekeleza ujumbe wao.

-Idadi kamili ya mitume wote wa Mwenyezi Mungu (s.w) haijulikani, bali waliotajwa ndani ya Qur’an ni 25.
Rejea Qur’an (10:47), (6:83-86)
Rejea Kitabu cha 2, EDK, Shule za Sekondari; Uk.23.



Sifa za Mitume.
i.Ni watu walizaliwa, walioa, walikula, waliugua, walikufa, n.k. kama binaadamu wa kawaida isipokuwa Nabii Adamu (a.s).
ii.Walikuwa na kila tabia njema, wakweli, waaminifu na wenye huruma.
iii.Walikuwa na upeo wa Elimu wa hali ya juu kuliko watu wote enzi zao kwa sababu kuletewa kwao wahayi.
iv.Walikuwa Wacha-Mungu wa hali ya juu kuliko watu wote.



Kazi za Mitume.
i.Kufahamisha na kufundisha juu ya uwepo wa Mwenyezi Mungu (s.w) na sifa zake. Qur’an (21:25), (16:36).
ii.Kufahamisha mambo ya ghaibu (Akhera) kama Moto, Pepo, Kiyama, Hisabu, Maisha ya Barzaq (kaburini) n.k.
iii.Kufundisha njia sahihi ya maisha anayoiridhia Mwenyezi Mungu inayopelekea kunusurika na adhabu zake. Qur’an (3:164).
iv.Kusaidiana na wafuasi wao katika kuamrisha mema na kuondosha maovu katika jamii.
v.Kuonya kutokana na adhabu na kubashiria mema kwa wafanyao mema.


5.Kuamini Siku ya Mwisho.
- Ni kuwa na yakini moyoni kuwa kuna maisha mengine baada ya kufa.
?Hatua za maisha baada ya kufa:
a)Kutokwa na roho.
b)Maisha ya kaburini (Barzaq).
c)Kufufuliwa.
d)Kuhesabiwa (Hisabu).
e)Kuishi Peponi au Motoni milele
- Kwa mujibu wa amali zao (vitendo vyao).



6.Kuamini Qadar ya Mwenyezi Mungu (s.w).
-Ni kuwa na yakini moyoni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w) anao mpango wa viumbe vyake vyote alioweka kabla ya kuumba chochote.

- Amekiumba kila kiumbe kwa lengo maalumu na kukikadiria mahitaji yake yote.
Rejea Qur’an (11:6), (57:22), (54:49) na (25:2).



                   

Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass

Nyuma Endelea


Je umeipenda post hii ?

Ndio            Hapana            Save post
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Main: Dini File: Download PDF Views 6144

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya    👉2 kitabu cha Simulizi    👉3 Madrasa kiganjani    👉4 Kitau cha Fiqh    👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉6 Simulizi za Hadithi Audio   

Post zinazofanana:

fadhila za sura kwenye quran

FADHILA ZA BAADHI YA SURA Umuhimu na ubora wa baadhi ya sura na aya.

Soma Zaidi...
NDANI YA SHIMO LA KABURI

Download kitabu Hiki Bofya hapa NDANI YA PANGO LA MAKABURI Mmoja wapo akatowa kamba na kulifunga jeneza vizuri na kuanza kulishusha chini ya mapango kwa kamba ile.

Soma Zaidi...
Ujumbe wa Qur-an Utawafikiaje Wale wasio Waarabu au wale Wasiojua Kiarabu?

Ujumbe wa Qur-an Utawafikiaje Wale wasio Waarabu au wale Wasiojua Kiarabu?

Soma Zaidi...
Maandalizi ya kujiandaa mwenyewe kabla ya kufa ama kufikwa na mauti (kifo)

Kwakuwa kila mtu anatambua kuwa ipo siku atakufa hivyo ni vyema kuanza kujiandaa mapema.

Soma Zaidi...
UANDISHI WA HADITHI WAKATI WA TABI'INA

Wakati wa Wafuasi wa masahaba (Tabi'ina)101-200 A.

Soma Zaidi...