a) Uthibitisho Kutokana na Qur’an Yenyewe
i. Kutojua kusoma na kuandika kwa Mtume Muhammad (s.a.w)
- Mtume (s.a.w) kutokujua kusoma na kuandika ni ushahidi tosha kuwa
asingeweza kutunga Kitabu mfano wa Qur’an. Rejea Qur’an (7:158), (29:48)
ii. Qur’an yenyewe inajieleza kuwa ni Kitabu cha Allah (s.w) kama ifuatavyo; “Uteremsho wa Kitabu hiki umetoka kwa Mwenyezi Mungu, Mwenye Nguvu na Mwenye Hikima” (45:2)
Pia rejea Qur’an (4:166), (32:2-3), (35:31), (25:1), n.k
iii. Hali aliyokuwa nayo Mtume (s.a.w) wakati akipokea wahyi
- Mtume (s.a.w) alikuwa akiogopa kuwa atasahau anayoteremshiwa, akawa na pupa kuyakariri, hii ni ushahidi kuwa hayakuwa maneno yake.
Rejea Qur’an (75:16-18), (87:6-7)
iv. Qur’an kushuka kidogo kidogo kwa kipindi cha miaka 23 kimatukio.
- Kama Qur’an aliitunga Mtume (s.a.w) angeliitunga yote kwa pamoja tena kwa haraka ili kuitumia kuongoza jamii.
Rejea Qur’an (17:106), (25:32), (76:23)
v. Mtume (s.a.w) kukosolewa ndani ya Qur’an
- Kama Mtume Muhammad (s.a.w) angelikuwa ndiye mtunzi wa Qur’an asingelikosolewa mara nyingi katika Kitabu alichokitunga mwenyewe. Rejea Qur’an (33:1-3), (66:1), (80:1-12), n.k
vi. Kutokea kweli matukio yalitabiriwa katika Qur’an
- Mifano ya matukio ni; Waislamu kuwashinda Warumi na Maquishi na kuwa katika hali ya furaha na amani, utabiri wa kuangamia Abu Lahab. Rejea Qur’an (30:2-3), (111:1-5), (93:4-5), (94:5-6), (48:1), n.k
vii. Mpangilio na muundo wa aya na sura za Qur’an wakati wa kushuka kwake na kuandikwa katika msahafu.
- Aya na sura za Qur’an zimepangiliwa ki-idadi na kimuundo kwa namna ya ajabu ambayo hakuna mwanaadamu yeyote anayeweza kufanya hivyo.
Mfano: neno mbingu saba limetajwa mara saba, neno “Yaum” (siku)
limetajwa mara 365, neno “shahri” (mwezi) limetajwa mara 12, n.k.
Rejea Qur’an (3:59), (2:87), (2:33-37), (20:115-121), n.k
viii. Wanaadamu kushindwa kutunga na kuandika Kitabu mfano wa Qur’an
- Qur’an imetoa changamoto kwa kuwataka wanaadamu kutunga kitabu au sura moja au aya moja tu mfano wa Qur’an hakuna aliyeweza.
Rejea Qur’an (17:88), (11:13), (2:23), (10:38), n.k
ix. Maudhui ya Qur’an na mvuto wa ujumbe wake
- Qur’an inaathiri na kugonga nyoyo za watu hata ambao si waislamu, mfano Umar Ibn Khattab na mshairi Labib ibn Rabiah kabla ya kusilimu. Rejea Qur’an (20:1-7), (4:82), (39:23), n.k
x. Ahadi ya Kuhifadhiwa na kulindwa Qur’an na kubakia katika asili yake
- Ni Qur’an pekee ambayo mwanaadamu hawezi kukiharibu kwa namna
yeyote ile ya kuongeza au kupungaza chochote.
Rejea Qur’an (15:9)
b) Ushahidi kutokana na Historia (Hadith)
- Historia ilivyokuwa inashuka Qur’an na namna ambavyo Mtume (s.a.w)
alikuwa akiipokea ni ushahidi pia kama ifuatavyo;
i. Mtume (s.a.w) kushikwa na hofu na wasiwasi sana alipotembelewa na
Malaika Jibril (a.s) katika Jabal (Pango la) Hiraa.
ii. Mtume (s.a.w) alikuwa anabadilika haiba yake na kutokwa na jasho jingi wakati wa kupokea wahyi.
Rejea Hadith ya Bi Aisha (r.a)
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiw ana App yetu. Bofya liln hapo chini kuweza ku download
Download NowJe! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Views 969
Sponsored links
👉1
Simulizi za Hadithi Audio
👉2
Madrasa kiganjani
👉3
Kitabu cha Afya
👉4
kitabu cha Simulizi
👉5
Kitau cha Fiqh
👉6
Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
Kafara ya mwenye kuvunja masharti ya ihram
Soma Zaidi...
fadhila za sura kwenye quran
FADHILA ZA BAADHI YA SURA Umuhimu na ubora wa baadhi ya sura na aya. Soma Zaidi...
Siku ya Taqwiya na kusimama Arafa
5. Soma Zaidi...
swala ya witri na namna ya kuiswali
3. Soma Zaidi...
NAFASI YA SUNNAH KATIKA UISLAMU
Nafasi ya Sunnah katika UislamuMtume Muhammad (s. Soma Zaidi...
HUKUMU ZA KUSOMA QURAN, HUKUMU ZA TAJWID, HUKUMU ZA NUN SAKINA, MIM SAKINA, QLQALA NA IQLAB, TANWIN NA MADA
Soma Zaidi...
Mafunzo ya Sura Zilizochaguliwa
Soma Zaidi...
UANDISHI WA HADITHI WAKATI WA TABI'INA
Wakati wa Wafuasi wa masahaba (Tabi'ina)101-200 A. Soma Zaidi...
swala ya kuomba mvua na namna ya kuiswali
12. Soma Zaidi...
Namna ya kuswali swala ya kuombea haja
9. Soma Zaidi...