image

Hadithi aliyoisimulia Kijakazi kwa sultan

Hadithi aliyoisimulia Kijakazi kwa sultan

Hadithi aliyoisimulia Kijakazi kwa sultan

Bongoclass-burudani

SULTANI ANASIMULIWA HADITHI NA KIJAKAZI WAKE

HADITHI ILIYOSIMULIWA NA MJAKAZI WA SULTANI
Mtukufu sultani, nakwenda kukusimulia tukio lililotokea leo hii wakati tulipokuwa tunaburudika. Tulikuwa tupo kwenye tafrija moja hivi jana wakati wa jioni kabla ya juwa kuzama. Katik tafrija hiyo tulipata kusikiliza usomaji wa quran kwa sauti nzuri sana hata machozi yakatutoka. Baada ya hapo tukabahatika kusikiliza mashiri. Mshairi maarufu kutokea India alikuwepo, na alighani kwa sauti njema sana.


Baada ya burudani kuisha ndipo tukaletewa chakula kizuri sana. Vyakula vya kuoka, na nyama iliyo kaushwa vizuri ililetwa bele ya hadhara. Vinywaji vilivyo vizuri vikahudhurishwa mbele yetu. Basi tulikaa vikundi vikundi kuzunguruka sahani za vyakula. Katika kundi nililokaa nilikuwa na aliyekuwa na shughuli yake siku ile. Na hapa kitu cha kushangaza ndipo kikatokea.


Katika vyakula vilivyoletwa kulikuwepo na zerbajeh. Hiki ni chakula zilichotengenezwa kwa mchanganyiko wa vyakula kadhaa na matunda. Chakula hiki unapokila harufu yake inaweza kukaa kwa muda wa siku nzima kwenye mikono. Ni chakula kitamu na kipendwacho na watu wa Baghadad. Basi ghafla mwenzetu mmoja alipoona chakula kile akaanza kutetemeka na kutokwa na majasho kana kwamba ameona kitu cha kutisha sana.


Yule bwana hakutaka hata kula chakula kile. Sikuwa na wasiwasi sana nikajuwa lamda hali chakula kile, ama lamda kuna mtu anamdai ndio maana akapata woga. Wakati tunakula nikamuona yule bwana kidolechake gumba kimekatwa. Alipokuwa nakata nyama, nikagundua vidole vyake gumba vya mikono vyote vimekatwa. Hapo nilishindwa kujizuia kuwa na shauku, nikataka kumuuliza kulikoni. Lakini ikabidi nimsubiri amalize kula.


Kumbe wakati ule hata yule mwenye shughuli yake alikuwa anashuhudia yanayotokea. Alikuwa akinisubiri nianza kuuliza. Kwa kuwa yeye ndiye mwenye shughuli isingekuwa vyeka kumkera mgebi wake. Ndipo naye akasubiri amalize kula ili amuulize. Yule bwana alipomaliza kula nikamuuliza “ndugu yangu nimeona hata huugusa chakula hiki “zerbajeh” ama hukupendi” naye akajibu “ninakipenda ila baada ya kula ni lazima nioshe mikono yangu mara 40 kwa maji, mara 40 kwa alita na mara 40 kwa sabuni. Sasa vitu hivi hapa havipo na si vyema kusumbuwa watu kwenye shughuli hii”


Kwa shauku zaidi nikamuuliza ana nini hasa. Ndipo akanieeza kuwa chakula hiki ndio sababu ya yeye kukatwa vidole gumba vya mkono wake. Kisha akatuonyesha na vidole kumba vya miguu yake, pia vimekatwa. Hapo nikapata shauku zaidi kujuwa hasa kwa nini amekatwa vidole gumba vyake vyote vinne kwa sababu ya chakula tu.


Wakati mazungumzo yetu haya yanaendelea yule bwana Mansur mwenye shughuli yake alikuwa anasikiliza. Basi akaagizwa kuletwe ndoo mbili za maji, sabuni na alita. Hapo kopo la kunawia na alita zikaandaliwa kwa ajili ya kutoa povu vyema. Kisha ikaletwa tena sahani yenye zerbajeh. Akaambiwa ale kisha atanawa kama anavyotaka. Basi akala vyema akanywa maji na kumshukuru Mungu. Kisha akaanza kunawa na alita mara 40 kisha sabuni mara 40 kisha maji mara 40. alipomaliza tukamtaka atusimulie hadithi yake ndipo akasimulia hadithi ifuatayo:-


HADITHI YA ALIYEKATWA VIDOLE GUMBA
Mimi nilikuwa mfanyabiashara mdogo sana, katika mji wa Baghdad. Nilikuwa ni muuzaji wa kofia na mikanda pamoja na nguo za ndani za wanawake. Ijapokuwa biashara yangu ilikuwa ni ndogo lakini ilikuwa ikinitosheleza kupata rizki . sikupata kuwa na mke wakati huo. Katika sehemu tulipokuwa tukiuza mimi ndiye niliyekuwaga mgogo pekee, nikiwa na miaka 21, huku sharubu ndio zilikuwa zikianza kuota.


Siku moja akaja msichana mmoja wa kitajiri sana, niligundua hilo baada ya kumuona amepanda farasi mzuri aliyekuwa na matandiko mazuri yenye mapambo ya kupendeza zaidi. Pia alikuwa ameongozana na wajakazi wawili. Alipokuja alionekana kushangaa sana pindi lipokuwa akitazama upande tulipokuwa tumekaa mimi na mwenzangu. Basi alinagiza wajakazi wake wanunue vitu alivyotaka na walipokamilisha waliondoka, huku akiwa anatuangalia. Sikuweza kuioa sura yake wala kusikia sauti yake. Alikuwa ni mrefu wa wstani mwembamba wa kawaida. Mwenye nywele ndefu. Niligundua hilo baada ya kumuangalia vyema pindi alipogeuka.


Sikuwa na umakini naye maana hata hakuwa mteja wangu. Wiki ilipita hatimaye siku ya jumamosi nikamuona tene, siku hii alikuja kwenye biashara yangu na kuulizia mikanda ya wanawake pamoja na ngua za ndani. Akataka nimchagulie nguo ya ndani inayomuenea vyama. Nilistaajabu sana maana katu sijapata mteja aliyewahi kunieleza maneno haya ya kipuuzi. Lakini pia nilistaajabu sana niliposikia sauti yake. Sauti laini, iliyo na mikwaro, nikajikuta moyo unaenda mbio na joto la mwili wangu linaongezeka. Jasho la kwenye makwapa linaanza kunichuruzika. Kwa hakika sijapatapo kusikia sauti tamu kama hii katika maisha yangu yote.


Nilitamani azungumze nami maneno mengine, nipate kuthaminisha zaidi sauti ya binti huyu. Nilipogundua kuwa si mtu wa maneno mengi nikamuuliza, “unava saizi gani” hakunijibu swali langi, alifikiri zaidi ndipo akanijibu “niangalie kwa ukaribu vizuri utajuwa saizi yangu”. mmmmmhhh haya. Hapo nikapata fursa ya kuthaminisha ngombe kwenye gunia. Nilistaajabu sana baada ya kuona mapigo ya moyo yanaongezeka na jasho la kwapa ninanitoka.


Nikaanza kumchagulia niliyoona inamtosha, nikampatia kisha kimpatia na mkanda. Wakati naendelea kuchaguwa alikuwa akiniangalia sana usoni. Alikuwa amefunika sura yake lakini niligundua kuwa alikuwa ananikonyeza. Sikupata kuiona sura yake, lakini niliamini huenda ni mrmbo kama sauti yake. Nilianza kuvutiwa na mteja wangu. Alipomaliza vitu vyake akaondoka bila hata kujuwa anapokaa.


Niliwaza kuwa pindia akija tena nimuulize maswali kadhaa nipate kujuwa nitamkuta wapi pindi nikimtafuta. Hali haikuwa kama nilivyotaka, muda mrefu ulipita bila hata ya kumuona. Baada ya wiki kama mbili akaja tena siku hii akadai kuwa amesahau pesa hivyo anaomba nimkopee atakweda kuniletea pesa siku nyingine. Kwa kuwa nilishaanza kulewa nikakubali kumkopea.


Alichukuwa karatasi na kuanza kutaja bishaa anazotaka. Nikaenda kumkopea vitu vile nikiwa mimi ndiye dhamana. Ilikuwa ni siku ya kipupwe, nilipokuwa ninarudi ghafla nguo aliyoifunika sura yake (nikabu) ikapeperuka, na hapo nikapata kuona sura iliyobandikwa kwenye paji lake. Nilitamani awe ni sanamu liwe nyumbani kwangu. Nilipata kuvutiwa ghafla na urembo wa binti huyu. Niligundua hakuwa na mkunjo hata mmoja kwenye uso wake. Nilizidi kulewa na kupenda.


Nikamletea bidhaa na nikapata kusikia neno ahsante kutoka kwenye kinywa chake. Niligundua anatabasamu pana na la kuvutia. Matukio yote haya yalitokea kwa muda mchache sana. Alichukuwa bidhaa zile na kutokomea mtaani. Nilishikwa na butwaa na nikasahau kumuuliza ni lini ataleta pesa ya watu. Nilipata kugundua kuwa kumbe unaweza kupenda hata kwa siku moja.. sikuweza kula, kulala wala kusinzia, kana kwamba sira yake ilikuwa ipo ukutani.


Niliamaka usiku nikakamata nguzo na kushika ukuta huku nikiufananisha ndiye yeye. Hatimaye nikapitiwa na usingizi paleplae. Asubuhi nilijikuta nipo chini, nikakumbuka hasa nini kilitokea. Wii moja, mbili na hatimaye mwezi ukapita bila ya kutokea, na huku ninadeni lake. Wenye mali zao walikuwa wakinitaka nilipe pesa yako. Mikawa nawwhidi kuwa nitawalpa kesho.


DENI LA MAPENZI
Badisiku ambayo niliamua niuze vitu vya ndani kwangu ili nilipe madeni ya watu, ndipo yule binti akatokea tena. Ilikuwa kama bahati vile akanikabidhi pesa ndefu nikalipa madeni na haikubakia hata kidogo. Siku hiyo alikaa karibu nami na kuanza kuzungumza hapa na pale. Nilimuomba niione sura yake kwa ukaribu zaidi, alimuita mjakazi wake mmoja na kumwambia akae karibu naye, kisha akafunua kitambaa kilichoziba uso wake.


Nilipata kujiridhisha baada ya kukutana na nyusi ndefu zilizolala vyema, zilizo nyeusi sana, silizonyooka kama mwezi mwandamo. Macho ya duara yaliyo meupe. Nywele nyembamba, zilizoshuka kukaribia masikio. Hakuwa mweupe sana kama mwarabu wa Sham. Sikupata kujuwa nini amepaka kwenye midomo yake, maana alikuwa anameremeta. Sikutaka zaidi kumuangalia, niliamini itakuwa ni makosa. Kwakuwa nilikuwa naangalia uso, iliniridhisha kukubali uwepo wake.


Hatimaye nikatamk maneno kumweleza, kama kuna dawa umenipa. Mwenzio zilali kutwa kucha kukuwaza. Siwachi kufukiri sura yako machoni mwangu. Nakiri kwa ulimi wangu, penzi lako nahitaji. Nilijikuta nabwabwanya maneno yasiyo mpangilio, yasiyo na vina vya mashairi, wala weledi wa mazungumzo. Niliamini kubwabwanya kwangu kutakuwa kumeelewaka japo kidogo. Hakuweza kunijibu kitu chochote, ila alinieleza kuwa atanijibu kwa barua. Lakini aliniomba kuwa nimkopee tena bidhaa kama za siku ile.


Hata sikuwahi kufikiri, nikaingia kwenye maduka ya wenzangu na kumchukulia bidhaa zake. Kwa haraka akawaagiza vijakazi wake, wakafunga mzigo na kupotelea mtaani. Baada tu ya kuondoka nikaanza kujiuliza, hivi inamaana utajiri wote alionao yule binti ndo anashindwa kuwa na pesa ya kununulia bidhaa hizi?, ama hii ni mbinu ya matajiri kunyonya wanyonge. Sikuweza kuwaza sana maana kila nikikumbuka sura yake, na kimna ambavyo moyo wangu kwake, hata deni pia nalisahau.


Sasa nikawa na mambo mawili ya kusubiria, kwanza barua na pili ni pesa ya watu. Sikumoja mapema asubuhi nikapokea barua kutoka kwa mtu asiyejulikana. Barua iliandikwa kwa maandishi meusi, kutokana na wino wa ngisi uliochanganywa na manukato. Imeandikwa kwenye karatasi nzuri. Kwa shauku nilikata kamba na kufungua barua ile. Maneno machache yaliandikwa:


Salam, kipenzi, natumai upo salama. Nashukuru kwa nguo ulionichagulia siku ile imenitosha sawa. Ujumbe wa barua hii utaletewa ifikapo jioni, na pesa yako pia. Basi ilipofika jioni akaja moja kati ya wale wajakazi wake. Akanipatia pesa yangu kisha akaanza kusimulia:-


“.….. toka alipoondoka hapa siku ile hakuweza kulala kwa kukuwaza wewe. Anakupenda na amenituma nije nikwambie hivyo. Kama upo tayari anakutaka wende ukaonekane kwao.” kwani anaitwa nani na kwao ni wapi? Huu ni mzigo wa maswali nilio mjibu. Anaitwa Shaniat bint ‘Aziz mkwe wa sultani Harun Rashid. Mmh sasa nitafikaje kwao?” nilimuulliza. “…. kuna mtihani umepewa na mke wa mfalme, uende kwa siri, ukifanikiwa atafanya taratibu zote za harusi yetu badala ya kuridhishwa nawe atakapo kuona, na kama ukifeli ukakamatwa, basi utapoteza maisha” haya ndiyo maneno aliyonijibu.


Sikujuwa ni kwa nini ameamuwa kunipa mtihani huu. Lakini nilijuwa kuwa kama nisipoweza kumuona ka masiku mengi zaidi huwenda nikawa kichaa ama punguani. Niliamini ni bora nijaribu kwenda kwa siri nikifa nife kiume, kuliko kubakia hapa na kujiwazia naishia kukumbatia ukuta. Nikamjibu kuwa nimekubali. Basi akanielekeza kuwa kesho mida ya jioni niende kwenye bostani lililopo karibu na ikulu na hapo nitakutana nae.


MTIHANI PENZINI
Sikuwa na wasiwasi maana niliamini kuwa nitafanikiwa tu. Siku ile nilioga na kuvaa ngua safi na kuvaa viatu vikubwa vya kuchomeka. Nikatoka kuelekea tulipoahidiana. Nilipofika pale nikakutana na kundi la vijakazi wa kike. Mmoja wao akaniuliza ndiye wewe mgeni, wasiri? Nikamjibu ndio. Hapo wakaniambia niingie kwenye moja ya boksi la mbao kisha likafungwa vyema. Niliweza kujihisi kama nipo kwenye jeneza vile. Wakafunganya na mizigo yao mingine na tukaondoak zetu.


Walipofika getini kwnyw jumba la mfalme mabawabu (walinzi wa geti) wakataka kuchunguza kilichomo. Wale wajakazi wakasema kuwa wamebeba nguo za mke wa mfalme. Walinzi wakawaruhusu kupita. Walipofika geti la pili, wakaulizwa tena wakazungumza vilevile. Waliporuhusiwa kupita ghafla mfalme akatokea. Akasema nataka nichunguze mwenyewe vitu vinavyokwenda kwa mkewangu. Hapo nikajua sasa ndio mwisho wangu. Hapo nikaanza kuhisi mkojo unauma. Tumbo likanza kunguruma na woga ukanijaa. Nikaanza kushahadia naa kutubu madhambi yangu.


Mfalme akawaambia watue mizigo, na wafungue boksi mojamoja. Kwa mkono wake mfalme akaanza kufungua kila boksi na anapojiridhisha hufunga. Ndipo akafika kwenye boksi ambalo nimo. Alipotaka kufungua mjakazi mmoja akamwambia, “mtukufu, humu kuna nguo za ndani za Malkia, si vyema zikaonekana hadharani, tunakuomba radhi ufunue boksi hili ukiwa peke yako. Basi mfalme alionekana kukubali na hapo nafsi ikatulia kiasi. Mfalme akaagiza maboksi yote yaingizwe ndani.


Boksi ambalo nipo nikachukuliwa na kupelekwa kwengine. Baada ya mwendo wa hatua kadha upatao dakika kama 10 boksi likatuliwa na kufungulia. Hapo nikatoka nje na kupata hewa safi. Mke wa Sultani alipiga makofi kwa kunipongeza nna kuniambia nimefaulu mtihani wa kwanza. Hapo nikapiga magoti kumsalimu na kumshukuru kwa tumaini alilonipa. Aliniangalia kwa muda kama wa dakika 2 hivi na kisha kapiga tena makofi na kusema “umefaulu mtihani wa pili” sikujuwa ni mtihani gani.


Akanielekeza pa kukaa huku nikisubiria chakula. Kikaletwa chakula, na vinywaji. Niliishia kunywa maji na chakula. Nilikula kiasi kidogo. Sikutaka kula saana nikiwa ugenni. Niligundua vinywaji vile vinatofautiana rang na harufu. Kwakuwa sukjuwa kwa undani vinywaji vile nikaamuwa ninywe maji tu. Baada ya chakula akaja tena mke wa sultani. Alikaa mbele yangu na kupiga tena makofi na kusema “umefaulu mtihani wa tatu” na sasa nitakuozesha mdogo wangu, il a harusi hii itakuwa ya siri, usijefanyiwa fitina na waliokataliwa posa zao.


Nikaelekezwa chumba cha kukaa, mke wa Mfalme akaend kuzungumza na mfalme pamoja na watu wa familia yao.wakakubaliana mahari iwe vipande 500 vya dhahabu. Mke wa mfalme alitowa mahari ili kunitolea na harusi ikafanyika. Sitaki kueleza zaidi kuhusu hiyo harusi. Mambo yakawa kama hivyo, muuza mikanda nimekuwa ndugu na Sultani wa Baghadad.


KWA NINI VIDOLE GUMBA VILIKATWA?
Baada ya harusi niliendelea kukaa pale kwa muda wa miezi mitatu hata bila ya kurudi kwangu au kuwasiliana na ndugu zangu. Siku moja mkewangu akanieleza kuwa ana ujauzito. Nilifurahi sana, nilimkumbatia kwa furaha. Habari njema zikamfikia mke wa Sltani, basi akaandaa tafrija ndogo ya pale ndani kama kusherekea furaha ya mdogo wake kuata ujauzito. Katika tafrija hiyo muda wa kula ulipofika vyakula mbalimbali vikaletwa.


Nikanawa mikono na kuanza kula. Mkewangu hakuwepo alitokakidogo. Nilitamani hata awepo nipate kumlisha. Nilianza kula na kunywa kisha kikala Zerbajeh, nilipogusa tu chakula kile badhi ya wajakazi walikunja sura, Mke wa Sultani akanieleza kuwa mke wako anachukia sana harufu ya chakula hiko, na ndo umeshaanz akula, hivyo itakubidi uvumilie kwa lolote litakalo tokea. Sisi katu hatuta ingilia ugomvi wenu. Basi nilijitahidi kunawa vyema kwa sabuni. Baada ya tafrija kwisha nikarudi kujipumzisha.


Ghafla nikaona mkewangu amebadilika sura, na kuniambia “yaani mtu kama wewe unakula zerbajeh bila hata ya kunawa”? nikamueleza mkewangu kipenzi mbona nimenawa” kama umenawa na hii harufu ninayoipata ni ya nini” “ nimejitahidi kunawa ila hii harufu haikati kwa urahisi” haya ni maneno tuliokuwa tukijibizana.


Looo!!! Looo!!!! huwezi amini kumbe kubishana ndipo nikawa nauchochea moto wa kifuu. “nilikuona mstaarabu, nikakupenda, na nakupenda sana kipenzi, lakini kwa hili katu siwezi kuvumilia….,” mtu mstaarabu kama wewe unakula bila kunawa jamani, hapana …!! hapana…!!! kwa hili lazima nikupe adhabu, itabidi ukatwe vidole vyako. Ulivyokulia bila ya kunawa.


Aliagiza wajakazi wanifunge wanipeleke kwa hakinu ili nikakatwe vidole. Wakanifunga kamba na kunifungia kwenye chumba. Nilikaa kwa siku 10 kwenye kachumba hako huku nikawa ninakula mlo mmoja tu kwa siku. Siku ya kumi akawaambia wajakazi wanitoe, akaninusa mikono yangu na kujiridhisha kuwa harufu imekoka. Hapo akaagiza dawa ziletwe na mkasi, bendeji na vitu vingine. Akawaambia wajakazi wanikamate madhubuti, na hapo akanikata vidole gumba vyangu vyote


“nakukata hivi vidole vilivyokuacha ukala zerbajeh bila ya kunawa. Nataka ukumbuke kuwa chakula hiki, utakapokula unawe mara 40 kwa alita, mara 40 kwa sabuni na mara 50 kwa maji. Vinginevyo nitamaliza na vingine. Nilijiwazia mambo mengi hata nikasema huwenda ni huu ujauzit ndio unamsumbuwa. Lakini ujauzto ndi anikate vidole. Baada ya hapo alilia sana na akachukuwa dawa akanipaka na kuendelea kuniuguza.


Niligunduwa kuwa ananipenda sana, japo sikupatapo kujuwa hasa kilichomtokea hata akachukia sana chakula hiki. Milipanga siki moja nije nimuulize. Baada ya wiki kama 3 vidonda vyangu vilipona na hapo akaja mke wa sultani na aliponikuta akapiga tema makofi na kuniambia kuwa “umefaulu mtihani wa nne” sasampohuru kuondoka. Sikuwa naelewa maneno ya mke waSultani kuhusu mitihani ile lakini pia nilifurahi.


Jioni mke wangua akanipatia pesa nyingi na vipande vya dhahabu na kunieleza kuwa nikanunue nyumba nzuri ya ssi kuishi. Nilifanya hivyo, nilitafuta nyumba nzuri sana nje kidogo ya mji na sasa nina watoto wawili.






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 518


Sponsored links
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 kitabu cha Simulizi     👉5 Simulizi za Hadithi Audio     👉6 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

UANDISHI WA HADITHI WAKATI WA TABI'INA
Wakati wa Wafuasi wa masahaba (Tabi'ina)101-200 A. Soma Zaidi...

Lengo la swala
Lengo la Kusimamisha SwalaBila shaka swala imepewa umuhimu mkubwa kiasi cha kufanywa nguzo kubwa ya Uislamu kutokana na lengo lake. Soma Zaidi...

Sababu za kushuka sura kwenye quran na fadhila za sura mbalimbali kwenye quran
Soma Zaidi...

NGUZO ZA IMAN
Jifunze tawhid yaani kumpwekesha Allah subhaanah wata'aala Soma Zaidi...

MAANA YA HADITHI SUNNAH
Maana ya SunnahKilugha: Neno sunnah katika lugha ya Kiarabu lina maana ya mwenendo au mila. Soma Zaidi...

Ndoa ya mke zaidi ya mmoja na taratibu zake
Soma Zaidi...

Kulala Muzdalifa na maan yake kwa mahujaji
7. Soma Zaidi...

Kwa Nini Mwanaadamu Hawezi Kuunda Dini Sahihi ?
1. Soma Zaidi...

DARSA ZA TAWHID
Jifunze tawhid yaani kumpwekesha Allah subhaanah wata'aala Soma Zaidi...

AMRI YA KUMFUATA MTUME (s.a.w9)
Amri ya Kumfuata Mtume (s. Soma Zaidi...

Umuhimu wa ndoa na kuoa ama kuolwa katika jamii
Matamanio ya jimai ni katika maumbile na hayaepukiki. Soma Zaidi...

Maandalizi ya kujiandaa mwenyewe kabla ya kufa ama kufikwa na mauti (kifo)
Kwakuwa kila mtu anatambua kuwa ipo siku atakufa hivyo ni vyema kuanza kujiandaa mapema. Soma Zaidi...