1.
1.DINI SAHIHI ANAYOSTAHIKI KUFUATA MWANAADAMU.
Kulingana na umbile lake, mwanaadamu daima hutamani kuishi kwa furaha na amani ili kufikia lengo la kuumbwa, na hapo ndipo inambidi kuchagua dini (njia sahihi ya maisha) kati ya Uislamu, Ukafiri, Ushirikina au Utawa itakayomtimizia malengo yake.
1.1. Sifa au Vigezo Vya dini sahihi
Dini sahihi ni ile inayomuwezesha mwanaadamu kuishi kwa furaha na amani ya kweli hapa Duniani na Akhera, na ni lazima iwe na sifa zifuatazo;
(a)Dini sahihi lazima ieleze ukweli juu ya maumbile;
Ni lazima ieleze ukweli juu ya mwanaadamu, lengo la kuumbwa kwake, hadhi/nafasi yake, dhima/kazi yake na maumbile yanayomzunguka na viumbe vyote vilivyo hai na visivyo hai, na hatima ya kila kitu.
(b)Dini sahihi ni lazima iwe na kanuni na sheria zinazoendana na maumbile yote;
Kanuni na sheria za dini sahihi ni lazima ziwe sambamba na kanuni za kimaumbile ili kuepusha mgongano wowote wa kimahitajio wa kimwili na kimazingira pia.
(c)Ni lazima itosheleze mahitajio ya mwanaadamu ya kimwili na kiroho;
Pia ni wajibu kwa dini sahihi kuelekeza na kutosheleza hisia za mwanaadamu pindi anapokuwa na hali ya furaha au hali ya majonzi, namna ya kukabiliana nazo ili kubakia katika lengo lake la kuumbwa (maisha).
(d)Dini sahihi pia lazima iwe ni mfumo wa maisha uliokamilika;
Dini sahihi haina budi kuwa na utaratibu kamili wa kila kipengele na Nyanja ya maisha ya kila siku kiuchumi, kisiasa, kiafya, kiutamaduni, kisheria, kielimu, n.k.
(e)Pia dini sahihi ni lazima iwe na ibada maalum zinazombakisha mwanaadamu katika maadili na hadhi yake;
Ni wajibu kwa dini sahihi kuwa na muongozo wa kumuinua na kumbakisha mwanaadamu katika mwenendo mzuri wa kiroho (kiutu) unaoweza kuustawisha mwili na kuleta mahusiano mazuri ya kiutu yasiyo na chuki, husuda, tamaa, kiburi, vurugu, n.k.
(f)Dini sahihi haina budi kuwa ya walimwengu wote na ya nyakati zote;
Ili kufikia lengo la kuumbwa mwanaadamu, dini sahihi ni lazima iwe inawahusu watu wa aina zote (wote), isiwe na jina la mtu au mahali na isiwe na mipaka ya kijiografia, rangi za watu, mahali, nyakati, n.k.
(g)Dini sahihi ni lazima iainishe na kusimamia haki zote za mwanaadamu;
Ni wajibu kwa dini sahihi kutoa na kusimamia haki, hukumu na adhabu kwa usawa na uadilifu kwa watu wote kibinafsi na kijamii bila upendeleo na ubaguzi wowote wa kirangi, taifa, nasaba, cheo au hadhi.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 632
Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani
👉2 kitabu cha Simulizi
👉3 Kitau cha Fiqh
👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉5 Simulizi za Hadithi Audio
👉6 Kitabu cha Afya
Presha ya kupanda (hypertension) dalili zake, na njia za kukabiliana nayo
Soma Zaidi...
KUAMINI MALAIKA
Jifunze tawhid yaani kumpwekesha Allah subhaanah wata'aala Soma Zaidi...
ushahidi juu ya Dalili Za Kuwepo Mwenyezi Mungu (S.W)
Dalili Za Kuwepo Mwenyezi Mungu (S. Soma Zaidi...
DARSA ZA TAWHID
Jifunze tawhid yaani kumpwekesha Allah subhaanah wata'aala Soma Zaidi...
nmna ya kufanya istikhara na kuswali swala ya Istikhara
Soma Zaidi...
nmna ya kufanya Talbiy kwa mwenye kuhiji
2. Soma Zaidi...
Muda wa kuhiji na mwenendo wa mwenye kuhiji
Soma Zaidi...
Historia ya kuhifadhiwa na kuandikwa kwa quran toka wakati wa Mtume (s.a.w)
Soma Zaidi...
1.0 NJIA ZA KUMJUA MWENYEZI MUNGU (S.W)
1. Soma Zaidi...
swala ya kuomba mvua na namna ya kuiswali
12. Soma Zaidi...
Je mahari inashusha hadhi ya mwanamke?
Je, Mahari inashusha hadhi ya mwanamke? Soma Zaidi...
SHIRK
Jifunze tawhid yaani kumpwekesha Allah subhaanah wata'aala Soma Zaidi...