image

Kuamini siku ya mwiho: Pia utajifunza kuhusu maisha ya barzakh (kaburini), siku ya qiyama

Kuamini siku ya mwiho: Pia utajifunza kuhusu maisha ya barzakh (kaburini), siku ya qiyama

Kuamini siku ya mwisho

Kuamini Siku ya Mwisho

Hatua (mazingira) ya maisha baada ya kufa

i. Kutokwa na roho

ii. Maisha ya Kaburini (Bar-zakh)

iii. Kufufuliwa na kuhudhurishwa mbele ya Allah (s.w)

iv. Kuhesabiwa na kuhukumiwa mwanaadamu (viumbe)

v. Maisha ya peponi kwa watu wema au motoni kwa watu waovu kulingana na vitendo vyao duniani.




Hoja au Madai ya Makafiri juu ya kuwepo Siku ya Mwisho na udhaifu wake


a) Mwanaadamu hana lengo la kuumbwa (maisha) isipokuwa ni kustarehe tu.

Udhaifu wa hoja hii;

- Kwa kutumia vipawa vya akili, ufahamu na utambuzi, hakuna uwezekano wa kuumbwa viumbe na maumbile mbali mbali na kuwekewa kanuni maalum kisha kusiwe na lengo la vitu hivyo.
Rejea Qur’an (44:38), (38:27)



- Lengo kuu la kuumbwa mwanadamu ni kumuabudu Muumba wake ipasavyo.

Rejea Qur’an (51:56), (102:8)



b) Hapana uwezekano wa kuwepo uhai baada ya mtu kuoza na kusagikasagika

- Makafiri wanapinga kuwepo uhai baada ya kufa na kusagikasagika katika udongo kwa kudai kuwa ni jambo muhali na halingii akilini mwao.
Rejea Qur’an (79:10-12), (56:47-48), (45:25)



Udhaifu wa hoja hii;

- Kutojulikana muda maalum wa siku ya mwisho sio hoja kudai kutokuwepo kwake, kwani kuna vitu hatuvidiriki katika milango ya fahamu lakini vipo.

- Kufufuliwa na kuwepo uhai baada ya kufa kutafanyika kwa wanaadamu wote wa mwanzo hadi wa mwisho kwa wakati mmoja na sio muda tofauti tofauti. Rejea Qur’an (34:3), (56:49-50)


- Aliyeumba na kuanzisha umbile la mwanzo atashindwaje kurejesha umbile lile kwa mara ya pili?
Rejea Qur’an (50:15), (30:27)



c) Kufa si lolote bali ni mtindo tu wa maisha ya ulimwengu.

- Makafiri wanadai kuzaliwa, kuishi na kufa ndio mtindo wa maishi ya ulimwengu, hivyo mtu akifa nafasi yake kuishi imekwisha.
Rejea Qur’an (45:24)



Udhaifu wa hoja hii;

- Kuumbwa kwa mwanaadamu kulifanyika kwa lengo maalum la kumuabudu

Allah (s.w) tu.

Rejea Qur’an (51:56)

- Mbingu na ardhi na maumbile yote tunayoyaona na tusiyoyaona hayakutokea kwa bahati nasibu, bali yupo Mjuzi aliyeumba na kupangilia kanuni zake. Rejea Qur’an (36:77-83), (75:3-4), (88:17-20)




d) Waliokufa hawajarudi kutoa ushahidi

- Wapinzani wa siku ya mwisho wanakana kuwepo uhai baada ya kufa kwa kusingizia kuwa hakuna mtu alikufa kisha akafufuka kutoa ushahidi.
Rejea Qur’an (45:25), (16:38-40)



Udhaifu wa hoja hii;

- Utaratibu wa Allah (s.w) ni kuwa, ufufuo utafanyika kwa wakati mmoja kwa watu wote na sio kwa mtu mmoja mmoja kwa muda wake.
Rejea Qur’an (56:49-50).



Hoja zinazoonesha Umuhimu na Ulazima wa Kuwepo Siku ya Mwisho

Kuwepo Siku ya mwisho ni jambo lililobudi (lisiloepukika) kwa sababu zifuatazo;



i. Wale waliofanya wema hapa duniani walipwe ujira na fadhila zao inavyostahiki.

Rejea Qur’an (55:60)



ii. Wale waliodhulumu haki za watu hapa duniani warudishe haki hizo kwa wenyewe mbele ya Hakimu wa Mahakimu.
Rejea Qur’an (95:8)



iii. Wale wababe waliofanya uovu uliokithiri hapa duniani bila kuadhibiwa wapate adhabu inayostahiki, wahukumiwe kwa mujibu wa makosa yao.
Rejea Qur’an (1:4)



iv. Watu waulizwe kwa vipi walitumia neema na vipaji mbali mbali walivyotunukiwa katika kuliendea lengo la kuumbwa kwao.
Rejea Qur’an (102:8)



v. Wabainike ni akina nani walifuata dini au njia sahihi ya maisha, waislamu au makafiri.
Rejea Qur’an (16:38-39), (39:46)



Ushahidi wa ufufuo kutokana na historia

Miongoni mwa matukio ya kihistoria yanayothibitisha kuwepo uhai baada ya kufa ni;



i. Mtu (msafiri) na punda wake waliokufa walifufuka baada ya miaka mia (100).

Rejea Qur’an (2:259)



ii. Kufufuka ndege wanne (4) wa Nabii Ibrarahim (a.s) kama mujiza wa kuonesha uwezekano wa kufufuliwa viumbe.
Rejea Qur’an (2:260)


iii. Kuamka vijana wa pangoni baada ya kulala kipindi cha muda wa miaka 309 ili kuwa ushahidi wa kufufuka viumbe baada ya kufa.
Rejea Qur’an (18:25)



iv. Kufufuka kwa watu wa Nabii Musa (a.s) waliokufa walipotaka kumuona Allah

(s.w) kwa dhahiri (jahara).

Rejea Qur’an (2:55-56)



v. Kufufuka kwa mtu (Myahudi) aliyeuliwa kwa dhuluma zama za Nabii Musa (a.s) ili

amtaje aliyemuua baada ya kupigwa na sehemu ya nyama ya ng’ombe. Rejea Qur’an (2:72-73)


vi. Nabii Isa (a.s) kufufua wafu (watu waliokufa) kwa idhini ya Allah (s.w) kama sehemu ya muujiza wake.
Rejea Qur’an (3:49), (5:111)



Ushahidi wa ufufuo kutokana na maisha ya kila siku

- Matukio ya maisha kila siku yanayothibitisha uwepo wa ufufuo ni kama ifuatavyo;

1. Kufa kwa ardhi (mimea) wakati wa kiangazi na kufufuka wakati mvua ikinyesha.

Rejea Qur’an (41:39)



2. Kufufuka (kuamka) kutoka usingizini baada ya mtu kulala.

Rejea Qur’an (30:23)



3. Kufufuka (kuzindukana) kutoka kwenye kuzimia ni ushahidi mwingine wa ufufuo ambapo mtu huwa hajitambui na hajiwezi kwa lolote lile.
Rejea Qur’an (7:143), (16:40)

Mazingira ya Siku ya Mwisho (Maisha ya Akhera) kwa mujibu wa Qur’an na Hadith

- Maisha ya Akhera yana hatua sita zifuatazo:

i. Kufikwa na mauti

- Ni hatua ya kutengana kati ya roho na mwili, ambapo roho hubakia hai hadi siku ya mwisho.
Rejea Qur’an (4:78), (56:83-87), (63:10-11), (23:99-100)



- Hali ya kutokwa na roho hutofautiana kati ya mtu mwema na muovu.

Rejea Qur’an (89:27-30), (79:1-2), (75:24-35)



ii. Maisha ya Kaburini (Barzakh)

- Ni kipindi anachokaa mtu baada ya kufa kwake mpaka kufufuliwa kwake siku ya Qiyama.
Rejea Qur’an (23:99-100), (14:27)



iii. Kufufuka na kukusanyika kwenye uwanja wa hesabu

- Ni pale watu wote, wa mwanzo na wa mwisho watafufuliwa baada ya kupigwa parapanda la pili na kuhudhurishwa mbele ya Allah (s.w) ili wahukumiwe.
Rejea Qur’an (39:68), (36:51-54), (80:33-42), (99:1-8), (82:17-19)



iv. Siku ya Hukumu

- Ni siku ambayo Ufalme utakuwa wa Allah (s.w) pekee na kila mmoja atahukumiwa kulingana na vitendo vyake.
Rejea Qur’an (40:16), (39:69), (84:8), (2:143), (45:28), (70:10), (17:13-14), (18:49), (99:7-8)


v. Makazi ya Peponi

- Ni mazingira (makazi) mazuri na bora watakaoishi watu wema tu yenye kila aina ya starehe isiyo na kikomo.
Rejea Qur’an (32:17), (36:55-58), (3:15-17), n.k

vi. Makazi ya Motoni

- Ni mazingira (makazi) mabaya watakaoishi watu waovu tu yenye kila aina ya adhabu na mateso yasiyo na kikomo.
Rejea Qur’an (15:43-44), (25:66), (37:62-67), (32:10-14), (78:21-30), (89:23-
26), (4:56), (22:19-22), (23:103-108), (44:43-50), (56:51-56), (38:55-58), (20:74), (67:6-11), (25:65-66).



Majina au Daraja (Milango) Saba ya Moto

- Kila muovu ataingia aina ya moto kwa mujibu wa vitendo vyake kama ifuatavyo;

1. Jahannam: – ni jina la ujumla la maisha ya motoni.

Rejea Qur’an (15:43-44)



2. Lahab: – ni Moto wenye muwako mkubwa sana.

Rejea Qur’an (111:3)



3. Hutwamah: – ni Moto wa kuvunjavunja, uliowashwa kwa ukali mno.

Rejea Qur’an (104:4)



4. Sai’ra: – ni Moto mkali mno unaounguza.

Rejea Qur’an (4:55)



5. Saqara: – ni Moto unaobabua ngozi mara moja.

Rejea Qur’an (74:26)



6. Jahiim: – ni Moto mkali sana.

Rejea Qur’an (26:91), (102:6)



7. Haawiyah: – ni Moto uwakao kwa ukali sana.

Rejea Qur’an (101:9)



                   





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 655


Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Kitau cha Fiqh     👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉6 Simulizi za Hadithi Audio    

Post zifazofanana:-

Sababu Ya Uislamu Kuwa Ndiyo Dini Sahihi Pekee
1. Soma Zaidi...

Kafara ya mwenye kuvunja masharti ya ihram
Soma Zaidi...

fadhila za kusoma quran
Fadhila na umuhimu wa kusoma quran 1. Soma Zaidi...

HADITHI 40 ZA IMAMU NAWAWI: haithi za Mtume (s.a.w) 40 zilizoandikwa na Imam Nawaw)
Soma Zaidi...

Swala ya kupatwa kwa jua na mwezi na namna ya kuiswali
11. Soma Zaidi...

Zijuwe suna (sunnah) za Udhu ama Kutawadha
Soma Zaidi...

Hutuba ya ndoa wakati wa kuoa
Soma Zaidi...

Muda wa kuhiji na mwenendo wa mwenye kuhiji
Soma Zaidi...

SIRA (HISTORIA YA ) MTUME MUHHAMAAD (S.A.W) KUZALIWA KWAKE, VITA ALIVYOPIGANA, SUNNAH ZAKE NA MAFUNDISHO YAKE
Soma Zaidi...

Hadithi aliyoisimulia Kijakazi kwa sultan
Soma Zaidi...

swala ya idi na nmna ya kuiswali swala ya idi
6. Soma Zaidi...

Ujumbe wa Qur-an Utawafikiaje Wale wasio Waarabu au wale Wasiojua Kiarabu?
Ujumbe wa Qur-an Utawafikiaje Wale wasio Waarabu au wale Wasiojua Kiarabu? Soma Zaidi...