Navigation Menu



image

NAMNA YA KUOMBA DUA, SUNNAH ZA DUA NA FADHILA ZA DUA

NAMNA YA KUOMBA DUA, SUNNAH ZA DUA NA FADHILA ZA DUA

Darsa za Dua

Ustadh Rajabu

DARSA ZA DUA

Sifanjema zinamstahikia Allah Mola wa viumbe, muumba wa mbingu na ardhi na vilivyomo. Mfalme na mmiliki wa ulimwengu na siku ya mwisho. Sala na amani zimuuendee kipenzi cha Allah mtume Muhammad (s.a.w) pamoja na masahaba zake na watu wa familiya yake.


Ama baada ya utangulizi huu, hiki ni kitabu cha dua kilichoandaliwa kwa ajili ya kutoa mafunzo juu ya dua na yanayohusiana. Kitabu hiki kimeandaliwa kwa lugha ya kiswahili na iliyo nyepesi zaidi ili kuwezesha wasomaji wapate kuelewa. Maandalizi ya kitabu hiuki yametokana na mafunzo kutoka kwenye quran na sunnah.


Kitabu hiki ni waqfu kwa ajili ya Allah na hakiuzwi. Kwa yeyote atakayetaka kukiprint awasiliane nasi kwa +255675255927 au rajabumahe@gmail.com. Kitabu hiki kimeanza kusambazwa kwa njia ya kimtandao hivyo tunatoa wito kwa anayeteka kukiprint awasiliane nasi kwa haraka zaidi.


Hiki ni kitabu cha kwanza katika mfululizo huu wa vitabu vya dua kutoka kwetu. Inshaa Allah tunatarajia kutoa mwendelezo wa kitabu hiki siku za mbeleni. Pia tunatoa wito kwa yeyote mwenye kuweza kuandika vitabu awasiliane nasi lkwa ajili ya mazungumzo zaidi.


Tumeandaa kazi hii kwa ajili ya Allah kwa kutaraji radhi zake na si vinginevyo. Pia tunatarajia dua kutoka kwenu wasomaji ili Allah atusamehe madhambi yetu pamoja na wazazi wetu na waislamu kwa ujumla.


Tunaomba kwa yeyote atakayeona kuna makosa kwenye kitabu hiki awahi haraka sana kuwasiliana nasi ili kuzuia kusambaa kwa makosa zaidi. Kitabu hiki cha kwanza nimekigawa katika sehemu kuu tano kama zitakavyoelezwa chini hapo.


Wabillah tawfiq
Al- ustadhi Rajabu Athuman
+255675255927
rajabumahe@gmail.com





KITABU CHA DUA
Hiki ni kitabu cha dua na ni waqfu kwa ajili ya Allah. Hakiuzwi na na sio ruhusa kukiuza. Kwa anayetaka kukiprint ni bure awasiliane nasi pindi akitaka kufanya hivyo.


Tumeandika kitabu hiki kwa kutarajia radhi za Allah na kutoa mafundisho kwa waislamu na si vinginevyo.


DUA
Kwa ufupi dua ni kumuomba Allah akuondoshee lililobaya, ama linalo kuudhi ama akupe jambo fulani. Na dua ni ibada kama ibada nyingine.


Dua ni jambo lenye kupendeza kama walivyosema maulamaa na masalafi wema walotangulia. Umuhimu wa dua na msisitizo wake unapatikana katika quran na sunnah.


Dua zimesisitizwa sana katika quran na sunnah hata mtume akasema لِيَسْأَلْ أَحَدُكُمْ رَبَّهُ حَاجَتَهُ حَتَّى يَسْأَلَهُ الْمِلْحَ “na aombe mmoja wenu haya yake (dua) kwa Allah mpaka chumvi.…”. Hivyo si kuomba mambo kakubwa tu na matatizo tulonayo ila mpaka chumvi.


FADHILA ZA DUA
1.Dua ni ibada. Basi utambue ewe ndugu muislamu kuwa dua ni ibada. Imepokewa hadithi kutoka kwa Nuuman Ibn Bashir رضىالله عنه kuw Mtume wa Allah صليالله عليه وسلم amesema "‏ الدُّعَاءُ هُوَ الْعِبَادَةُ“hakika dua ni ibada” (imepokewa na Tirmidh na ameisahihisha).


2.Dua ndio jambo tukufu zaidi kwa Allah kama Mtume صليالله عليه وسلم aliposema katika hadithi iliyosimuliwa na Abu Huraurah رضىالله عنه kuwa Mtume amesema “hakuna kitu kitukufu mbele ya Allah kuliko dua” (imapokewa na tirmidh, imam Ahmad na Alhaakim kwa isnad sahihi) لَيْسَ شَيْءٌ أَكْرَمَ عَلَى اللَّهِ تَعَالَى مِنَ الدُّعَاءِ “


3.Allah anamchukia mtu ambaye hamuombi. Abuu Hurairah رضىالله عنه amesema kuwa Mtume صليالله عليه وسلم amesema "‏ مَنْ لَمْ يَسْأَلِ اللَّهَ يَغْضَبْ عَلَيْهِ ‏" “mtu yeyote ambaye hamuombi Allah, Allah humchukia mtu huyo” (amepokea hadithi tirmidh)


4.Allah anapenda kuombwa. Katika masimulizi ya Ibn Mas’ud رضىالله عنه Mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema “muombeni Allah katika fadhila zake, hakika Mwenyezimungu Mtukufu (غزّ وجلّ) anapenda kuombwa” (amepokea Tirmidh).


5.Dua ni malango wa rehema. Katika masimulizi ya ibn ‘Umar رضىالله عنه kuwa Mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema "‏ مَنْ فُتِحَ لَهُ مِنْكُمْ بَابُ الدُّعَاءِ فُتِحَتْ لَهُ أَبْوَابُ الرَّحْمَةِ وَمَا سُئِلَ اللَّهُ شَيْئًا يَعْنِي أَحَبَّ إِلَيْهِ مِنْ أَنْ يُسْأَلَ الْعَافِيَةَ ‏"‏ “mwenye kufunguliwa mlango wa dua, hufunguliwa mlango wa rehema.…” (amepokea Tirmidh).


6.Dua huondosha mabalaa na majanga. Katika masimulizi ya Ibn ‘Umar, رضىالله عنه Mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema “hakika dua hunufaisha kwa (hukinga) yale yanayoshuka (yanayotokea), na yale ambayo hayajashuaka ( hayajatokea). Basi jilazimisheni na (kuomba) dua enyi waja wa Allah.


ADABU ZA KUOMBA DUA.
1.kuelekea qibla. Amesimulia Abdallah Ibn Zayd رضىالله عنه kuwa “alitoka Mtume صلّي الله عليه وسلّم kwenda kuomba dua ya mvua akaelekea kibla”. (amepokea Bukhari).


2.Kunyanyua mikono miwili juu. Amesimulia Abuu Musa رضىالله عنه kuwa “aliomba Mtume صلّي الله عليه وسلّم dua akanyanyua mikono yake mpaka nikaona weupe wa kwapa lake” (amepokea Bukhari). Na amesimulia Ibn ‘Abas kuwa Mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema ‏ "‏ إِذَا دَعَوْتَ اللَّهَ فَادْعُ بِبُطُونِ كَفَّيْكَ وَلاَ تَدْعُ بِظُهُورِهِمَا فَإِذَا فَرَغْتَ فَامْسَحْ بِهِمَا وَجْهَكَ “muombeni Allah kwa matumbo ya viganya vyenu, wala msimuombe kwa migongo ya viganja vyenu.…”. (amepokea Abuu Daud na Bayhaqiy).


3.Kuanza dua kwa kwa kumsifu Allah na kumshukuru (kama kusema alhamdu lillah ….) na kumswalia Mtume صلّي الله عليه وسلّم. Amesimulia ‘Abdullah Ibn Mas’ud رضىالله عنه kuwa nilikuwa nikiswali, wakati Mtume yupo na Abuubakar na ‘Umar, basi nilipokaa nikaanza kumshukuru Allah na kumsifu na nikamswalia Mtume صلّي الله عليه وسلّم kisha nikajiombea dua, akasema mtume صلّي الله عليه وسلّم ‘omba utapewa, omba utapewa’”. (amepokea tirmidh kwa isnad sahih). Na katika masimulizi ya Fudailah Ibn ‘Ubayd رضىالله عنه amesema “hakika amefundisha mtume صلّي الله عليه وسلّم uma wake jinsi ya kuomba dua akasema ‘pindi anapoomba dua mmoja wenu basi aanze na tahmid (kumshukuru Allah) na thanaai (kumsifu Allah) kisha amswalie Mtume صلّي الله عليه وسلّم kisha aombe chochote anachotaka’” ‏"‏ إِذَا صَلَّى أَحَدُكُمْ فَلْيَبْدَأْ بِتَحْمِيدِ اللَّهِ وَالثَّنَاءِ عَلَيْهِ ثُمَّ لِيُصَلِّ عَلَى النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم ثُمَّ لِيَدْعُ بَعْدُ بِمَا شَاءَ ‏"‏ (amepokea Abuu Daud, tirmidh, Ibn Hiban na baihaqy).


4.Kuanza kuomba dua kwa kujiombea mwenyewe. Kwa anayetaka kumuombea mtu mwingine dua anatakiwa aanze na kujiombea mwenyewe. Amesimulia Ubaiya Ibn K’ab رضىالله عنه kuwa عَنْ أُبَىِّ بْنِ كَعْبٍ، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم كَانَ إِذَا ذَكَرَ أَحَدًا فَدَعَا لَهُ بَدَأَ بِنَفْسِهِ “alikuwa mtume صلّي الله عليه وسلّم anapomkumbuka mtu na akataka kumuombea dua huanza kwa kujiombea mwenyewe kwanza.” (amepokea tirmidh kwa isnad sahih).


5.Kurudia rudia katika kuomba na kusisitiza maombi yako. Ila usiharakishe majibu kutaka kujibiwa haraka hata ukawa unamlaumu Allah. Amesimulia Abdallah ibn Ms’ud رضىالله عنه kuwa alikuwa Mtume صلّي الله عليه وسلّم anapenda kuomba mara tatutatu na (akawa) anaomba istighfar (msamaha) mara tatutatu. (amepokea Abu Daud kwa isnad salih).


6.Kuwa na yaqini juu ya kujibiwa na kujiepusha na yaliyo haramu. Mtu anatakiwa asiwe na shaka juu ya kujibiwa dua yake. Amesimulia Abuu Hurairah رضىالله عنه kuwa Mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema "‏ ادْعُوا اللَّهَ وَأَنْتُمْ مُوقِنُونَ بِالإِجَابَةِ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ لاَ يَسْتَجِيبُ دُعَاءً مِنْ قَلْبٍ غَافِلٍ لاَهٍ ‏"‏ “muombeni Allah mkiwa na yakini juu ya kujibiwa na jueni kuwa Allah hakubali dua ya mtu ambaye moyo wake umeghafilika naye. (amepokea Tirmidh na Alhaakim).


7.Usiharakishe kujibiwa. Isitokee mtu akawa na haraka ya kutaka maombi yake yajibiwe kama anavyotaka yeye kwa haraka hata akawa analaumu. Amesemulia Abuuhurairah رضىالله عنه kuwa Mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema "‏ يُسْتَجَابُ لأَحَدِكُمْ مَا لَمْ يَعْجَلْ يَقُولُ دَعَوْتُ فَلَمْ يُسْتَجَبْ لِي ‏" “atajibiwa (dua yake ) mmoja wenu maadam hajaharakisha (kujibiwa) akawa anasema nimeomba na wala sijajibiwa”. (amepokea Bukhari na Muslim). Na katika masimulizi mengine ya Abuuhrairah kuwa mtume amesema “hataacha mja kujibiwa dua yake maadam hajaomba madhamdhi au kukata udugu”. (amepokea Muslim na Abuu Daud). Hii ina maana dua itajibiwa tu ila isiwe ya kuomba madhambi au kukata udugu.


8.Kuitikia “aamiin”. Mwenye kuomba dua basi aitikie “aamiin” eidha awe mwenyewe pekee au yupo na kundi la watu. Amesimulia Abuuhurairah رضىالله عنه kuwa Mtume صلّي الله عليه وسلّم “atakapoomba dua mmoja wenu basi na aitikie ‘aamiin’ mwenyewe’”. (amepokea Ibn ‘Adiy).


MASHART YA KUKUBALIWA KWA DUA.
1.kuchunga adabu za dua kama zilivyotajwa hapo juu.


2.Kuwa twahara nje na ndani. Yaani kujiepusha na mambo maovu na machafu ya siri na yasiyo ya siri. Amesema Mtume صلّي الله عليه وسلّم “hakika Allah ni mzuri na anapenda (vitu) vizuri.…”. (amepekea Bukhari na Muslim) Hivyo mtu anatakiwa ahakikishe ni mzuri ndani na nje.


3.kujiweka mbali na yaliyo haramu yote, na kujiepusha kula na kunywa bya haramu au kuvaa vilivyo haramu. Amesema Mtume صلّي الله عليه وسلّم “ukitaka dua maombi yako basi kifanye kizuri chakula chako (kisiwe cha haramu) “ (amepekea Bukhari na Muslim). Na pia katika hadithi ndefu iliyo sahihi katika kuwa mtume anashangaa mtu ambaye chakula chake haramu, kinywaji chake haramu, a mavazi yake haramu. Isitoshe mtu huyu amechafuka na manywele yapo timtim. Vipi atajibiwa dua yake mtu huyu. (amepekea Bukhari na Muslim).


4.Kuzingatia nyakati ambazo dua hujibiwa. Tutaziona hapo mbele.


5.Sifa ya dua yenyewe. Tutaona dua zenye sifa ya kujibiwa.


6.Hali inayozunguruka dua. Tutaona hali ambazo dua hujibiwa.


NYAKATI AMBAZO DUA HUJUBIWA.
1.Theluthi ya mwisho ya usiku. Huu ni usiku wa manane usiku mkubwa. Muda huu mweye kuomba dua katu haiwezi kurudi kama anavyosimulia Abuuhurairah رضىالله عنه kuwa Mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema "‏ يَنْزِلُ رَبُّنَا كُلَّ لَيْلَةٍ إِلَى السَّمَاءِ الدُّنْيَا حِينَ يَبْقَى ثُلُثُ اللَّيْلِ الآخِرُ فَيَقُولُ مَنْ يَدْعُونِي فَأَسْتَجِيبَ لَهُ وَمَنْ يَسْأَلُنِي فَأُعْطِيَهُ وَمَنْ يَسْتَغْفِرُنِي فَأَغْفِرَ لَهُ ‏" “anashuka Mola wetu aliye tukuka kuja mbingu ya dunia kila usiku pindi inapobaki theluthi ya usiku ya mwisho kisha husema ‘nani ataniomba nimjibu maombi yake, nani antaniomba nimpe na nani ataniomba msamaha nimsamehe”. (amepokea Bukahari, muslim na wengine).


2.Baada ya swala za faradhi. Anayetaka kuomba dua basi aombe baada ya kuswali swala ya faradhi, dua yake itajibiwa. عَنْ أَبِي أُمَامَةَ، قَالَ قِيلَ يَا رَسُولَ اللَّهِ أَىُّ الدُّعَاءِ أَسْمَعُ قَالَ ‏"‏ جَوْفُ اللَّيْلِ الآخِرُ وَدُبُرَ الصَّلَوَاتِ الْمَكْتُوبَاتِ ‏"‏ Amesimulia Abuu Umama رضىالله عنه kuwa aliulizwa Mtume صلّي الله عليه وسلّم ‘dua gani husikulizwa (zaidi na Allah? Akasema:) usiku mkubwa (theluthi ya mwisho ya usiku) na baada ya swala za faradhi’”. (amepokea tirmith kwa isnad sahihi).


3.Kati ya adhana na iqama. Huu ni muda unaopatikana baada ya kuadhiniwa na mpaka kukimiwa kwa swala. Hapa mwenye kuomba dua itakuwa ni yenye kujibiwa. Amesimulia Anas رضىالله عنه kuwa Mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema “hairudishi (haiachi kujibiwa dua) kati ya adhana na iqama”. (amepokea Abuu Daud, Nisai na tirmith kwa isnad sahihi).


4.Wakati wa kusujudi. Hii ni dua inayoomwa wakati mtu akiwa amesujudi, dua hii pia ni yenye kujibiwa. Amesimulia Abuuhurairah رضىالله عنه kuwa Mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema “muda ambao mja anakuwa karibu zaidi na Mola wake ni pale akiwa amesujudi. Basi zidisheni dua (muda huu) na uweni na uhakika kuwa mtajibiwa. (amepokea Muslim na Daud).


5.Muda wa kukutana majeshi kwenye jihad, muda wa kunyesha kwa mvua, muda wa kukimiwa kwa swala na na muda wa kuiona alkaba. Amepokea Abuu Umamah رضىالله عنه kuwa Mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema: “hufunguliwa milango ya mbinguni na hujibiwa dua katika maeneo manne (nyakati): muda wa kukutana safu katika jihadi, muda wa kunyesha kwa mvua, muda wa kukimiwa kwa swala na muda wa kuiona alkaba”. (amepokea Tabrany).


6.Siku ya ijumaa. Siku ya ijumaa kuna muda ambao dua hujibiwa bila ya tatizo. Muda huu ni mchache sana na hakuna anaoujua. Zipo riwaya nyingi sana zinataja muda huu. Ila kuna riwaya zinaonesha muda huu ni baada ya swala ya al-’asr mpaka magharib. Ila ukweli ni kuwa muda huu ni mchache sana na haujulikani, jambo la msingi ni kujitahidi kumuomba Allah siku ya ijumaa yote huenda muda huo ungeupata.


HALI AMBAZO MTU AKIOMBA DUA ITAJIBIWA.
1.Dua ya kumuombea aliye mbali. Chukulia mfano una ndugu yako yupo nchi nyingine ama mji mwingine kisha ukamkumbuka na ukataka kumuombea dua, basi dua hii itajibiwa tu. Mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema “hakika dua iliyo nyepesi (na haraka ) kujibiwa ni dua ya mtu kumuombea aliye mbali” (amepokea Abuu Daud na Tirmidh kwa isnad sahihi). Pia amesimulia Abuu Dardaa رضىالله عنه kuwa mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema “dua ya mtu muislamu ni yenye kujibiwa anapomuombea ndugu yake aliye mbali. Juu ya kichwa chake kuna Malaika anaitikia ‘aamiin’ na wewe upate mfano wa wake”. (amepokea Ahmd na Muslim).


2.Dua ya mzazi, msafiri na mwenye kudhulumiwa. Hali za watu watatu hawa wakiomba dua Allah atajibu dua zao bila ya shaka. Mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema ‏ "‏ ثَلاَثُ دَعَوَاتٍ يُسْتَجَابُ لَهُنَّ لاَ شَكَّ فِيهِنَّ دَعْوَةُ الْمَظْلُومِ وَدَعْوَةُ الْمُسَافِرِ وَدَعْوَةُ الْوَالِدِ لِوَلَدِهِ


3.“dua za watu watatu (hawa) ni zenye kujibiwa na hakuna shaka juu ya hili: dua ya mzazi, msafiri na mwenye kudhulumiwa”. (amepokea Abuu Daud, Ahmad na Tirmidh kwa sanad sahihi).


4.Dua ya mwenye swaum (funga), imamu muadilifu, na mwenye kudhulumiwa. Watu hawa dua zao zitajibiwa tu, kingozi muadilifu, mtu aliyekuwa kwenye funga na kabla hajafuturu na mtu aliyedhulumiwa. Amesema Mtume صلّي الله عليه وسلّم watu watatu dua zao hazirudi: mwenye funga mpaka afutauru, imamu muadilifu (kiongozi muadilifu), na mwenye kudhulumiwa.…….” (amepokea tirmidh kwa isnad sahihi).


SIFA ZA (MANENO NA MATAMSHI YA) DUA YENYE KUJIBIWA.
Hapa tutaona dua iliyo katika sura ambayo Allah ataijibu. Dua zenye kujibia wakati mwingine zina sura yake na sifa zake katika maneno na matamshi. Hebu tuone sifa hizo.


1.Dua ya nabii Yunusi. Mwenye kuomba dua na akatumia maneno aliyoyasema nabii Yunusi (amani ishuke juu yake) dua hii ni yenye kujibiwa. Amesema mtume صلّي الله عليه وسلّم “dua ya nabii Yunus pindi alipokuwa kwenye tumbo la samaki (aliseme) ‘LAA LILAAHA ILLAA ANTA, SUBHAANAKA INII KUNTU MINADHWALIMIINA’ hakika hataomba mtu muislamu dua kwa kutumia maneno haya kitu chochote isipokuwa atajibiwa na Allah”. (amepokea tirmidh).


2.Kuomba dua kwa kutumia jina la Allah lililo kubwa. Allah ana majina mengi na mazuri. Lakini katika majina hayo lipo ambalo ni kubwa na ukiomba dua kwalo lakina utajibiwa. Kwa ufupi ni kuwa jina hili limefichwa na hakina yeyote anayelijuwa. Ila mtume ametowa ishara ya kuonesha wapi linapatikana na maneno gani mtu atumie kulipata jina hilo.


Amesema mtume صلّي الله عليه وسلّم “jina kubwa la Allah lipo kwenye aya sita za mwisho za surat hashri. (amepokea Dilamy kutoka kwa Ibn ‘Abas). Pia katika mapokezi mengine ya Tabrany kutoka kwa Ibn ‘Abas kuwa mtume amesema jina kubwa lipo kwenye aya ya 20 ya surat al-imran. Na pia zipo hadithi nyingi sana zinazoashiri wapi jina hilo lipo. Nitaleta chache tuu.


i) Aisha رضىالله عنها aliomba dua hii “ ALLAHUMMA INII AD’UKA LLAHA WA-AD’UKAR-RAHMANA, WA-AD’UKAL-BARRAR-RAHIIMA, WA-AD’UKA BIASMAAIKAL-HUSNAA KULLIHAA MAA ‘ALIMTU WAMAA LAM A’ALAM AN TAGHFIRA LII WATARHAMNII” Mtume akacheka kisha akasema “hakika jina kubwa lipo ndani ya dua hii. (amepokea Ibn Maajah kutoka kwa ‘Aisha) hadithi hii ni ndefu nimeikatisha na kuchukua hiyo dyua tu. ii)hadithi ya Anasرضىالله عنهkuwa” عَنْ أَنَسٍ، قَالَ دَخَلَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم الْمَسْجِدَ وَرَجُلٌ قَدْ صَلَّى وَهُوَ يَدْعُو وَيَقُولُ فِي دُعَائِهِ اللَّهُمَّ لاَ إِلَهَ إِلاَّ أَنْتَ الْمَنَّانُ بَدِيعُ السَّمَوَاتِ وَالأَرْضِ ذَا الْجَلاَلِ وَالإِكْرَامِ ‏.‏ فَقَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم ‏ "‏ تَدْرُونَ بِمَ دَعَا اللَّهَ دَعَا اللَّهَ بِاسْمِهِ الأَعْظَمِ الَّذِي إِذَا دُعِيَ بِهِ أَجَابَ وَإِذَا سُئِلَ بِهِ أَعْطَى ‏"amesimulia Anas رضىالله عنه kuwa alikuwa amekaa na mtume صلّي الله عليه وسلّم wamekaa msikitini na kulikuwa na mtu mmoja anaswali kisha akaomba dua kwa kusema “ ALLAHUMMA ANNII AS-ALUKA BIANNALAKAL-HAMDA, LAA ILAAHA ILLA ANTAL-MANNAANU BADI’US-SAMAAWATI WAL-ARDH YAA DHALJALALI WAL-IKRAM YAA HAYYU YAA QAYYUUM” akasema Mtume صلّي الله عليه وسلّم umemuomba Allah kwa jina lake kubwa ambalo anapoombwa kwalo atajibu”. (amepokea tirmidh kwa isnad gharib).


iii)amesimulia Abdillah Ibn Buraydah رضىالله عنه kutoka kwa baba yake kuwa Mtume صلّي الله عليه وسلّم alimsikia mtu mmoja akisema “ALLAHUMMA INNIASALUKA BIAN-ASHHADU ANNAKA ANTALLAHU LAA ILAAHA ILLA ANTA. AL-AHADUS-SWAMADUL-LADHII LAMYALID WALAM YUULAD, WALAM YAKUN LAHU KUFWAN AHAD” akasema Mtume صلّي الله عليه وسلّم hakika umemuomba Allah kwa jina lake kubwa ambalo akiombwa hutoa na akiombwa dua hujibu. (amesimulia Abuu Daud,tirmidh,Ibn Maajah na Ibn Hiban).


Iv). Mtume amesema اسْمُ اللَّهِ الأَعْظَمُ فِي هَاتَيْنِ الآيَتَيْنِ ‏{وَإِلَهُكُمْ إِلَهٌ وَاحِدٌ لاَ إِلَهَ إِلاَّ هُوَ الرَّحْمَنُ الرَّحِيمُ}‏ وَفَاتِحَةِ سُورَةِ آلِ عِمْرَانَ ‏"‏Jina kubwa la Allah linapatikana kwenye aya hizi‘ waillahukum ilahu wahidu laa ilaaha illa huwar-rahmanir-rahiim’ na mwanzoni mwa surat al ‘Imran


3.dua ya Mtume صلّي الله عليه وسلّم ni yenye kujibiwa. "‏ لِكُلِّ نَبِيٍّ دَعْوَةٌ مُسْتَجَابَةٌ وَإِنِّي اخْتَبَأْتُ دَعْوَتِي شَفَاعَةً لأُمَّتِي وَهِيَ نَائِلَةٌ إِنْ شَاءَ اللَّهُ مَنْ مَاتَ مِنْهُمْ لاَ يُشْرِكُ بِاللَّهِ شَيْئًا ‏"‏ Katika hadithisahihi mtume amesema Nabii yeyote ameomba dua yake na akajibiwa. Na nikaifanya dua yangu mimi ni shifaa kwa umati wangu sikku ya qiama. (amepokea Bukhari, Muslim na tirmidh kutoka kwa Anas).


4.Dua wakati wa raha hujibiwa wakati wa shida. Hii ni sifa ya dua yenye kujibiwa mbayo watu wengi hatujui. Nikuwa pindi unapopata neema na raha hapo ndipo pa kumuomba Allah na Allah atakujibu wakati unapopata matatizo kwa kukufariji na kukuondlea matatizo. Amesimulia Abuuhurairah رضىالله عنه kuwa mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema "‏ مَنْ سَرَّهُ أَنْ يَسْتَجِيبَ اللَّهُ لَهُ عِنْدَ الشَّدَائِدِ وَالْكُرَبِ فَلْيُكْثِرِ الدُّعَاءَ فِي الرَّخَاءِ ‏" ‏ “mwenye kutaka kujibiwa dua yake wakati akiwa na shida basi azidishe kumuomba Allah wakati wa raha”. (amepokea Tirmidh kwa isnad gharib).


Na katika mapokezi mengine amesema Mtume صلّي الله عليه وسلّم "‏ مَنْ سَرَّهُ أَنْ يَسْتَجِيبَ اللَّهُ لَهُ عِنْدَ الشَّدَائِدِ وَالْكُرَبِ فَلْيُكْثِرِ الدُّعَاءَ فِي الرَّخَاءِ ‏" “Mwenye kupenda kujibiwa dua zake wakati wa shida na taabu basi na azidishe dua wakati wa raha” (amepokea tirmidh)


KUKUSANYIKA KATIKA DUA.
Ni jambo la kupendeza kuomba dua mkiwa kwenye kundi. Zipo dua ambazo siku zote zinaombwa watu wakikusanyika kama dua ya kuomba mvua. Kukusanyika kwenye dua ni sunnah katika sunnah zingine.


Ijulikane kuwa pindi mtu akiomba dua kisha wengine wakaitikia aamiin huenda katika waloitikia akawepo walii wa Allah ambae ikawa sababu ya dua kujibiwa. Pia watu waliokuwepo kwenye kundi aombe mmoja na wengine waitikie aamiin na wanyanyue mikono yao.


Maswahaba Allah awaridhie walikiwa wakiombeana dua na walikuwa pia wakikusanyika kayika kuomba dua. Mtume صلّي الله عليه وسلّم alikuwa pia akiwahimiza maswahaba wake kuwa katika kundi wanapoomba dua na wengine waitikie aamiin. Amesimulia Habiib Ibn Salamah رضىالله عنه kuwa mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema “halikusanyiki kundi la watu na wakaomba dua wengine na wengine wakaitikia ‘aamiin’ isipokuwa Allah ataijibu dua hiyo”. (amepokea tbrany, Bayhaqy na Alhaakim).


NAMNA AMBAYO ALLAH HUJIBU DUA.
Itambulike kuwa dua ambayo imefata vigezo na masharti ya dua itajibiwa tu. Ila pia itambulike kuwa dua hujibiwa katika njia kuu tatu ambazo ni kupewa alichoomba, kufutiwa madhambi au kulipwa siku ya qiama kwa kuingizwa peponi. Hivyo itambuluke kuwa mtu anaweza kuomba dua kisha asijibiwe huenda Allah anataka kumpa kheri zaidi au huenda ameshamjibu kwa kumfutia madhambi yake. Allah ndiye anaejua lile ambalo ni bora kwa wajawake katika wakati wowote ule.


Amesimulia Abuuhurairah رضىالله عنه kuwa Mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema مَا مِنْ أَحَدٍ يَدْعُو بِدُعَاءٍ إِلاَّ آتَاهُ اللَّهُ مَا سَأَلَ أَوْ كَفَّ عَنْهُ مِنَ السُّوءِ مِثْلَهُ مَا لَمْ يَدْعُ بِإِثْمٍ أَوْ قَطِيعَةِ رَحِمٍ ‏"‏ “ “mtu yeyote anaeomba dua ila atajibiwa ima awahishiwe kujibiwa haphapa duniani, au acheleweshewe (kujibiwa hapa duniani na badala yake ) ajibiwe akhera au asamehewe madhambi yake kwa kiasi kile alichoomba, maadam hajaomba (jambo la) madhambi au kukata udugu aua hajafanya haraka ya kutaka kujibiwa hata akawa anasema ‘nimemuomba Mola wangu na hakunijibu’”. (amepokea tirmidh).
Pata kitabu Chetu Bofya hapa






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 2357


Sponsored links
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 kitabu cha Simulizi     👉5 Kitabu cha Afya     👉6 Simulizi za Hadithi Audio    

Post zifazofanana:-

DARSA ZA QURAN
DARSA ZA QURAN 1. Soma Zaidi...

HADITHI 40 ZA IMAMU NAWAWI: haithi za Mtume (s.a.w) 40 zilizoandikwa na Imam Nawaw)
Soma Zaidi...

swala ya kuomba mvua na namna ya kuiswali
12. Soma Zaidi...

UANDISHI WA HADITHI WAKATI WA TABI'I TABI'IIN
Wakati wa Wafuasi wa Masahaba (Tabi'i Tabi'ina)201-300 A. Soma Zaidi...

ihram na nia ya Hija na Umra
1. Soma Zaidi...

ushahidi juu ya Dalili Za Kuwepo Mwenyezi Mungu (S.W)
Dalili Za Kuwepo Mwenyezi Mungu (S. Soma Zaidi...

Ni nini maana ya ndoa?
Soma Zaidi...

fadhila za sura kwenye quran
FADHILA ZA BAADHI YA SURA Umuhimu na ubora wa baadhi ya sura na aya. Soma Zaidi...

swala ya witri na namna ya kuiswali
3. Soma Zaidi...

Swala za tahajud na namna ya kuziswali
4. Soma Zaidi...

nmna ya kufanya istikhara na kuswali swala ya Istikhara
Soma Zaidi...

Kwa Nini Mwanaadamu Hawezi Kuunda Dini Sahihi ?
1. Soma Zaidi...