1. Kuwa Muaminifu (Kuchunga Amana)

Uaminifu ni uchungaji wa amana. Amana ni kitu chochote halali mtu alichokabidhiwa ili akihifadhi na kukirudisha kwa mwenyewe atakapokihitaji au ili akitumie inavyostahiki au akifikishe mahali palipokusudiwa. Mali uliyokabidhiwa na mtu au umma ni amana; uongozi au cheo ulichopewa na jamii ni amana.

Amana kuu aliyotunukiwa Binadamu na Mola wake Ni roho, vipaji au vipawa vyote alivyonavyo na neema zote za Allah(sw) zilizomzunguka. Binadamu ametunukiwa vitu hivi ili aweze kumuabudu Mola wake inavyostahiki na kuwa Khalifa wetu katika ardhi. Amana hii kuu anaibainisha Allah (sw) katika aya ifuatayo:“Kwa yakini sisi tulidhihirisha amana juu ya mbigu na ardhi na milima (majabali) vikakataa kuichukua na vikaiogopa lakini mwanadamu akaichukua. Bila shaka yeye ni dhalimu mkubwa, mjinga sana. ” (33:72)

Amana iliyokataliwa na kuogopewa na mbingu, ardhi na milima (ya majabali) si nyingine bali amana ya kuwa Khalifa wa Allah(sw) kuongoza ulimwengu kwa kufuata kanuni na sheria zake.

Hivyo kila mwenye akili hanabudi kuwa na yakini kuwa chochote alicho nacho ni amana kutoka kwa mola wake Muumba ili aitumie katika kumuabudu ipasavyo na kusimamisha ukhalifa katika jamii. Allah (sw) anatukumbusha mara kwa mara juu ya amana hii na kutuamuru:“Sema: Hakika swala yangu, na matendo yangu (ibada zangu) na uzimawangu na kufa kwangu ni kwa ajili ya Allah. Hana mshirika wake. Na haya andiyo niliyoamrishwa, na mimi ni wa kwanza wa waliojisalimisha ”. (6:1 62-1 63).

Muislamu wakweli anatakiwa awe na msimamo huu. Awe na yakini kuwa kila alichonacho ni cha Allah (s.w)na analazimika kukitumia kwa ajili yake tu. Kinyume cha hivyo ni kumfanyia khiana Allah (s.w) na Mtume wake. Tunaonywa katika Qur-an:“Enyi mlioamini! Msimfanyie khiana Allah na Mtume wala msikhini amana zenu na hali mnajua. Na jueni ya kwamba mali zenu na watoto ni mtihani na jueni ya kwamba kwa Mwenyezi Mungu yapo malipo makubwa. (8:27-28).“Hakika wamefuzu waumini.... Ambao amana zao na ahadi zao wanaziangalia” (23:1, 8)

Kutokana na uzito wake hebu tuangalie amana katika upeo mpana katika utendaji wetu wa kila siku .Uongozi wa aina yoyote ni amana

Uongozi wa aina yoyote ni amana na Muislam anahimizwa achunge amana hiyo ndio Uislam wake ukamilike. Mtume (saw) ames em a:

“Kila mmoja wenu ni mchunga na ataulizwa juu ya wale au vile alivyokuwa akivichunga. Imamu (kiongozi) ni mchunga. Ataulizwa juu ya wale aliokuwa akiwaongoza . mwanamume ni mwangalizi wa watu wa nyumbani kwake. Ataulizwa juu yao. Mke ni mwangalizi wa nyumba ya mumewe. Ataulizwa juu ya jukumu hili. Mtumishi (mfanyakazi) ni mwangalizi wa vitu au mali ya mwajiri wake . Ataulizwa juu ya jukumu hili”.Madaraka ni Amana

Pamoja na amana hii ya uongozi aliyonayo kila mtu kutokana na nafasi yake ya asili katika jamii kuna amana nyingine ambazo hukabidhiwa na jamii kwa watu kulingana na uwezo wao. Kazi na majukumu ni lazima vigawanywe kulingana na uwezo wa kila mtu ili kila mtu achunge amana yake. Kumpa mtu kazi au madaraka asiyo na uwezo nayo ni kumuingiza kwenye mtihani na wenye kumchagua watakuwa ni wenye kuulizwa juu ya kushindwa kwake. Halikadhalika mtu kujipachika mwenyewe madaraka au kuomba madaraka au kazi asiyo na uwezo nayo ni kujiingiza katika kujifelisha mtihani kwa ushahidi wa hadith ifuatayo;

Abu-Dhar (r.a) amesimulia kuwa alimuomba Mtume (saw) amchague kuwa Gavana wa nchi fulani. Mtume (saw) kusikia ombi hili alitingisha bega lake na akasema:Ee Abu-Dhar! Wewe ni dhaifu na madaraka haya ni amana. Siku ya kiyama hili litakuwa ndio chanzo cha aibu na fedheha. Lakini watasalimika wale watakao chukua madaraka hayo (kazi hiyo) na wakayaendesha kama inavyostahiki. (Muslim)

Katika Uislamu, si ujuzi na uzoefu wa kazi tu vinavyoangaliwa katika kumvisha mtu amana ya kazi au madaraka Fulani, bali hapana budi viambatane na tabia nzuri na uaminifu. Halikadhalika tabia nzuri na ucha-mungu havitatosha kumfanya mtu achaguliwe kufanya kazi fulani, bila ya kuwa na ujuzi na uzoefu unaostahiki. Mfano mzuri tunaupata kwa Nabii Yusuf (a.s) yeye alikuwa Mtume wa Allah(sw) na kwa hiyo alikuwa mfano bora wa tabia njema na ucha-mungu. Lakini hakujitolea kuchukua dhima ya kuendesha nchi kwa misingi ya tabia njema na utume wake tu bali pia kwa msingi wa ujuzi juu ya wadhifa huo kama tunavyofahamishwa katika aya ifuatayo:Akasema(Yusuf):”Nifanye mtazamaji wa khazina za nchi (yote) hakika mimi ni mlinzi mzuri na mjuzi hodari”. (12:55)

 

Uchaguzi ni Amana

Tunatakiwa tuwe waaminifu katika kuwachagua watu kuchukuwa nafasi za kazi katika nyadhifa mbali mbali. Tuwachague kutokana na ujuzi wao, uzoefu wao, tabia yao, na uaminifu wao. Kama kutokana na hongo , udugu, unafiki, ukabila au upendeleo wa namnayoyote, tutaacha kufuata utaratibu wa kumchagua mtu kulingana na sifa zinazostahiki kwa kazi fulani na badala yake tukawachagua wasiostahiki, tutakuwa moja kwa moja tumekhini(tumefanya khiyana). Mtume (saw) amesema kuwa:

Atakaye mchagua kiongozi kwa upendeleo ambapo palikuwa na mtu mwingine ambaye alistahiki zaidi mbele ya Allah kuliko yule aliyemchagua, basi atakuwa amemfanyia khiana Allah, Mtume wake na waislamu wote. (Hakim)Kazi ni Amana

Pamoja na kuwa waaminifu katika kuwachagua watu kwa nyadhifa na kazi mbalimbali, waliochaguliwa nao wanatakiwa wawe waaminifu katika kutekeleza kazi. Muislamu analazimika kuifanya kila kazi yake kwa ufanisi na kila mara ajitahidi kuifanya vizuri zaidi.

Inafahamika wazi kuwa uzembe katika kazi huleta madhara mengi katika jamii. Kutokana na kukosekana uaminifu katika kutekeleza majukumu mbali mbali katika jamii huzaa magonjwa mengi ambayo hudhoofisha jamii. Magonjwa haya ni wizi, hongo, upendeleo, n.k. Uzembe na ulaghai katika kazi vimeshutumiwa vikali katika Uislamu kama inavyobainishwa na hadith zifuatazo:

Mtume wa Allah amesema: “katika siku ya Hukumu wakati Allah (sw) atakapokusanya watu wote, waliopita na wasasa, bendera itakitwa kwa kila Mlaghai (mdanganyifu) ambayo itamtambulisha. Kisha itanadiwa kuwa hili ni kundi la wadanganyifu”. (Bukhari)

Katika hadith nyingine Mtume (saw) amesema:

Patakuwa na bendera katika kila kichwa cha mdanganyifu itakayoinuliwa kulingana na udanganyifu wake . Sikilizeni! Hapana ulaghai au udanganyifu mkubwa kuliko ule wa Amir (Kiongozi) anayedanganya watu (ummah). (Muslim)

Kwa maana nyingine hapatakuwa na mdanganyifu mkubwa zaidi anayestahiki kupata adhabu kali zaidi mbele ya Allah (sw) kuliko yule alipewa madaraka kuangalia mambo ya watu katika jamii halafu akawa amelala usingizi wa kukoroma (anastarehe) bila ya kujali matatizo yaliyowaelemea.Mali ya Umma ni Amana

Uaminifu ni pamoja na kutochukua kitu cha mtu binafsi au kitu cha ummah pasina idhini ya wenyewe. Kuchukua mali ya mtu au mali ya umma na kuwapa wengine pasi na idhini au kuifanyia shughuli isiyopendelewa na mwenye mali ni hiana au ukosefu wa uaminifu. Hata kuchukua malipo zaidi kuliko mahitaji ya mtu ya lazima ni kufanya khiana. Kuhusu jambo hili Mtume (saw) amesema:

Yeyote yule tutakaye mpa shughuli, upatikanaji w a m ahitaji yake itakuw a ni jukumu letu pia, kama utachukuwa zaidi kuliko mahitaji yake basi atakuwa anakhini. (Abu Daud)

Hapa tunapata fundisho kuwa katika Uislam watu watakao ajiriwa na umma kutoa huduma mbali mbali watastahiki kulipwa mishahara itakayowawezesha kutosheleza mahitaji yao. Atakayepokea mshahara zaidi ya mahitaji yake bila ya kujali wadhifa wake na cheo chake atakuwa amekhini mali ya Ummah. Atakuwa amekhini kwa sababu atakuwa ametumia mali ya ummah ambayo ilitakiwa wapewe wanaohitajia zaidi, kama vile maskini,mafakiri, mayatima, wasafiri walioharibikiwa katika njia ya Allah, n.k. tunaonywa katika Qur’an:“Na hiana kwa nabii kufanya khiyana atakayefanya khiana, atavileta siku ya kiyama alivyovifanyia khiana, kisha kila mtu atalipwa kwa aliyoyachuma, wala hawatadhulumiwa”. (3: 161)

Ni kawaida kuwa watu wengi hudharau au hulichukulia kwa wepesi suala la uaminifu katika mali ya ummah. Kinyume chake Uislamu umelipa uzito sana suala hili. Uislamu umeharamisha unyonyaji wa mali ya ummah hata kwa mali iliyo ndogo kiasi gani. Msisitizo wa ubaya wa kuhini (mis-appropriate) mali ya ummah, ambao hufunga njia zote za kujipatia mali kwa njia za haramu, uko wazi katika Hadith zifuatazo:

Adi bin Umaira (r.a) amesimulia kuwa amemsikia Mtume (saw) akisema: “Yeyote yule tutakayempa madaraka na akawa ameficha sindano au kitu kidogo kuliko hiki, basi atakuw a amekikhini na atatokea nacho siku

ya Kiyama”Pale pale aliinuka Ansar mweusi akasema:”Ee Mtume wa Allah! Nivue madaraka (nijiuzulu) ya Ugavana. ” Mtume alimuuliza kuwa kuna nini? Akajibu (Ansar): “ Nimesikia yote uliyozungumza sasa hivi”. Mtume(saw) akasema; “Bado ninasema kuwa yeyote yule tutakayemfanya gavana hana budi kutuonyesha kila kitu (katika mali ya ummah). Achukuwe chochote kile kilicho haki yake na akiw eke pembeni chochote kile alichoambiwa akitunze”. (Muslim).

Katika hadith nyingine, mtu mmoja aliyeitwa Ibn Labtih kutoka kabila la Uzd alitumwa na Mtume (saw) kama kiongozi wa kukusanya zakat na sadaqa. Aliporudi na alivyokusanya alisema; “Hivi ndivyo vitu vyenu na hivi nimepewa zawadi “. Msimulizi wa Hadith hii anasema aliposikia habari hii Mtume (saw) alisimama na kumhimidi Allah kisha akasema;

…Ninamchagua miongoni mwenu kiongozi wa mambo haya ambayo Allah (sw) amenipa majukumu nayo. Wakati mtu huyo anaporudi, anasema hiki ni chetu na hiki nimepewa zawadi. Kama anasema kweli kwa nini asingelibakia nyumbani kw a w azazi wake. Hebu tuanga lie hasa niwapi zawadi hii imetoka? Kwa jina la Allah, kama yeyote miongoni mwenu anapokea kitu chochote kisichomstahiki, siku ya Kiyama atatokea mbele ya Allah(s.w) akiwa amebeba kitu hicho. Sitaki kumwona yeyote yule miongoni mwenu, akutane na Allah (sw) akiwa amebeba ngamia kichwani mwake au ngombe au mbuzi wakilia kichwani mwake na akasema;

“Ee Allah! Nim efikis ha ujumbe wako”. (Muslim).Siri ni Amana

Kutoa siri za watu, kikundi au nchi ni ukosefu wa uaminifu wa hali ya juu. Ufujaji wa siri huharibu mipango yote ya kheri iliyokusudiwa kufanywa. Ufujaji wa siri huvunja ushirikiano, uhusiano na urafiki kati ya watu. Mtume (saw)amesema;

Wakati mtu anapomwambia mwingine jambo kisha akamgeukia (akamwambia kuwa ni siri), basi hiyo ni amana.

Uislamu unasisitiza sana kuwa mambo yote ya siri yaliyoongelewa kwenye mkutano wowote usioenda kinyume na maadili ya Uislamu ni lazima yachungwe. Hapana siri kwa mikutano inayojadiliana kutenda maovu. Muislamu akitokea kuhudhuria mikutano ya kujadili mambo ya uovu huo. Kuhusu siri za mikutanoMtume (saw) amesema:

Siri ya mikutano ni amana, lakini mikutano ya aina tatu haitajuzu kutunziwa siri; ule ambao damu inamwagwa bila haki; ule ambao unahusiana na uzinifu; au ule ambao mali inaporwa. (Abu Daud).Siri za ndani ya nyumba haziruhusiwi kabisa kutolewa nje, hata jirani au rafiki wa karibu sana hatakiwi akafahamu. Na siri za mke na mume zinatakiwa ziishie chumbani. Mtume (saw) amesema:Katika siku ya Hukumu, jambo litakalo kuwa la uhaini mkubwa kuliko yote mbele ya Allah (sw) ni mume kutoa siri ya mkewe kwa wengine, hata kama mume atakuwa anampenda mkewe na mkewe akawa anampenda mum ewe. (Muslim).Muislamu wa kweli ni lazima awe ni mwenye kuaminika pindi anapoaminiwa kwa kupewa amana yeyote ile iwe ni mali, madaraka, heshima, siri, n.k. Kama anavyotuhakikishia Mtume (saw) katika hadith;Mfano mzuri wa uchungaji wa amana ni ule aliouonesha Mtume (saw) katika kipindi kigumu cha mabadiliko muhimu ya historia ya ulimwengu. Tunafahamu kuwa Mtume(saw) alikuwa mwaminifu mno mpaka akapewa jina la Al-Amiin (mwaminifu) kwa kiasi ambacho hata wale waliokuwa wakimpiga vita walikuwa wakiweka amana zao kwake. Safari ya kuhamia Madina ilipowadia na wakati maisha yake yalipokuwa hatarini (kwani njama za kumuua zilishatimia), Mtume (saw) hakusahau amana za watu alizokuwa nazo pamoja na kwamba watu hao hao ndio maadui zake. Akambakiza Ali(r.a) ili kuwarudishia wenyewe amana zao ndipo afunge safari kumfuata Mtume na masahaba wengine Madina. Leo hii Muislamu akikhini amana ya mtu atakuwa na kisingizio gani? Madhambi yote husameheka mbele ya Allah isipokuwa kufa na dhambi ya shirk na kukhini amana ya mtu. Siku ya Kiama ni lazima amana hiyo irejeshwe kwa mwenyewe. Kila Muislamu wa kweli hana budi Kumuiga Mtume (saw) na kuwa Amiin (mwaminifu) katika maisha yake yote.