1. Kujiepusha na Uwongo

Uwongo ni kinyume cha ukweli. Uwongo ni giza na ukweli ni nuru. Uwongo ni upotofu na ukweli ni uongofu. Ambapo ukweli ni uhakika wa asili wenye kudumu, uwongo ni uzushi ambao hutoweka mara tu ukweli u nap os im am a.“Na sema: Ukweli umefika na uwongo (batwili) umetoweka. Hakika uw ongo ndio w enye kutow eka.” (17:81)

Uongo ni uovu wenye kumuangamiza mja hapa duniani na huko akhera. Aidha uwongo ni miongoni mwa maovu makubwa mbele ya Allah (s.w) kama inavyobainika katika Hadith zifuatazo:

Abubakar (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: Nikufahamisheni juu ya madhambi makubwa katika madhambi

makubwa? Sikia! Ni kumshirikisha Allah (s.w), kutotii wazazi na kusema uwongo”. (Bukhari na Muslim).

Katika Hadithi nyingine tunafahamishwa:Abubakar (r.a) anasimulia kuwa Mtume wa Allah aliuliza: “Je, nikufahamisheni madhambi makubwa?” Aliuliza swali hilo mara tatu. Tukamjibu: “Kwa nini usitufahamishe, Ee Mtume wa Allah?” Akaeleza “Ni kumshirikisha yeyote na Allah (s.w). “Na kusema uwongo na kutoa ushahidi wa uwongo. “Aliendelea kurudia hili mpaka tukaanza kujishauri, kuwa ingelikuwa vyema kama tusingelimuuliza. ” (Bukhari)Mtume (s.a.w) ametukataza kusema uwongo hata katika mazungumzo ya utani. Mtume (s.a.w) alitoa makemeo makali kama ifu atavyo:

Kuna Kifo kw a mtu anayejihusisha na simulizi za uw ongo ili kuchekesha watu na kuna kifo kwake, kuna kuangamia kwake. (Tirmidh).

Katika Hadith nyingine Mtume (s.a.w) amesema:

Muumini hataweza kuikamilisha imani yake mpaka aache kusema uwongo katika utani na katika midahalo hata kama ni mkweli katika mambo yote mengine. (Ahmad)

Pia katika Hadith nyingine Mtume (saw) aliulizwa;

Kuwa Mu is lamu anaweza kuwa mwoga. Akajibu “Ndiyo”. Akauliza tena, “ Je, Mu is lamu anaweza kuwa bakhili?” akajibu, “Ndiyo, anaweza kuwa bakhili. ” Aliuliza tena, “Je, Muumini anaw eza kuw a mw ongo?” Alijibu, “Hapana ”. (Malik)Ieleweke kuwa si kwamba maovu mengine yaliyotajwa katika Hadith hii yanaruhusika, bali maovu hayo baada ya kuyafanya muislamu anaweza kutanabahi na kurejea kwa mola wake kwa kuleta toba ya kweli na toba ya kweli haipatikani mpaka awe mkweli katika kukiri makosa yake. Kwa mujibu wa Hadith, Mwongo si Muumini bali Mnafiki.

Mtume (saw) pia anatutahadharisha tujiepushe na kuwabembeleza watoto kwa kuwadanganya kuwa tutawapa zawadi fulani. Mtume(saw) anasisitiza kuwa ukimwahidi mtoto zawadi hunabudi kumletea zawadi hiyo. Tukiwadanganya watoto hao kwamba tutawapa kitu na tusiwape, tutakuwa tunawafundisha uwongo.Uwongo na Ulaghai katika Biashara

Waislamu wa kweli hawanabudi kuwa wakweli katika kila kipengelecha maisha yao. Imekuwa kawaida kwa wafanyabiashara waliowengi kutumia udanganyifu na ulaghai katika biashara ili kujipatia faida kubwa. Wafanyabiashara wasio waadilifu mara nyingi huwapunja watu kutokana na kutojua kwao bei halisi za vitu, hasa wanunuzi wanapokuwa wageni wa sehemu ile. Pia baadhi ya wafanyabiashara huchanganya bidhaa mbovu na nzuri au kuficha dosari (upogo) ya bidhaa na kuiuza kwa bei ya bidhaa nzima. Na baadhi ya wafanyabiashara hutumia viapo vya uwongo ili kuwahadaa watu wanunue bidhaa zao. Huu wote ni udanganyifu katika biashara. Biashara ya namna hii ni biashara haramu kama Mtume (saw) anavyotufahamisha :

“ Si halali kwa Mu is lamu kuuza bidhaa yenye dosari, mpaka azioneshe dosari hiyo kw a mnunuzi. ” (Bukhari)

“…Kiapo cha uwongo kitasaidia biashara inunuliwe , lakini inapunguza mapato”.(Ahmad)Ni wapi uwongo unaporuhusiwa?

Katika maisha ya kila siku kuna sehemu tatu tu ambapo uwongo unaruhusiwa. Ni katika vita, katika kuleta suluhu na katika maongezi ya kusuluhishana kati ya mume na mkewe au mke na mumewe kama tunavyojifunza katika hadith zifuatazo:-Asma bint Yazid (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah (saw) amesema: Uwongo si halali ila katika mambo matatu; uwongo wa mume kwa mkewe (au wa mke kwa mumewe) ili kumfurahisha; uwongo katika vita na uwongo katika kusuluhisha au kuleta amani kati ya watu”. (Ahmad, Tirm idh).Ummu Kulthumu bint U’qubah (r.a) amesema, Sikumsikia Mtume wa Allah (saw) akitoa ruhusa ya kusema uwongo juu ya chochote watu wanachosema ila katika mambo matatu:- vita, kurudisha amani kati ya watu (kusuluhisha) na mazungumzo ya mume kwa mkewe au ya mke kwa mumewe”. (Muslim)Hivyo, Muislamu wa kweli analazimika kuwa mkweli katika mazungumzo, katika mahusiano yake ya wengine na katika utendaji wake wa kila siku katika kila kipengele cha maisha yake. Atakuwa mkweli katika mazungumzo ya kawaida, katika uchumi, siasa , familia, n.k. Pia ukweli kwa muumini ni lazima upatikane katika dhamira, msimamo na utii.