picha

kuwa na kauli njema, na faida zake katika jamii

11.

kuwa na kauli njema, na faida zake katika jamii

11. Kuwa na Kauli Njema


Muislamu anatakiwa kila mara azungumze mambo ya maana na ya kheri. Ulimi utumike kusema ukweli, kuamrisha mema, kukataza maovu, kuwashauri wengine juu ya mambo ya kheri, kupatanisha waliogombana, kumsabihi Allah, kutoa elimu yenye kunufaisha watu na katika mazungumzo mengine ya kheri.


“Na ni nani asemaye kauli bora kuliko (yule) aitaye (watu) kwa Allah na (mwenyewe) akafanya vitendo vizuri na kusema (kwa maneno yake na vitendo vyake): “Hakika mimi ni miongoni mw a Waislamu ”. (41:33).
Allah (s.w) anatuamrisha kusema maneno mazuri katika aya ifu atayo:

“Na waambie waja wangu waseme daima maneno yaliyo mazuri. Maana Shetani huchochea ugomvi baina yao. Hakika shetani kwa wanaadamu ni adui aliye dhahiri”. (17:53)
Hivyo Muislamu hana budi kuzungumza na watu kwa maneno mazuri ya heshima. Maneno mazuri ya heshima yanajenga na kuzidisha upendo kati ya watu. Maneno mazuri ya heshima ni ngao ya kumzuilia shetani asiingilie kati na kuleta migongano na kutoelewana. Ni katika msingi huu tunaamrishwa tuulinganie Uislamu kwa hekima na kwa mawaidha mazuri:

“Walinganie (watu) katika njia ya Mola wako kwa hekima na mawaidha m em a, na ujadiliane nao kw a namna iliyo bora. Hakika Mola w ako ndiye anayemjua aliyepotea katika njia yake naye ndiye anayewajua walioongoka ”. (16:125).
Kauli njema ni yenye kumuongoza mja kwenda Peponi na kauli mbaya humuongoza mja kwenda Motoni kama tunavyojifunza katika Hadithi zifuatazo:
Sahl bin Sa ’d(r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: “Atakayeweza kuchunga kilichopo kati kati ya taya zake (ulimi) na kilichopo katikati ya miguu yake miwili (utupu) ninaw eza kumhakikishia Pepo.” (Bukhari).

Abu Hurairah(r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: “Mja atatamka neno lenye kumfurahisha Allah bila ya kuona uzito wake, bado Allah (s.w) humlipa malipo makubwa kutokana na neno hilo. Na mja atatamka neno lenye kumuudhi Allah bila ya kuona uzito wake, na bado linakuw a ndio mw anzo w a kumuingiza Motoni. (Bukhari).



                   

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Sunnah Main: Post File: Download PDF Views 2776

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Dua za Mitume na Manabii     👉4 web hosting     👉5 ai web app     👉6 Bongolite - Game zone - Play free game    

Post zinazofanana:

NAMNA AMBAZO DUA HUJIBIWA

NAMNA AMBAYO ALLAH HUJIBU DUA.

Soma Zaidi...
Wajbu wa wazazi kwa watoto wao

Wajibu wa Wazazi kwa Watoto Wazazi wanawajibu kwa watoto wao.

Soma Zaidi...
Historia ya Imamu Bukhary Muandishi wa Hadithi za Mtume s.sa. w

Hii ni historia ya Imamu Bukhary pamoja na kitabu chake cha sahihul Bukhari.

Soma Zaidi...
AINA ZA HADITHI

Aina za HadithKuna aina kuu mbili za Hadith- (a) Hadith Nabawiyyi.

Soma Zaidi...