Mipaka katika kuwatii Wazazi
Pamoja na msisitizo huu mkubwa wa kuwatii wazazi, utii wetu kwao ni lazima ulandane na utii wetu kwa Mwenyezi Mungu (s.w) na Mtume wake. Endapo watatuamrisha tufanye jambo lolote lile Iinalokwenda kinyume na maamrisho ya Mwenyezi Mungu (s.w) na Mtume wake tutalazimika kutowatii na kubakisha utii wetu kwa Mwenyezi Mungu (s.w) na Mtume wake kama inavyobainishwa katika aya zifuatazo:
Na tumemuusia mwanaadamu afanye wema kwa wazazi wake; na kama wakikushurutiza kunishirikisha na yale usiyo na ilimu nayo, basi usiwatii, kwangu ndiyo marejeo yenu, basi nitakwambieni mliyokuwa mkiyatenda. (29:8).
Na (wazazi wako) wakikushurutisha kunishirikisha na (yale) ambayo huna ilimu nayo, usiwatii, lakini kaa nao kwa wema hapa duniani; shika njia ya wale wanaoelekea kwangu, kisha marejeo yenu ni kwangu, hapo nitakuambieni mliyokuwa mkiyatenda. (3 1:15).
Hata hivyo, pamoja na aya hizi kutukataza kuwa tusiwatii wazazi wetu endapo watatuamrisha kumshikirikisha Mwenyezi Mungu (utii kwa yeyote yule kinyume na Mwenyezi Mungu ni shiriki), bado tunasisitizwa tuwaheshimu, tuwahurumie na kuwatendea wema kwa kadiri ya uwezo wetu wote katika mambo yote ya kheri. Hana radhi ya Mwenyezi Mungu (s.w) yeyote yule atakayewavunjia heshima na kuwatendea visivyo wazazi wake na hata wazazi wa wengine. Hebu tuzingatie Hadith ifuatyo:
Abdallah bin Umar amesimulia kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema:Katika madhambi makubwa, ni mtu kuwatukana wazazi wake. Wakauliza (Maswahaba); Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Mtu anawezaje kuwatukana wazazi wake? "Ndio" al/ibu Mtume, anamtukana baba wa mwingine ambaye humrudishia kwa kumtukania baba yake na anamtukana mama wa mwingine ambaye humrudishia tusi hilo kwa mama yake. (Bukhari na Muslim).
Umeionaje Makala hii.. ?
Post hii itakufundisha jinsi ya kumswalia mtume, pamoja na kuzijuwa fadhila unazopata kwa kumswalia Mtume
Soma Zaidi...DUA ZA KUONDOA WASIWASI, SIHIRI NA UCHAWI 1.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza maana ya hadithi al Quds na Hadith an-Nabawiy
Soma Zaidi...ADHKARI MBALIMBALI NA DUA Hapa tutajifunza dua mbalimbali ambazo ni adhkari.
Soma Zaidi...Hapa utakwendabkuijuwabhistoria ya uandishi wa hadithi. Pia utaijuwa sababu iliyopelekea uandishi wa hadithi kuwa mdogo .
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukufundisha namna ama staili ambazo Allah hujibu dua za watu.
Soma Zaidi...